Wadada kuweni makini na ofa

Wadada kuweni makini na ofa

Uta Uta

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2016
Posts
3,743
Reaction score
8,802
Wadada hasa wa mjini wanapenda sana ganda la ndizi. Unakuta dada hata kama anao uwezo wa kununua kinywaji hanunui anasubiri tu ofa ili hela yake ikae tu isitumike.

Sasa jana kuna dada mtaani kapoteza simu kila anaemuuliza umeibiwaje anajibu kisanii sanii, ukimhoji zaidi anakuwa mbogo balaa unajua tena dunia haina siri.

Kumbe dada yule aliingia mkenge kwa tapeli mmoja maarufu kwa njia ya ofa. Huyo jamaa anatafuta wadada wazuri anakupa ofa ya kula na kunywa kama siku mbili siku ya tatu anachukua chumba guest anakuwekea madawa katika kinywaji, anakula mpaka jicho halafu anakuibia kila kitu kisha anasepa.

Sasa dada yule alikutwa na jamaa asubuhi guest aking'ang'a macho keshaliwa jicho na jamaa kasepa na kila kitu. Dada hasira zake anatumalizia sisi mtaani.

Wadada kuweni makini na ofa hizo
 
"Ukitaka kula kidogo kubali kuliwa, sasa wewe unataka kula tu bila kuliwa? Haiwezakani hata kidogo"- Jakaya M. Kikwete
 
Wadada hasa wa mjini wanapenda sana ganda la ndizi.
Unakuta dada hata kama anao uwezo wa kununua kinywaji hanunui anasubiri tu ofa ili hela yake ikae tu isitumike. Sasa jana kuna dada mtaani kapoteza simu kila anaemuuliza umeibiwaje anajibu kisanii sanii, ukimhoji zaidi anakuwa mbogo balaa unajua tena dunia haina siri
Kumbe dada yule aliingia mkenge kwa tapeli mmoja maarufu kwa njia ya ofa.
Huyo jamaa anatafuta wadada wazuri anakupa ofa ya kula na kunywa kama siku mbili siku ya tatu anachukua chumba guest anakuwekea madawa katika kinywaji, anakula mpaka jicho halafu anakuibia kila kitu kisha anasepa.
Sasa dada yule alikutwa na jamaa asubuhi guest aking'ang'a macho keshaliwa jicho na jamaa kasepa na kila kitu. Dada hasira zake anatumalizia sisi mtaani. Wadada kuweni makini na ofa hizo
Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna uoga kulingana na tamaduni zetu za kiafrika ndizo zinazolealea hizi tabia mbovu za wanaume. Huyo Dada akiamua kumfatilia kwa kusema wazi yaliyotokea jamii itamuona wa ajabu lakini ndo itakuwa mwanzo wa mwisho wa huu upumbavu.

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Harudii tena huyo. Bora lakini yamezidi mterezo haya majitu( baadhi lakini).

Bomba Mvua
 
Kama wewe mdada chukua tahadhari, hapa tunapashana tu updates za mjini kwa hiyo ukishaisikia unachukua tahadhari
Mimi mwanaume, nimeuliza kwa kuwa lengo lako ni tahadhari bhas taarifa ziwafikie walengwa kwa usahihi...wajue sehemu flani kuna kadhia hiyo..

Hapo utakuwa umewachanganya na kuwapoteza. Tutashindwa kunywa now juice kisa tu hofu za kudhulumiwa Utu wao na kuibiwa. Toa code.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom