Wadada hawajui kula na kipofu

Wadada hawajui kula na kipofu

kasuagatz

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2021
Posts
288
Reaction score
360
Wasalaaam wana jukwaa.

Hivi wanawake ni viumbe vya ajabu sana sababu hawajuwi kula na vipofu kama kichwa cha maada hapo.

Ipo hivi, mfano umemtongoza kabla hajakupa jibu amekubali au la anakupiga mzinga, kitu ambacho kinamuumiza kila mwanaume kuombwa vitu visivyo msingi. Kwani kabla yangu ulikuwa ukiishi vipi? Umemtokea tu unaombwa vocha, mara gesi imeisha, mara kusuka, inatia hasira.

Kitu mbacho hawajui ni kuwa, omba omba unamwambia mtoke anataka umtumie nauli basi hata ukimtumia hiyo nauli anaishia kulia tu na hatatokea eneo la tukio. Wakati angekuja kwa nauli yake angekuwa kachukua pointi 3 zote muhimu.

Sababu ukija na nauli yako siwezi nikakuacha sijakupa chochote, ni uongo lazima kujiongeza nikupe nauli. Mnafeli sana aisee kwenye suala hili la kuwa omba omba.

Badilikeni, hakuna mwanaume atavumilia ku date na mwanamke hana hata vocha ya buku mbili!

Asanteni.
 
Back
Top Bottom