Wachungaji sasa wameamua kula kondoo

Wachungaji sasa wameamua kula kondoo

Kanyafu Nkanwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2010
Posts
850
Reaction score
103
Zamani wachungaji walikuwa wanawalinda na kuwaongoza kondoo. Siku hizi wameamua wenyewe kuwala kondoo

Mwalimu mbaroni kwa rushwa ya ngono

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), mkoani Iringa inamshikilia mwalimu wa shule ya sekondari Pomerin iliyoko Wilaya ya Kilolo mkoani hapa, Michael Ngilangwa kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wake anayesoma kidato cha kwanza shuleni hapo.

Kaimu kamanda wa taasisi hiyo, Gasto Mkono, aliiambia Tanzania Daima kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 12, mwaka huu, majira ya saa 6 usiku katika nyumba moja ya kulala wageni mjini hapa, baada ya mwalimu huyo kuwekewa mtego mkali na maafisa uliowekwa na taasisi hiyo.

Alisema mwalimu huyo aliomba rushwa hiyo ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza (jina limehifadhiwa) kwa madai ya kumsaidia kufanya vizuri katika somo la Kingereza ambalo mwanafunzi huyo alikuwa akifeli mara kwa mara pamoja na kumsaidia fedha za matumizi madogo madogo.

Hata hivyo, alisema kutokana na hali hiyo mwanafunzi huyo alitoa taarifa TAKUKURU na kuweka mtego ambao ulifanikisha kumnasa mwalimu huyo na mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
 
Tukiwa bado tunashangaa adhabu aliyopewa mchungaji mwingine kule Singida ya miaka 30,tunapata habari za mwingine huko Iringa. Hii inaonyesha jamii yetu ilivyooza ktk maeneo mengi.

Mimi ninaamini kwa sasa,unaweza kuwa salama ukikutana na simba aliyeshiba kuliko kukutana na mwanadamu aliyeshiba. Kwa sababu mwanadamu aliyeshiba hutumia nguvu zake vibaya.
 
Hata hivyo, alisema kutokana na hali hiyo mwanafunzi huyo alitoa taarifa TAKUKURU na kuweka mtego ambao ulifanikisha kumnasa mwalimu huyo na mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika nyumba hiyo ya kulala wageni.

Akithibitishwa kwa uozo wake huyo mwalimu na mchungaji, akaozee jela!!!

BTW Kanyafu, umeandika kwenye title ya thread 'wachungaji'. Kwenye habari yenyewe naona ni 'mchungaji', hao wengine ni wapi na matukio yao ni yepi hayo??
 
Nadhani huyo ticha si salama kabisa, rushwa ya ngono siku hizi hakuna kabisa maana dunia imebadilika. Angemwana sera zake ipasavyo wala haya yasingemkuta, angekula kondoo wake kiulaini kama ananawa na maji ya sabuni.
 
Kila mtu ana 'weekness' zake. naye huyo ndo zake. biblia inatukumbusha kuwa tusihukumu. Kwani wafalisayo walipeleka mke aliyekuwa amezini kwa Yesu, Bwana yesu akawaambia kuwa, 'kama kuna mtu ambaye hajawahi kufanya dhambi na awe wa kwanza kumrushia mawe' wote walitoweka! Huyo mchungaji si wa kwanza kufanya hivyo. Nadhani labda tumwombee ili naye ajifunze kupangilia maombi yake kwa mademu wampe kwa makubaliano na kila mtu 'afaidi mapenzi'.
 
Akithibitishwa kwa uozo wake huyo mwalimu na mchungaji, akaozee jela!!!

BTW Kanyafu, umeandika kwenye title ya thread 'wachungaji'. Kwenye habari yenyewe naona ni 'mchungaji', hao wengine ni wapi na matukio yao ni yepi hayo??

Anawakilisha.
 
Back
Top Bottom