Wadada, ni lini mliacha kufuma?

Wadada, ni lini mliacha kufuma?

Lukansola

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2010
Posts
5,435
Reaction score
1,611
Wakuu, kila mmoja apokee heshima kwa stahili yake. wenye mambo! haya, wale wa oyooo poa tu, wa shikamoo pia hali kadhalika.

hebu nipeni maoni yenu kuhusu ulikoishia utamaduni wa kina dada/mama kufuma.

kwenye kumbukumbu zangu bado ipo taswira ya kina mama waliofuma vitu kama soksi, sweta n.k.
Nakumbuka mama yangu alifuma. vitambaa vya meza na makochi nyumbani, hakuwa akinunua alifuma vyake, unakuta akiwa kajipumzisha baada ya kutoka kazini mdogomdogo anahesabu nyuzi hivyohivyo mpaka seti inakamlika.

Na si mama tu, bali hobby ilikuwepo sana zamani kuliko sasa.

Ni nini kilitokea hamfumi tena?
 
siku hizi mambo yamebadilika sana..........

nakumbuka hata zamani hizo mama alikuwa anafuma vitambaa lakin

mara ya mwisho kumuona anafuma tena sijui ni lini
 
Pia zamani nakumbuka wanawake walikuwa hawafugi kuku,hawapiki vitenge n.k
nadhani ni teknologia imekua
 
Marhabaa

Nilijua fumanizi kumbe kufuma

Ingawa mimi si ke naweza jaribu kutia mchango wangu hapa

Kwa kweli ilikuwa kama utamaduni fulani mtu akiwa hata kibaruani akipata muda wa bure anautumia vizuri kwa kufuma

Karne hii ya sasa nafikiri teknolojia imeathiri kwa kiasi kikubwa, imewafanya kina mama wawe bize sana na tamthilia, simu za mikononi, mambo yao sijui FB, IST, WHATSAPP na mengineyo mengi
 
ni majukumu tu yameongezeka maana umenifanya niikubuke sindano yangu ya kufumia sijui nimeitupia wapi..
 
mkuu mi nadhani kitu kikiwa hobby lazima utakipangia muda, huko kwenye mitandao si ndio wangeongeza ujuzi zaidi? au!
 
hahaha unaweza kufuma swate wewe! ila huu ni ujuzi wa hali ya juu sana nawavulia kofia rudisheni utamaduni huu please.
 
Mama yangu hadi leo japo si sana kama zamani akiwa amepumzika utamkuta anafuma mkoba au mkekma.....lakini wa dada wa siku hizi au wamama wakipata mda wa kupumzika huwa mara nyingi wanautumia kwenye Facebook,Jf,Twitter watapata wapi mda wakufanya mambo kama hayo ni ngumu sana..zamani walikuwa hawataki mda wao ukapotea bure.
 
Kwa kweli sijui nini kimetokea huu utamaduni umepotea kabisa,sidhani kama ni kuongezeka kwa majukumu kwani nakumbuka tukiwa wadogo mama alimudu kwenda kazini,kutuhudumia na kila akipata muda kidogo tuu utamuona anachukua sindano na bunda lake la uzi anaanza kufuma vitambaa
 
siku hizi mambo yamebadilika sana..........

nakumbuka hata zamani hizo mama alikuwa anafuma vitambaa lakin

mara ya mwisho kumuona anafuma tena sijui ni lini

mwambie mama akufundishe, uendeleze fani.
 
mkuu mi nadhani kitu kikiwa hobby lazima utakipangia muda, huko kwenye mitandao si ndio wangeongeza ujuzi zaidi? au!
Swali zuri umenikamata sana

Sababu mitandaoni nako unakuta ujuzi unaongezeka zaidi unaweza ukaona madesigner mbali mbali na baadhi ya kazi zao zikakushawishi

Kweli umenibana, tuwasubiri kina mama nao waje na michango yao labda inaweza kutusaidia zaidi
 
ila hata siku hizi nadhani ni wachche huwa wanatandika vitambaa vya kufuma kama zamani nakumbuka mama alikuwa anafuma kwa ajili ya makochi yake ya enzi zile ila siku hizi hakuna tena
 
Mama yangu hadi leo japo si sana kama zamani akiwa amepumzika utamkuta anafuma mkoba au mkekma.....lakini wa dada wa siku hizi au wamama wakipata mda wa kupumzika huwa mara nyingi wanautumia kwenye Facebook,Jf,Twitter watapata wapi mda wakufanya mambo kama hayo ni ngumu sana..zamani walikuwa hawataki mda wao ukapotea bure.

Hapo nyekundu naweza tetea mkuu, unajua unaweza jifunza vitu vingi, sababu kuna elimu kubwa sana hapa, pamoja na
wataalamu mbalimbali kuanzia WAPISHI, MAFUNDI, MADAKTARI , WAJASILIAMALI, WAFANYABIASHARA na mengineyo mengi yenye faida kubwa sana tofauti na kwenye hiyo mitandao ya jamii mingineyo

Ambayo ukichunguza kwa undani inakuwa inawachochea sana katika maswala ya kugegedana kwa asilimia kubwa
 
mkuu mi nadhani kitu kikiwa hobby lazima utakipangia muda, huko kwenye mitandao si ndio wangeongeza ujuzi zaidi? au!
Kama alivyochangia Heaven on Earth
Alafu siku hizi hata aina ya viti sebuleni imebadilika maana zamani utakuta sebuleni kuna ofisi chair, stuli na kochi zile za mito ya kuhamishika lakini siku hizi unakuta kuna sofa ambalo jinsi lilivyo tu tayari lina mapambo halihitaji swaga zingine pia meza unakuta ya kioo imenakshiwa vizuri kabisa nayo haihitaji kitambaa kama zile meza zetu za ngoma.

Kwa sweta na a soksi nadhani kuna haja a kuendelea na zoezi maana sweta zilikuwa kiwango aisee
 
Last edited by a moderator:
Swali zuri umenikamata sana

Sababu mitandaoni nako unakuta ujuzi unaongezeka zaidi unaweza ukaona madesigner mbali mbali na baadhi ya kazi zao zikakushawishi

Kweli umenibana, tuwasubiri kina mama nao waje na michango yao labda inaweza kutusaidia zaidi

Pole sana HARUFU, nami nasubiri niwasikie...

cc. Faiza Foxy
 
Hapo nyekundu naweza tetea mkuu, unajua unaweza jifunza vitu vingi, sababu kuna elimu kubwa sana hapa, pamoja na
wataalamu mbalimbali kuanzia WAPISHI, MAFUNDI, MADAKTARI , WAJASILIAMALI, WAFANYABIASHARA na mengineyo mengi yenye faida kubwa sana tofauti na kwenye hiyo mitandao ya jamii mingineyo

Ambayo ukichunguza kwa undani inakuwa inawachochea sana katika maswala ya kugegedana kwa asilimia kubwa
Nakubaliana na wewe hata mm nimejifunza mambo mengi sana JF na sikumaanisha kuwa labda huko wanako kuwa nako busy hakuna wanacho kipata hapana....Namaanisha kwamba tunauzika utamaduni wetu japo kwenye hii mitandao ya kijamii kila mtu anajifunza kwa jinsi anavyojua mwenyewe...Naiheshimu sana JF mkuu
 
Kama alivyochangia Heaven on Earth
Alafu siku hizi hata aina ya viti sebuleni imebadilika maana zamani utakuta sebuleni kuna ofisi chair, stuli na kochi zile za mito ya kuhamishika lakini siku hizi unakuta kuna sofa ambalo jinsi lilivyo tu tayari lina mapambo halihitaji swaga zingine pia meza unakuta ya kioo imenakshiwa vizuri kabisa nayo haihitaji kitambaa kama zile meza zetu za ngoma.

Kwa sweta na a soksi nadhani kuna haja a kuendelea na zoezi maana sweta zilikuwa kiwango aisee

mkuu hapo kwenye meza ya ngoma nimecheka sana nazikumbuka.

sweta noma mkuu, fikiria mtu anapanga nyuzi mpaka sweta Linatokea.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe hata mm nimejifunza mambo mengi sana JF na sikumaanisha kuwa labda huko wanako kuwa nako busy hakuna wanacho kipata hapana....Namaanisha kwamba tunauzika utamaduni wetu japo kwenye hii mitandao ya kijamii kila mtu anajifunza kwa jinsi anavyojua mwenyewe...Naiheshimu sana JF mkuu
Ubarikiwe mkuu pamoja sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom