Wadau, hivi ni kwanini hasa Watu Wanaoana?

Wadau, hivi ni kwanini hasa Watu Wanaoana?

SJUMAA26

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
607
Reaction score
168
Baada yamjadala wenye hoja nzito nzito uliokuwa ukihoji na kudadisi kwa kina kamahabari za M(m)ungu ni za kweli au ni hadithi tu za watu wa mashariki yakati kuonekana kuisha, leo nimeamua kuleta kwenu mjadala unaotaka kudadavua kwakina sababu hasa zinazowafanya watu wengi kukimbilia kufunga ndoa!
Nimezungumzana wanandoa zaidi ya 20, wengi wao wamekuwa wakitoa sababu aidha za kufikirikaama za juu juu tu zinazozidi kuacha maswali mengi zaidi kuliko majibu! Kwamfano:- Mtu mmoja anadai alioa kisa ni agizo la Mungu (kupitia Biblia) likisemaBwana Mungu Aliona si vyema mtu (Adam) akakaa peke yake, hivyoakamfanyia msaidizi (Eva/Hawa) anayefanana naye. Mwingine akasema Munguameagiza hilo ili tuzae tuongezeke tukaijaze dunia! Wengine wakadai kwa binadamualiye kamili, sharti awe na mke/mme wake ili watimizianehaja za kimwili na hivyo kujiepusha na dhambi za uzinzi na uasherati! Cha ajabu zaidi, baadhi ya wanandoahawakuwa na majibu madhubuti zaidi ya kusema wamejikuta wameoana tu nabaadhi yao walisema ndoa ni kwa ajili ya hadhi na heshima katika jamii! Sasa binafsi, kwa sababu hizo chachetu, bado sijaona mantiki na sababu muhimu hasa zinazowafanya watu kukimbilia kuingiamikataba migumu kama ya ndoa, sasa hebu tujaribu kwenda pamoja:-
1. Mungu Anapodai si vyema mtuakakaa peke yake maana yake ni nini? Uzuri aliotaka kutuonyesha hapo ni upiiwapo tu hata mwanaye Yesu (ambaye pia inasemekana ndiye Mungu mwenyewe)hakuoa? Na pia hata Yeye mwenyewe (Mungu) hana mke? (Maana angekuwa na mkeasingeweza kuruhusu Yesu azaliwe na binadamu wa kawaida, au huyo Maria ndiyealikuwa wife wake) Sasa iweje kwake iwe vyema lakini kwa wengine si vyema?
2. Na kama swala lilikuwa ni kuzaa ilituijaze dunia, iweje sasa Mungu huyo huyo aumbe wagumba na watu tasa?Lakini pia, kwa maeneo kama China ambako idadi ya watu inazidi carryingcapacity ya eneo, hii hoja ya kuijaza dunia bado ina mantiki kweli? Na kamabado ina mantiki, iweje leo hii kuna kampeni zinazoendeshwa za Uzazi wa mpango,huku sio kuhujumu kwa namna Fulani lengo halisi la ndoa? (Manake Mungu mwenyewehakuweka kikomo cha idadi ya watoto wanaotakiwa kuzaliwa katika familia, sasahii imetoka wapi?)
3. Kama lengo ni kutimiziana haja zamwili, iweje leo wanandoa wengi ndio wanaoongoza kwa kutongoza na kuwa navimada & mahawara nje ya ndoa na wengine wakitafuna mabeki 3 wao na houseboys? Sasa kwa wanandoa wa namna hii (ambao naamini ni wengi sana) wana sababugani za kujionyesha kwa watu kuwa wako pamoja wakati bado wanaendeleza Uzinzina Uasherati kwa kwenda mbele?
4. Na kama ndoa ni kuleta hadhi katikajamii, inakuwaje kwa wanandoa ambao kila kukicha wako kwa wajumbe /wenyeviti wa mitaa, balozi tena na wengine wana migogoro kwa wazazi na hata kesimahakamani ili mradi ni vurugu na fujo tupu zinazofanya hata baadhi ya watotowazikimbie familia zao na kuwa machokoraa mitaani? Au hii ndio heshima na hadhiya ndoa?
Jamani, ngoja nisimalize uhondo wa mada yenyewe, kwawanandoa na watarajiwa, hebu toeni mawazo yenu hapa ili na sisi tunasema “badotupo tupo sana” tuweze kujifunza na hatimaye kufanya maamuzi sahihi na siyokudumbukia kwenye mikataba ya ulaghai inayoishia kwenye kesi na usaliti wa kilakukicha lakini tukijifariji kuwa tuko kwenye ndoa kumbe tumenaswa na ndoano!Karibuni!
 
Hii ndo digital mapenzi yamekuwa kama fasheni leo kwangu kesho kwako, mara nyingi wengi wanakua katika ndoa lakin wanatoka nje wakiamini bila nyumba ndogo ndoa haitadumu lakini wengi wao unogewa na penzi zito kwa nyumba ndogo hatimaye kunasa moja kwa moja.
 
Yap! Challenge nzuri sana!!!
Ngoja waje waliokwenye ndoa watupesababu zao!
...
Mimi single taririka kihivi;
Ndoa ni taasisi moja ambayo KILA ANAESTAHILI kutekeleza ni muhimu KIMWILI NA KIROHO!!!
Hizo changamoto ni lazima zitokee! Thus why tumepewa akili na maarifa kuliko viumbe wote!
Hata usipofunga ndoa bado utakuwa na changamoto nyengine!
...
Kuna mtu ali-define Maisha kihivi: Maisha ni Matatizo!
Hivyo basi tusipooana tutaishi kama wanyama!!!!!!!!!
Wewe ukiona hakieleweki tafuta mmama kuanzia miaka 40 na kuendelea uone utamu wa ndoa!
Mabinti wa bongo fleva tuachie tupige pige hivyo hivyo tu!!!!
 
Khaaa!!! hayo maswali yalivyo magumu mpaka nimeshindwa nianzie wapi! Ngoja nikapate lunch pengine akili itatulia kujibu walau mawili matatu!
 
Mimi siwezi kuwajibia watu wengine kwa nini walioa ngoja nijibu sababu zangu mwenyewe.
-Nilihitaji mwanamke nitakayempenda sana ili nimuonyesha upendo wangu nilio nao kwake kwa maana hiyo nilihitaji kuwa naye karibu aifurahie dunia ya Bwana ili nilipo naye aewpo.
-Nilihitaji kuwa na mtu nitakaye mwamini sana hata nisipokuwepo kama nipo,pia mwenye akili anayeweza waongoza wanangu kwenye maadili ninayojua mimi ni mema.
-Nilihitaji kiumbe wa kunijali sana kwenye raha ama shida.
-Nilihitaji kiumbe ambaye ningekuwa huru sana kwake naye huru kwangu kwa kila kitu isipokuwa yaliyo kinyume.
-Alihitajika wa kumega naye sakaramenti bila masharti kama yale ya viruka njia mara vocha,simu nk.ndo unaona anakenua mpaka gego la mwisho na mwaaaaa zisizo na idadi.
-Status ukiwa umeoa na unasimamia nyumba yako vyema kuna uzito wake ndo maana hujawahi kusikia rais asiye na mke.
-Kuwa na watoto mwanawane tutakaolea mimi na mama mtumishi kama Mungu akijaaaalia.......wana .....ni kama mishale mikononi mwa shujaa.
-Naogopa gonjwa la UKIMWI ndo maana nilihitaji mwaminifu hasa nashukuru Mungu alinipa kama nilivyotamani....atakupa msaidizi wa kufanana nawe.

Angalizo.
hizo ni zangu si lazima zifanane na za wengine kama kila ndoa haiwezi fanana na nyingine na sababu haziwezi fanana.
 
Khaaa!!! hayo maswali yalivyo magumu mpaka nimeshindwa nianzie wapi! Ngoja nikapate lunch pengine akili itatulia kujibu walau mawili matatu!

Kwa sisi waumini wa Kikristo hili swali rahisi sana rafiki...

Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Hivyo watu wanaoana ili kutimiza hilo agano, hakuna atayekuhimiza ila ni mtu kwa utashi wa nafsi na akili unaamua mwenyewe kuoa wakati ukifika.
 
Back
Top Bottom