Wadada wa mujini na magari vp?

Wadada wa mujini na magari vp?

Wanashobokewa na viserengeti. ..

halafu hiyo avatar yako huwa inanichekesha sana. Inanikumbusha harakati za kina mama na finca za kunyang'anyana mito ya makochi. Marejesho haya yaache tu!
 
duh! kwa hiyo mnataka kabla hatujawashobokea tuanze na usaili kwamba gari ni la mkopo au la kuazima au la kampuni? kwani likiwa la sirekali au la kuazima halisevu papaz? Sisi gari ni gari tu ilimradi ujue kuzingatia muktadha (context). Si umeona wengine huko wanaponda vitz wakati mi nikiona hata nissan march macho yananitoka? By the way, hivi mtu akikopa hela akanunua gari inaathiri vipi umiliki wake? marejesho ya huo mkopo anakatwa bibi yake au? Kama hukopesheki nani atakupa huo mkopo? Basi huwa nawaangalia makonda na madereva wa daladala na wanadamu wengine wenye wivu wanavyowatukana wenye magari madogo "....toa kopo lako hapo wewe. Kopo lenyewe la mkopo.." Mie huo mkopo nautafuta ninunue phoenix sifikii vigezo. He! nshatoka nje ya mada. Sole

Mbona ya mkopo yapo wewe mwenyeo tu, unalipia mpaka laki 2 tu kwa mwezi waweza kuenda na wewe ili utembee na gari. kua na gari ni kitu cha kawaida sana huku mtaani kwetu na hakushobokei na kajigari chako
 
na wadada wenye magari wanawashobokea kina nani? au wao hawashoboki?

wadada wenye magari hawana haja ya kumshobokea mtu ila wenye kutaka watayatumia kama mtego wa kunasia mabuzi. kama ni kutimiza haja tu basi atampata mtu wa hadhi yake.
 
Ukitaka kuwakamata wenye uelewa mdogo huwa wanapenda sana magari ndo wanaona mtu labda tajiri

Hata wenye uelewa mkubwa, nimeshuhudia mdada kaunga masters lakini benebene kwa mwana anamkoko tu na pesa za kutumia, anasuuzwa kila kukicha....
 
mjini hapa. joto!!!

wengine kazi zetu za kukimbia kimbia, kupanda na kushuka ngazi siku nzima. we still want to smell fresh all the time. ndomana kuna sanitary breaks.

sasa nitoke kazini all fresh halafu nipande daladala kufuata mwanamume?? aaaahhh-pana.

Ndo maana mjini kuna watu kazi yao kukodi magari ili wawamege madem wenye mtizamo kama wako..............
 
Back
Top Bottom