Wachezaji 15 wafariki Nigeria

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054

Wachezaji 15 wa soka la kulipwa nchini Nigeria wamefariki dunia baada ya basi lao walilokuwa wakisafiria kupinduka.

Wachezaji 15 wa soka la kulipwa katika timu ya FC Jimeta ya Nigeria wamefariki dunia baada ya kupata ajali katika mji wa Akwanga nchini humo.

"Timu ilikuwa ikisafiri kuelekea Abuja kwaajili ya mechi ya ligi ya Nigeria" alisema Mohamed Sanusi mkuu wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF).

"Basi lao lilipata ajali baada ya kugonga mwamba na kupinduka ambapo wachezaji 11 walifariki papohapo na wengine wanne walifariki hospitali. Wakati huohuo wachezaji wawili hali zao wamelazwa hospitali na hali zao ni mbaya ".

Timu hiyo ilikuwa imepangwa kucheza na timu ya Prisons FC ya Abuja.

Mwezi disemba wacheza soka wanawake 18 walifariki baada ya basi lao walilokuwa wakisafirisha.

Habari hii nimeitoa NIFAHAMISHE
 
Last edited by a moderator:
Ajali kama TZ. Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi. Amen.
 
Mungu awalaze mahali pema peponi Amina.

Hii habari inanikumbusha kikosi cha Zambia kilichoteketea akabaki Bwalya peke yake, kama sikosei...very sad
 
Back
Top Bottom