Wadada mnadanganywa, umri ukienda mnaanza stress zenu

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,917
11,799
Kuna tukio limenitokea leo kuna mdada miaka kama 28+ nimemkuta kwenye mgahawa anakunywa chai alivyoonekana ni kama alikuwa na kitu kinamchanganya pamoja na hasira alipomaliza kunywa chai akatoka haraka huku akiacha simu pale mezani.

Nikatoka nje kumuita akanitukana nikachukua ile simu nikapanda gari nikaondoka nimefika nyumbani akanipigia simu nikamwambia njoo maeneo fulani uchukue simu yako alipofika ndipo akanieleza sababu hasa ya kuwa na hasira anadai kuwa amekuwa na uhusiano na wanaume wawili kwa vipindi tofauti ambao walimuahidi watamuoa lakini wanaishia kumumwaga na anavyoona umri unaenda na amekataa wanaume wengi waliokuwa wana nia ya kumuoa hali imepelekea kuchukia wanaume.

Hali kama hii huwapata wanawake wengi unakuta binti yupo kwenye form yake anawakataa watu wenye nia ya dhati ya kumuoa kwa kigezo kwamba ana mchumba mwisho wa siku anamwaga na umri unakuta umesonga presha toka kwa wazazi unakuwa mwanzo wa stress na kujipeleka kokote kule ili mradi tu aolewe.

Wadada shtukeni.
 
huwa wananisikitishaga sana wadada wa hivi yaan huwa nawaonea huruma sana
kila siku nawaambia mwanaume anayekupenda kweri lazina atangaze ndoa

sasa mkuu molembe si ungemuoa tu au wewe ushavuta jiko tayali
Mkuu mimi tayari
 
teh teh....

ujumbe mzuri....ila ni wagumu kukuelewea mkuu....


ngoja waje..
 
Endelea kusubiri.
Ukuchukua no yke mkuu ningemsandia natafta mke wa kuoa lkn awe anajitmbua yeye ni nan
Mkuu sikuchukua namba yake ila yeye amechukua yangu kwa kigezo kwamba atanitumia chochote kwa uungwana wangu, kwa kweli ukipata mke kama yule unakuwa umepata mke anayejitambua sio hivi vichenchede vya miaka 18~25 visumbufu sana.
 
Back
Top Bottom