Wadau mliofanikiwa kwenye Forex, kwa mpango wangu huu nami nitafanikiwa ama nitaangukia pua?

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Wakuu habari

Baada ya kutafakari kwa muda nimeona nijaribu forex trade, ndio inaweza kuniletea uhuru kamili, ambao nimekuwa nikiusaka tangu nizaliwe, kujiriwa niliacha kwa kukosa uhuru ila hata kujiajiri naona freedom yake ipo limited kwa kuwa kuna maamuzi ya serikali na mamlaka zake yananiathiri. Uzuri wa Forex ni hakuna hakuna bosi wala serikali

So baada ya kuchukua Kama mwezi hivi nikisoma, na kupitia charts kwenye MT4 nataka nianze demo kwa muda wa miei 6 hivi kisha nitafungua micro account na nita depositi dola 1000 kama pilot

Nikifanikiwa ku trade na kuongeza account iongezeke angalau kwa 50% au zaidi ndani ya mwaka Basi nitafungua mini account ya dola 10,000, lengo langu ikiwa Ni kuja ku trade kwa standard account ya dola 100,000

ila nimesikia 95% ya watu wanaoingia kwenye hii venture huwa wanafeli na ndio maana nikaanzisha huu Uzi kupata criticism na mapendekezo kutoka kwa watu waliofanikiwa.
nimejipanga namna hii ili nisiingie kwenye Hilo kundi la 95% Ila Kama una cha ziada changia kwenye comments

1. Wengi wanai treat hii Kama get rich quick scheme, mfano mtu kutengeneza dola 10,000 ndani ya mwezi kwa kianzio Cha dola 1000 tu au chini yake, japo Ni possible Ila Mimi Sina expectation kubwa hivyo, Niki double account yangu ndani ya mwaka itakuwa mafanikio makubwa sana kwani itakuwa return ya 100% kwenye uwekezaji ambacho ni exceptional kwangu, kwani uwekezaji kwingine unanipa return ya 20% tu kwa mwaka, hela ukiiweka Benki riba ni chini ya 10%

2. Kutaka mafanikio ya haraka ndio kunawafanya watu kuweka leverage kubwa Kama za 1:100 au zaidi ili ku trade na lot kubwa kwa mtaji mdogo, hii ni suicide. Mimi leverage niliyopanga itakuwa 1:5

3. Expectation kubwa zinakufanya ku trade hata kwenye setups ambazo hazina uhakika Sana.
Mimi nitakuwa na trade trend reversals kwenye 4hr na 1Day pair za USDCAD na NZDUSD , nimepitia chat zake kwenye MT4 nikaona hakuna signal fake nyingi lakini naweza kukaa hata mwezi au zaidi kabla ya kupata signal iliyokidhi vigezo nilivyoweka, kwenye timeframe za chini kama 30Min na 1Hr kuna signals nyingi lakini kuna fake nyingi sana pia, so ndani ya mwaka pengine naweza kupata trade hata 10 tu kwenye 4hr na 1Day..!

4. Mtaji mdogo, Kuna watu wanaanza ku trade hata na dola 100 au 50, hii inakufanya uwe under capitalized, wakati unatakiwa at most 2% ya capital yako ndio unaitrade
Mimi nitakuwa na dola 1000 ambazo nitakuwa na risk dola 10 Hadi 20 kwenye trade moja kwa kubalance lot size na pips zitakazokuwa kwenye stop loss

5. Watu wengi Hawa practice demo, watu kwa Sababu wanakuwa na mshawasha wa kutengeneza hela haraka unakuta hata Ile demo Hawa practice au Wana practice kwa muda mfupi na wala hawazingatii wananchojifunza huko, Mimi demo yangu itakuwa miezi 6 na Kama Nikiona mambo magumu basi Nita extend hata Hadi mwaka, sitaingiza hela kwenye account kama nikifeli demo


Hayo ndio machache niliyoyaona kwa haraka, pengine niki trade na demo nitagundua mengi zaidi, kama mkakati huu una matumaini ya juu sana au ya chini sana au kuna vitu ume miss niambie kwenye comments

Pia kama una suggestion ya broker mzuri niambie pia maan a nataka broker nitakyemtumia kwenye demo ndio huyo huyo nitamtumia kwenye real account
 

We ingia tu uje utupe mrejesho. Forex sio issue. Issue ni vidole vyako kubonyeza “sell” “buy” na “close trade” plus muda utakaokaa kusubiri. Hiyo Ndio forex.
Hahaa, kuzuia mihemko sio? Jambo dogo Sana kwangu. Mi nadhani wengi wanashindwa kuzuia mihemko kwa sababu Wana risk hela ambayo hawako comfortable kuipoteza
Unaenda kutoa savings zako karibu zote unacheza forex halafu unakuta huna kazi nyingine, nadhani hisia zitakuwa juu sana
 
Mkuu vitu muhimu ni proper risk management jitahidi tuu katika hilo ..set target your willing to lose set target ya unacho tarajia kupata kwa kila trade moja.”stoploss ni rafiki mzuri”

Jaribu kucontrol vitu vichache like fear of missing out itakupush kiasi mengine yapo sokoni
 
Ni rahisi sana kuongea na kuweka mipango kama hiyo, ila ukishaingia hautaweza kuvumilia kudouble akaunti kwa mwaka mzima wakati wenzako wanadownload pesa kila siku😂😂😂
 
Ni rahisi sana kuongea na kuweka mipango kama hiyo, ila ukishaingia hautaweza kuvumilia kudouble akaunti kwa mwaka mzima wakati wenzako wanadownload pesa kila siku😂😂😂
wenzako akinani wa kule instagrm au sijuakupata vizur
 
Back
Top Bottom