Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,745
- 5,446
Hizi tabia za wachambuzi na watangazaji wa michezo vya asubuhi kwa Wasafi FM na E FM kuchanganya lugha za Kiswahili na Kiingereza linakera sana. Kwanza wengi wao hata Kiingereza hawujui, wanachanganya 'tenses' na kwa anayejua Kiingereza masikio yanawasha na kwa wale wanaojifunza Kiingereza wanaishia kupotoshwa.
Tabia hii wamekuwa nayo kwa muda mrefu sana, hasa baadhi yao kwenye Wasafi FM. Kama mnataka kuchanganya lugha ili muonekane wajuvi basi jifunzeni kwanza lugha yenyewe kabla ya kuja 'kuchapia' mkiwa hewani. Au basi jifunzeni kwa Jeff Lea, ambaye akiamua kuchokea Kiingereza anakuwa anaitumia kwa kwa misemo murua na sahihi ya kugha hiyo.
Tafadhalini sana, mjiepushe kutumia maneno ya Kiingereza ambayo mnachanganya 'tenses' na kuishis kujidhalilisha ninyi wenyewe na redio zenu.
Vv