Wachumi watoboa Shilingi kuwa hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachumi watoboa Shilingi kuwa hoi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, May 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Wachumi kadhaa wameelezea sababu tofauti za Shilingi ya Tanzania kutokuwa imara na kuporomoka thamani mara kwa mara.
  Katika uchunguzi wa Nipashe ambao umefanywa kwa takribani wiki mbili sasa kwa kuuliza wachumi pamoja na maofisa waandamizi wa serikali juu ya kuporomoka kwa kasi ya kutisha ya sarafu ya Tanzania, pamoja na mambo mengine ni kuendelea kwa manunuzi mengi ya huduma na bidhaa kufanywa kwa dola kuliko shilingi.
  Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Donath Olomi, alisema moja ya sababu zinazochangia kuporomosha thamani ya shilingi ni manunuzi makubwa ya nje yasiyoendana na mauzo nje ya nchi, mikutano ya kimataifa kufanyika hapa nchini na safari za viongozi nje ya nchi.
  Kwa mujibu wa Dk. Olomi, ili kuimarisha thamani ya Shilingi, lazima manunuzi nje ya nchi ambayo sio ya lazima yadhibitiwe na kuhakikisha kwamba huduma mbalimbali nchini zinalipiwa kwa shilingi badala ya Dola.
  Alitoa mfano kwamba huduma kama za hoteli zinapaswa kulipiwa kwa shilingi badala ya dola ili kulinda thamani ya shilingi.
  Kwa upande wake, Dk. Haji Semboja, mhadhiri wa uchumi chuo kikuu hicho, alisema Shilingi inapoteza uimara kutokana na Dola ya Marekani kununuliwa kwa fedha nyingi za Kitanzania tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.
  “Ushindani mdogo na mataifa mengine katika kuelekea kwenye maendeleo ndiyo sababu kubwa iliyosababisha kuporomoka pesa yetu,” alisema Dk. Semboja.
  Kadhalika, alisema kuwa mauzo duni ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi ni sababu nyingine inayochangia kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
  Alisema njia inayoweza kunusuru hali hiyo ni pamoja na nchi kuendelea kuzalisha bidhaa nyingi na kuongeza mauzo ya nje ili kupata fedha za kigeni.
  Njia nyingine inayoweza kusaidia kumaliza tatizo hilo, kwa mujibu wa Dk. Semboja ni kuongeza mauzo ya dhahabu na madini mengine yaliyopo nchini ili kulipatia taifa fedha za kigeni.
  Aidha, alisema fedha zinazotolewa na wahisani wa nje kusaidia shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali nazo kwa kiasi kikubwa zitasaidia kuondoa tatizo hilo.
  Kwa upande wa athari ambazo zimeanza kuonekana kutokana na kuporomoka kwa shilingi, Dk. Semboja alizitaja kuwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za petroli na dizeli.
  Dk. Semboja ambaye pia amekuwa akifanya kazi za utafiti na ushauri katika taasisi kadhaa ikiwemo Repoa, alishauri serikali kuchukua tahadhari kabla hali hiyo haijaleta athari zaidi.
  Naye Dk. Deo Mushi wa chuo hicho, alisema uuzaji nje wa mazo ya kilimo kwa wingi unaweza kuinusuru shilingi ya Tanzania.
  Hoja hiyo iliungwa mkono na Theo Mushi, mchambuzi wa masuala ya uchumi na mkazi wa jijini Dar es Salaam, ambaye alisema kuwa kwa kipindi hiki ambacho ni cha msimu wa kilimo cha mazao ya biashara ya asili hali hiyo hutokea.
  Mushi alisema shilingi inaweza kuimarika ifikapo Agosti ambapo mazao hayo yataanza kuuzwa nje.
  Lakini alionyesha wasiwasi kwamba mwaka huu ni wa uchaguzi, kuna uwezekano wa kuwepo na njama za wajanja kuchapisha fedha kwa ajili ya kampeni za kisiasa na hivyo kuchangia kuporomosha thamani ya shilingi.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ni mchumi kitaaluma, alisema kushuka kwa thamani ya shilingi kunatokana na uingiaji wa fedha za kigeni kuwa mdogo kuliko mahitaji.
  Alisema athari yake ni kupanda kwa bei ya bidhaa za nje na hivyo kusababisha gharama ya maisha kupanda.
  Kuhusu taarifa za kuwapo kwa fedha kwenye mzunguko ambazo hazitokani na uzalishaji, Profesa Lipumba alisema, hali hiyo inawezekana na mara nyingi husababishwa na wauzaji wa dawa za kulevya kwa vile hawazalishi wala kulipa kodi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, alisema kushuka kwa Shilingi kunategemea na uzalishaji na alisema hali hiyo si kitu cha ajabu.
  Kuhusu kuwapo kwa fedha kwenye mzunguko ambazo hazitokani na uzalishaji, Khijjah alisema bado haijathibitika ingawa inawezekana kuwapo. “Tuna chombo chetu cha kuratibu fedha haramu. Bado kinaendelea na uchunguzi wa suala hilo.”
  Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu, alithibitisha kushuka kwa thamani ya Shilingi ukilinganisha na Dola ya Marekani.
  Hata hivyo, alisema Shilingi imeimarika kwa kiasi kikubwa zaidi kulinganisha na Euro na Pauni ya Uingereza.
  “Thamani ya Shilingi imeshuka ukilinganisha na Dola ya Marekani, lakini Shilingi imeimarika kwa kiasi kikubwa zaidi ukifananisha na Euro na Pauni ya Uingereza,” alisema Profesa Ndulu alipozungumza na Nipashe.
  Gavana alisema kama ilivyokuwa kwa sarafu nyingine maarufu, kama vile Euro na Pauni, kushuka kwa thamani ya Shilingi kwa kiasi kikubwa kunatokana na kuimarika kwa thamani ya Dola ya Marekani ili kuboresha matarajio ya faida, ambayo yamepunguza kasi ya kukuza mikopo.
  Alisema kwa miezi 10 iliyopita, BoT imekuwa ikiuza wastani wa Dola milioni 80.
  Kuhusu taarifa za kuwapo kwa fedha kwenye mzunguko ambazo hazitokani na uzalishaji, kama wa viwandani na huduma, Profesa Ndulu alisema uwingi wa fedha za Tanzania umezingatia viwango walivyokubaliana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuwa vinalingana na mahitaji nchini na siyo zaidi.
  “Ujazi wa fedha unaendana na mahitaji ya ubadilishanaji katika biashara ya bidhaa na huduma,” alisema Profesa Ndulu.
  Alisema uzalishaji siyo bidhaa tu ila pia huduma kama afya na elimu, ambazo zinahitaji vitendea kazi, malipo ya mishahara, dawa, vitabu nakadhalika.
  “Vyote hununuliwa na kuuzwa kwa kutumia fedha,” alisema Profesa Ndulu na kuongeza kuwa utaratibu uliopo ni wa kuhakikisha kuwa ujazi wa fedha taslimu hauzidi mahitaji na kwamba vigezo maalum huwekwa kupima hali ya ujazi wa fedha usiozidi viwango vya mahitaji yanayoendana na juhudi za kudhibiti mfumuko wa bei.
  Gavana alisema kwa miaka mitatu sasa, viwango havijavukwa na kwamba IMF wameipasisha Tanzania kila wanapokuja kufanya tathmini ya kuzingatia viwango hivyo.
  Alisema kazi ya msingi kabisa ya BoT ni kuhakikisha kuwa viwango hivyo havivukwi kwa kutumia nyenzo na sera mbalimbali chini ya mamlaka ya hapa nchini.
  Imeandaliwa na Muhibu Said, Richard Makore na Restuta James.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Embu kwanza watanzania wanaolipwa kwa shillingi wagome kutumia huduma au kwenda sehemu zinazo charge in dollars for six month alafu tuone kama kuna any special measures needed. The situation is fuelled by Tanzanians themselves accepting and using these services that demand dollars. Tatizo sehemu kubwa au za mbwembwe watu wenye mapato mazuri nao huzitumia kwa wingi hivyo kubidi ku-convert sh/ into dollars along the way fuelling the demand. As a result the price of dollar soars.

  Its simple cut their supply of profit in dollars (not using the services) wenyewe watahiitaji hiyo shilling ni kuamua tu, kwani na nyie mnawaendekeza, you follow their demands ndio maana mna ishia kuumia. Obviously mtakuwa mna nunua dollars kwa wingi na kwa mujibu wa BoT they haven't got enough to satisfy the demand kila siku itapanda bei kwa mtaji huo. Kwa sababu jamaa faida ni ugenini hivyo kuzidi kupunguza seculation inayoitajika. BoT as to fill the gap all the time apparently its becoming too much for them and a chore.
   
Loading...