Wacheza pool watiwa mikononi mwa polisi

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Tamko la Rais limeanza kutekelezwa kwa vitendo kwa kukamata vijana mtaani na kuwalisha ugali wa bure Keko.

Nimepata habari hizi mtaani kuwa polisi na walinzi shirikishi/sungusungu wamekamata vijana na kuwapeleka vituo vya polisi.

Naamini huu ni mradi wa Polisi kutengeneza hela kwa kukamata vijana wasiokuwa na kazi kwakuwa hakuna mazingira yaliyoandaliwa kuwawajibisha hao wanaowakamata zaidi ya kuitia gharama serikali za kuwalisha chakula cha bure.

Vizuri kauli ya Rais iandaliwe mazingira ya kutekelezwa kabla ya kukurupuka kuitekeleza wakati matokeo yatakuwa hasi kwa serikali.
 
Acha kuongopea watu. Site ipi inatafuta watu niwapeleke ndugu zangu? Mm ni fundi lakini kazi hazipatikani. Acheni undezi kuongea vitu ambavyo hamvijui. Wewe kila siku upo kwenye kiyoyozi, unawaongopea watu
Naongea na mafundi wengi hawana kazi,wauzaji vifaa vya ujenzi mauzo yameshuka watu hawajengi hela hamna.huyo jamaa hajui maisha halisi ya mtaani
 
Naamini mkuu.mtaani kunanuka njaa.kwenye Bar wateja kwishnei
 
Back
Top Bottom