Kwanini nividharau Vipindi vyote vya Michezo vya Redio, Watangazaji na Wachambuzi wa Michezo Tanzania?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Walichokuwa wakisema Wiki Moja kabla ya Kucheza na Congo DR leo na kupokea Kichapo cha Kishalubela ( Kikatili ) ni.....

"Congo DR ya sasa si lolote na chochote kwani Wachezaji wao wengi tunawajua na tunao hapa Tanzania. Congo DR watakufa kwa Mkapa na Kipigo Kwao hakikwepeki kwani kwa sasa Tanzania tuko vizuri na tuna Kikosi bora kuwahi kutokea katika Kipindi chote. Serikali ya Rais Samia nayo imeweka Mikakati na Hamasa Kubwa hivyo Congo DR watatutambua na Watanzania tujae Uwanjani"

Baada ya Kipigo cha Kikatili ( Kishalubela ) kutoka kwa Congo DR haya ndiyo wasemayo sasa....

"Congo DR wana Timu yenye Uwezo na Uzoefu mkubwa kuliko Tanzania. Taifa Stars ina Wachezaji dhaifu na hawajui nini cha Kufanya wakiwa Uwanjani. Kocha Kim Paulsen si Kocha mzuri na hata Wachezaji anaowaita si wazuri pia. Serikali ilifanya vibaya mno kuweka Hamasa Kubwa kwani iliwaathiri Kisaikolojia Wachezaji wetu. Safari ya kwenda Kombe la Dunia QATAR Mwakani wala haipo na tusidanganyane"

Nifikishieni salamu zangu nyingi kwa Vipindi vya Michezo vya Redio, Watangazaji na Wachambuzi wa Michezo kwa ..

Wasafi FM..Sports Arena

EFM...Sports Headquarters

Clouds FM... Hili Game na Sports Extra

East Africa Radio...Kipyenga Extra

Asanteni sana na mno tu Wakongomani.
 
Tatizo lilianzia hapa
FB_IMG_16366415533933646.jpg


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Watangazaji wote wa vipindi vya michezo wamejaa usimba na uyanga na si utaifa. Upuuzi mtupu.

Hakuna mahali tutafika.
 
Uko sahihi Sana....yaani Hawa viongozi wameleta pressure kwa wachezaji...sijui walienda kufanya Nini kule uwanjani...yaani viongozi wa kisiasa hupenda kutaka 'kupora' mafanikio wakiona kuwa upo uwezekano wa timu kupanda ushindi...
Walienda kufanya nini lakini hao makolokolo..!!!???
 
Hawa si wachambuzi "analysts" bali ni watoa maoni "commentators"!
Wanatia kinyaa wanapotaka kuhodhi 'narrative" za michezo Tanzania!
 
Hata wewe unaweza kuwa mchambuzi ukitaka........ isitoshe hao kazi yao ni kuongea tu hivyo hawastahili hiyo lawama.
 
Back
Top Bottom