Wadada wamcheka bibi akikata roho

Wadada wamcheka bibi akikata roho

Habari za asubuhi wana JF,

Leo nimekutana na kituko cha mwaka katika hospitali yetu ya mkoa wa Mwanza Sekoutoure. Nilienda kumjulia hali jirani yangu amelazwa. Pembeni yake kulikuwa na bibi ambaye alikuwa anatapatapa katika kumalizia kukata roho.

Yule bibi akawa ana lalama kwa lugha ya huku kwetu ya kisukuma akisema MAAYOO MAAYOO yaani MAAMAA MAAMAA, hapo wodini kulikuwa na mabinti wawili ambao anao walikuja kwa minajili ya kumsalimia mgonjwa wao.

Wale mabinti wakawa wanacheka wanamuangalia yule bibi anayetapatapa kukata roho, nikawaauliza mbona mnamcheka bibi wa watu? wakanijibu tena kwa kujiamini kabisa: "INACHEKESHA YAANI HAKA KABIBI NAKO ETI KANAVYOKATA ROHO KANAMTAJA MAMA YAKE"

Baada ya muda mfupi bibi aliaga dunia.

Sikuwasemesha tena hao wadada, zaidi ya kuwashirikisha wana JF wenzangu kuwa duniani kuna vituko!
labda ni watani
 
Inawezekana hivyo vibinti uchwara ndivyo vinavyomroga huyo bibi...ila wakumbuke nao siku yao yaja.
 
Kuna muda mwengine kuna baadhi ya vitu vinachekesha hasa pale unapovuta picha ya kile unachokiona, mfano hapo alikuwa akilia mayooooooo!! mayoooo!! Nafwaaaaa! alafu usikute sura yake imekaa kicomedy comed.
 
Wote tutapita katika njia hiyo huwez kufurahia mauti ya mwenzio binadamu tumekuwa na roho za ajabu sana ila mungu atawalipa hao mabiti unacheka mwenzako anakufa kweli ningelikuwa mm nisingewavumilia
 
Kwa nini alikuwa Analia?.Tujifunze kitu maana kuna wanaokufa taratiibu bila ya mizengwe na wanakufa kama huyu bibi.Mungu yupo na shetwani yupo pia. Endeleeni kumpinga Mungu huku mkimkaribisha shetwani . japo hawakupaswa kumcheka katu Bali kumuombea.
Ndugu,suala la kulia ktk utokaji wa roho ni la kawaida sana.
Mfano kuna siku nililala bahati mbaya chakula kikaingia ktk mfumo wa hewa havari yake sio ya kitoto ndugu masna pumzi zilikata kwa sekunde chache!
Nikavuta picha je roho ikiwa inatoka si ndio balas zaidi
 
Binafsi imeniuma sana sio kitendo cha kawaida, kweli binadamu tunatofautiana sana labda wao hawatakufa
 
kuna mazoea fulan kizaz hiki kipo kias kwamba kila kitu tunaona ni sawa tu
 
Mkuu hao mabinti hawakupata malezi mazuri.

Kama mwezi mmoja uliopita nilikuwa zahanati moja hivi. Mama mmoja akawa amelala chini na ukitizama hali yake ilikuwa sio nzuri. Nesi akashauri waliyemleta mgonjwa wambebe wampeleke kwenye chumba cha jirani. Wale ndugu zake au wanawe mmoja wa kike na mwingine wa kiume wakambemba lakini kutokana na uzito wa yule mama wakawa wanalemewa lakini baadaye wakambeba.

Kuna binti na mwanaume walikuwa wamekaa pembeni wakawa wanacheka jinsi yule mwanaume na mwanamke walivyokuwa wanahangaika kumbeba yule mama.

Nilisikitika sana hata nesi aliyeshauri yule mama abebwe aliwakemea sana.

Unapokuwa na watoto, washauri tangu wakiwa wadogo wasimcheke kilema au mtu aliyepo kwenye matatizo. Ila kama hukuwahi kushauriwa hivyo basi wazungu wanasema “You cannot reason someone out of something they were not reasoned into.”
 
Ndugu,suala la kulia ktk utokaji wa roho ni la kawaida sana.
Mfano kuna siku nililala bahati mbaya chakula kikaingia ktk mfumo wa hewa havari yake sio ya kitoto ndugu masna pumzi zilikata kwa sekunde chache!
Nikavuta picha je roho ikiwa inatoka si ndio balas zaidi
Hapo hukuwa unakufa ulikuwa uzembe wako tu. Vipi ushuzy hukukutoka?.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom