A
Anonymous
Guest
Siku chache baada ya kutitia kwa Mgodi ya dhahabu wa Ikinabushu, Wilaya ya Bariadi Mkoani na kusababisha vifo vya wachimbaji 22, kuna mapya yameibuka ambayo ni nyuma ya pazia ya kilichotokea kabla na baada ya tukio hilo la Jumapili Januari 14, 2024.
Baada ya tukio hilo Serikali ilitangaza kutoa siku 6 kwa Wachimbaji wa eneo hilo kukamilisha taratibu za kisheria ikiwemo usajili na kufuata kanuni ya uchimbaji salama.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde aliongoza kikao kilichohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda na mbunge wa Bariadi, Mathew Kundo, ambapo uamuzi uliotolewa ni kutoufunga mgodi huo bali ukaguzi utafanyika na taratibu za kiusalama zikiwa sawa shughuli zitaendelea kama kawaida.
Ukweli umefichuka, Mgodi ulifungwa
Taarifa za uhakika ni kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, Afisa Madini wa Mkoa wa Simiyu alifika eneo husika kufanya ukaguzi kisha akatoa maelekezo kuwa mazingira si salama, hivyo akaagiza shuhuli zote zisimamishwe hadi kutakapofanyika maboresho ya kuweka usalama.
Baada ya maelekezo hayo eneo likazungushiwa utepe wa kuwa halitumiki na Maafisa wakawekwa kulinda.
Wachimbaji waliukaribia mwamba wa dhahabu
Inadaiwa wakati zoezi la usitishaji shughuli za mgodi likifanyika, Wachimbaji walikuwa wameukaribia kwa ukaribu kabisa mwamba wa dhahabu, hivyo kusitishwa kwa kazi ilikuwa imewaumiza wengi hasa wenye mashimo na wasimamizi.
Mchezo mchafu wafanyika usiku mwingi
Usiku wa kuamkia Januari 14, 2024 Wasimamizi wa Mgodi kwa kushirikiana na Wamiliki wa Mashimo wakapanga mpango wa siri kuendelea na uchimbaji wa madini ili angalau wapate chochote kutoka kwenye mwamba wa madini.
Inadaiwa wakawakusanya vijana zaidi ya 20 wakawaandikisha majina wakiwataka waingie kwenye mashimo huku wakiwaahidi dau nono watakapotoka.
Zoezi hilo likafanyika usiku wa Saa Saba na Nusu Usiku, wakachimba na kufanikiwa kukukusanya mifuko zaidi ya 22 ambayo ilikuwa imeshatolewa na ipo juu kwenye ardhi.
Ilipofika majira ya saa kumi alfajiri ndipo ghafla udongo ukaanza kutitia na mashimo kufukiwa na kuwafukia wachimbaji waliokuwa chini.
Shuhuda anasema wanaficha
Shuhuda ambaye alikuwepo eneo la tukio anasema “Hakuna Mchimbaji aliyevamia, pesa ilitembea, wale vijana wachimbaji hawawezi kuingia shimoni ndani bila ruhusa ya wenye mashimo au wasimamizi.
“Kinachofanyika Wasimamizi wa Mgodi wanaficha kilichotokea kwa kuwa hayo ni makosa yao wao, wao ndio waliosababisha mauti ya wale watu na inawezekana idadi ni kubwa zaidi ya waliopoteza maisha.”
Wanaficha ukweli
Ili kuficha siri, inadaiwa Maafisa wa Serikali wakiulizwa wanasema Wachimbaji walivamia usiku na kuingia kwenye mashimo kwa nguvu.
"Wale vijana hawana nguvu hiyo ya kuweza kuvamia na kuingia kwa nguvu, Maafisa wa Mgodi wanaficha kilichotokea kwa kuwa wanajua walichokifanya, wao ndio sababu ya maisha ya watu kupotea na wanakaa kimya wakijua hakuna anayejua siri yao," anasema shuhuda mwingine.