Tangu nimeanza kufatilia soka la bongo,mwaka 1990,sijawahi kusikia mchezaji kutoka yanga akishinikiza kwenda simba,bali nimeshuhudia wa simba wakingangania kuvaa uzi wa YANGA tena wakiwa kwenye kiwango cha juu,mfano,Hamisi gaga,method mogela,zamoyoni mogela,athumani idi,saidi maulidi,CALVIN YONDAN..Ngasa nae hana raha na azam,Bahanuz nae aliwachomelea simba,akawaambia nataka kuchezea timu niipendayo (yanga).Simba wamekuwa wakiambulia magalasa tu kutoka yanga,au waliofukuzwa kwa utovu wa nidhamu...
yawezekana ni kweli wewe umeanza kufuatilia mpira miaka ya karibuni lakini pia yawezekana wewe si mjuaji wa mpira na wachezaji kihivyo. Awali ya yote tambua wachezaj hawachezi kwa kufuata mapenzi bali wanacheza wa kufuata maslahii, ni wachezaji wachachesana wanaohamia timu flani sbabu tu ya mapenzi, ila wengi ubaki timu ileile hata kama siyo wanayoipenda iwapo malipo wanayopaa yatakuwa yanaridhisha
ngoja nianze kukupa mifano ya wachezaji waliohama yanga kwenda simba kufuata mapenzi na si pesa na hawa walisajiliwa almost bure kwakuwa walikuwa na mapenzi ya simba 1, ezekiel grayson 'jujuman' huyu alikuwa yanga akakata kuendelea kucheza akaamua kwenda Simba, 2, kuna mbunge wa sasa wa kilombero ccm, Abdul Mteleta , huyu naye aliondoka yanga kwenda simba kufuata mapenzi na si pesa
kuna wachezaji walioondoka yanga kwenda simba kwa pesa lakini hawa pia walikuwa na mapenzi na simba, mfano thomas kipese, steven nemes, godwin aswile, athumani china, n,k
kuna wachezaji walibaki kuchezea yanga muda mrefu lakini hawa walikuwa na mapenzi na simba, wengine hawakupata bahati ya kusajiliwa simba si kwa sababu hawakuwa wazuri bali simba walikuwepo wachezaji wazur zaidi au pesa walizokuwa wakipewa na yanga ziliwatosha mfano yusuph macho 'musso' alichezea sana yanga baadae ndo akaenda simba japo ni mpenzi mzuri wa simba, wengine ni kama ivo mapunda, shadrack nsajigwa, abdul mtiro, n,k
pia kumbuka hawa ni wachezaji ambao tunawajua lakini kumbuka hata huyu yondani pia inadaiwa ni simba kwani familia yao yote ni simba na hata yeye alipata kusea atakapokuwa yanga washabiki wanaweza kuwa na wasiwasi nae kwambaakifanya makosa anafanya kwa kuwa yeye ni simba damu