Wabunge zaidi ya 20 wa CCM kuhamia upinzani

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
2,602
Reaction score
409
Taarifa rasmi kutoka kwa chanzo changu cha kuaminika wabunge zaidi ya 20 wa ccm wanatarajia kuhamia upinzani. Mtoa habari huyo anasema,wamechoshwa na ubabe wa makinda na wanasema wanataka wafanye hivyo kujenga historia ya taifa kwa kuuenzi uzalendo badala ya kukumbatia wezi na mafisadi.
Aliongeza kuwa,makinda yupo pale kuchagua watu wa kuchangia,watu machachari hawatapewa nafasi. Na wameamua kumuweka mahali pale kama mtu anayekubali kuvunja kanuni kwa ajili ya kulinda serikali ya wizi na wezi wenyewe. Wanasema,mwaka mmoja si kitu historia itawakumbuka.
 
Wabunge wengi wa CCM ni mazezeta. Wamegeuka kuwa sehemu ya watawala baadala ya wao kuwa wawakilishi wa wananchi kwa kuwawajibisha watawala. Wao kuhamia upinzani sio rahisi! Wanaoweza kufanya hivyo ni wa kuhesabu... Sidhani iwapo watakuwa wengi kiasi hicho.
 
Taarifa rasmi kutoka kwa chanzo changu cha kuaminika wabunge zaidi ya 20 wa ccm wanatarajia kuhamia upinzani. Mtoa habari huyo anasema,wamechoshwa na ubabe wa makinda na wanasema wanataka wafanye hivyo kujenga historia ya taifa kwa kuuenzi uzalendo badala ya kukumbatia wezi na mafisadi.
Aliongeza kuwa,makinda yupo pale kuchagua watu wa kuchangia,watu machachari hawatapewa nafasi. Na wameamua kumuweka mahali pale kama mtu anayekubali kuvunja kanuni kwa ajili ya kulinda serikali ya wizi na wezi wenyewe. Wanasema,mwaka mmoja si kitu historia itawakumbuka.
Chama kipi sasa chenye uzalendo? CDM? CUF? NCCR? bado sijaona
 
Wabunge wengi wa CCM ni mazezeta. Wamegeuka kuwa sehemu ya watawala baadala ya wao kuwa wawakilishi wa wananchi kwa kuwawajibisha watawala. Kuhamia upinzani sio rahisi! Wanaoweza kufanya hivyo ni wa kuhesabu... Sidhani iwapo watakuwa wengi kiasi hicho.
Kwa hiyo wakihama CCM uzezeta unaisha? Watu wengine hata kutapatapa hamuwezi
 
Mbona unatapatapa kama kuku anayetaka kutaga? Umeuliza swali zuri. Ni kweli wakija watapigwa msasa sana tu, kisha watavuliwa magamba na kuvalishwa magwanda na uzezeta wao utakwisha... Upo hapo? Swali lingine?
 
Hebu hao wabunge wafanye haraka ili sisi wananchi tuwapokee kwa hoihoi, vifijo, shangwe na ndelemo hadi wenyewe wajishangae ni kwa nini walibaki CCM musa wote huo.
 
Uhakika wa habari hii ni 0.00001 wabunge wengi wa ccm ni wabunge maslahi, hawana uchungu na nchi. Hawawezi kuacha mafao yao kwa mamilioni eti kwa kuhamia upinzani kamwe!
 
Hebu hao wabunge wafanye haraka ili sisi wananchi tuwapokee kwa hoihoi, vifijo, shangwe na ndelemo hadi wenyewe wajishangae ni kwa nini walibaki CCM musa wote huo.
haa haa upo tayari kuwalipa mafao yao ya ubunge?
 
Kama ni kweli basi sio wabunge wa kuwapokea…hao inaonekana wamekosa "mgao" huko CCM na sasa hivi wameamua kuhama…wangepata mgao,kweli wangehama??mbona hawakusimamia kidete juu ya rasimu ya Warioba?? Katiba ndio msingi wa kila kitu,,tungekuwa na katiba nzuri haya ya matatizo ya IPTL yasingetokea…Naamini mkuu hao wabunge ni njaa tu…nawashari hao wabunge waanzishe chama chao tu
 
Shiida ya wabunge wa ccm hata kama n machachari unakuta bado anakiabudu chama kama mungu wake wa huku duniani, yaan yy chama ni kama mama yake, kuhama chama anaona kama n kumkana mzazi, bila kutoa mentality hii hawawez kuhama
 
Wabunge hawa watz wanatia aibu sana...kwann wasimtimue kazi huyu kibibi...
 
Ndoto za mchana hizi!!

Hamna hata Mbunge mmoja wa CCM atakaye kuwa tayari akose 300,000 per day na aziache zaidi ya Milion 100 kama kiinua mgongo mwakani!

Hamna kitu kama hicho
 
Dawa ya hapo ni kumtimua huyo bibi kiroboto ambaye wana mtumia kama mwavuri
 
Tafadhali kumbukeni ya Shibuda. Isije ikawa njama ya kuangamiza kabisa upinzani. Kama ni wajasiri waseme huko huko waliko.
 
Taarifa rasmi kutoka kwa chanzo changu cha kuaminika wabunge zaidi ya 20 wa ccm wanatarajia kuhamia upinzani. Mtoa habari huyo anasema,wamechoshwa na ubabe wa makinda na wanasema wanataka wafanye hivyo kujenga historia ya taifa kwa kuuenzi uzalendo badala ya kukumbatia wezi na mafisadi.
Aliongeza kuwa,makinda yupo pale kuchagua watu wa kuchangia,watu machachari hawatapewa nafasi. Na wameamua kumuweka mahali pale kama mtu anayekubali kuvunja kanuni kwa ajili ya kulinda serikali ya wizi na wezi wenyewe. Wanasema,mwaka mmoja si kitu historia itawakumbuka.

Mara CCM,mara Makinda haueleweki mkuu au umesikia Makinda ndio mwenyekiti wa CCM?
 
Hela hiyo hiyo imeshazungushwa kwa wabunge kadhaa kwa hiyo hata wakipiga kura ya maoni ya kutokuwa na imani na spika bado ataibuka kidedea! Bongo is really a fun country where the learned are not learned!
 
Taarifa rasmi kutoka kwa chanzo changu cha kuaminika wabunge zaidi ya 20 wa ccm wanatarajia kuhamia upinzani. Mtoa habari huyo anasema,wamechoshwa na ubabe wa makinda na wanasema wanataka wafanye hivyo kujenga historia ya taifa kwa kuuenzi uzalendo badala ya kukumbatia wezi na mafisadi.
Aliongeza kuwa,makinda yupo pale kuchagua watu wa kuchangia,watu machachari hawatapewa nafasi. Na wameamua kumuweka mahali pale kama mtu anayekubali kuvunja kanuni kwa ajili ya kulinda serikali ya wizi na wezi wenyewe. Wanasema,mwaka mmoja si kitu historia itawakumbuka.
kuna kale ka mtego ka kiinua mgongo, vipi wataziacha kweli? Hawa wabunge wetu au wengine?
 
Back
Top Bottom