WaCongomani waisifu Tanzania leo kanisani Mbezi Beach.

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,356
26,516
Wakati mwingine kanisani mtu unapata kujiona jinsi unavyoonekana kimataifa.
Leo kanisani Mbezi Beach KKKT, kulikuwepo na ugeni wa kwaya toka Congo iitwayo CPCA Couples Shalom Coir toka Goma Congo.
Kivutio cha kwaya hii ni kwamba ni ya watu walio katika ndoa, yaani mtu na mke wake kama couples kumi hivi.

Wameimba wimbo mmoja wakiisifu na kuishukuru Tanzania , Rais na watu wake , kwa amani waliyo nayo na kuendekeza uhusiano mzuri uliopo kati ya Congo na Tanzania.
Huu wimbo waliimba wakiwa wana mshukuru Mungu kwa uhusiano wa amani uliopo.
it was moving!
Nilikaa karibu na mzee mmoja na niliona akilengwa lengwa na machozi.

Wimbo mwingine ulikuwa juu ya upendo wa mke/mume wakiimba pamoja kimahaba, burudani tosha.

Kwa kweli siku ya leo hawa waCongo wameiweka nuru siku yangu.
God Bless.
 
amina.. nimefarijika. Kama sisi hatuoni thamani yetu wapo wanaoona.
Utukufu, sifa, heshima Ziende kwa Mungu
 
Back
Top Bottom