Kama ambavyo imekwishaelezwa na vyombo mbalimbali vya habari, raisi Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko kwenye bara za lake la mawaziri na moja ya mabadiliko hayo yanahusu wizara ngumu ya Madini na Nishati.
Raisi amemteu mheshimwa George Simbachawene kuwa waziri kamili wa Wizara hiyo nyeti nchini Tanzania akiwa ni waziri wa nne kwenye serikali hii ya awamu ya nne.
Mheshimiwa Simbachawene kabla ya uteuzi huo alikuwa ni naibu waziri wa wizara hiyo kati ya mwaka 2012 na mwaka 2014 kabla ya kuhamishwa kwenda wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi katikati ya mwaka 2014.
Ilipofunguliwa Akaunti ya Escrow na baadae kuamuliwa kwamba IPTL ifanyiwe utaratibu wa kufilisiwa ni George Simbachawene aliepewa jukumu la kusimamia kazi hiyo akiwa naibu waziri wa madini na Nishani na hata baadae kushirikiana na maofisa wa wizara ya Ardhi.
Isisahauliwe kwamba kuna baadhi ya viongozi wa wizara hizi mbili walokuwa chini ya Simbachwene wakishughulika na akaunti ya Escrow ambao leo hii wako makakamani wakituhumiwa makosa yanayohusiana na hii akaunti ya Escrow.
Lakini tangu uteuzi huu ufanywe ni mashambulizi dhidi ya watu wengine ambayo ndio yanafanyika badala ya watanzania kukaa na kufikiri huu mchezo unaofanywa na serikali hii ya sasa.
Je Bunge letu linaona hali hiyo ni sawa pia?
Kama bunge linaona kuna kasoro katika uteuzi huu basi kuna budi kupiga kura ya kutokuwa na imani na uteuzi huu.
Sifahamu maoni ya wanachama wenzangu lakini mimi nimeona hio kasoro.
Mkuu, unapotoa maoni kwenye masuala fulani fulani, unapaswa kutumia hoja katika kuwakilisha maoni yako, mimi nimeeleza kile nilichokiona katika uteuzi ulofanyika
Unafahamu hata mzee wetu Mkapa aliwahi kusema kwamba kuna watanzania ambao wanaendekeza uvivu wa kufikiri na hio sio lengo la mada yangu.
Ni maoni yangu huru kabisa kwamba iwaje wale ambao walikuwa wakiongoza wizara ya madini na nishati(Profesa Muhongo na Simbachawene) ionekane tu kwamba ni profesa Muhongo ndio tatizo na sio viongozi wote hawa wawili ambao wameshindwa kazi ya kuongoza wizara hiyo nyeti?
Jibu lilikuwa ni kutafuta waziri mwingine mpya kutoka eneo lingine ili aendeleze au kubadilisha sera za madini na nishati, likiwemo suala la kudhibiti malipo makubwa yanayofanywa kwa TANESCO kwa ajili ya usambazaji umeme.
Wewe kaa na usubiri utakuwa kuona mambo makubwa yanaibuka baadae kidogo.
Yuko na mtaalamu Mhe Mwaijage kwa hiyo tuwape moyo vijana wanaweza kufanya vizuri zaidi baada kuona kilichowapata watangulizi wao.
Inawezekana lakini ni moja ya vikosa vidogo,
Kosa kubwa la Muhongo ni kulidanganya bunge na watanzania kwamba pesa iliyowekwa kwenye akaunti ya Escrow haikuwa ya umma wakti sio kweli.
Ni kosa hilo tu na kamati ya Zitto ikamulika jambo hilo na baadae waheshimiwa John Mnyika na David Kafulila wakatishia kumwajibisha waziri mku kwa kushindwa kutekelza maazimio ya kamati ya PAC.
Hapa tunaongelea facts za kitaifa, wewe kama umezoea mipasho nenda leaders club ndio utawakuta
Muhongo mtendaji mzuri kapigwa zengwe mpaka kaondoka,Simbachawene hata kazi hajaanza zengwe limeanza tena,labda mnataka ateuliwe MTU toka Sayari ya Mars.
Mwijage ana utaalamu gani wakati yeye na Asumta Mshama ndio walikuwa watetezi wa hiyo kashfa?
Tena huyo usimtaje kabisa hapa! Kwa sasa magufuli kama ni mkweli kama ambavyo anasema sheria za madini zirudi bungeni kubadilishwa basi NA SHERIA YA KINGA YA RAIS IRUDI BUNGENI IBADILISHWE ILI TU- DEAL NA AWAMU MBILI ZA NYUMA.Kama kosa ni hilo hata Kikwete alisisitiza kuwa pesa si za umma, hatua gani bunge limechukua?
Tena huyo usimtaje kabisa hapa! Kwa sasa magufuli kama ni mkweli kama ambavyo anasema sheria za madini zirudi bungeni kubadilishwa basi NA SHERIA YA KINGA YA RAIS IRUDI BUNGENI IBADILISHWE ILI TU- DEAL NA AWAMU MBILI ZA NYUMA.
Sent using Jamii Forums mobile app
mda ni mwlimu mzuri sana kila lifanikialo gizani litakuwa nuruni mda ukifika
Vapour vapour. Huna hoja. Unatupotezea muda. Kama Muhongo anahusika kwa hiyo wote waliokuwa chini yake wanahusika?! natural logic haipo hapo na systematic logic hsipi hapo. Kilichobaki hapo ni wivu kujaa chuki na kukosa kazi kushinda JF kuandika hewa.
Du we kiboko unaona mbali snaMkuu, unapotoa maoni kwenye masuala fulani fulani, unapaswa kutumia hoja katika kuwakilisha maoni yako, mimi nimeeleza kile nilichokiona katika uteuzi ulofanyika
Unafahamu hata mzee wetu Mkapa aliwahi kusema kwamba kuna watanzania ambao wanaendekeza uvivu wa kufikiri na hio sio lengo la mada yangu.
Ni maoni yangu huru kabisa kwamba iwaje wale ambao walikuwa wakiongoza wizara ya madini na nishati(Profesa Muhongo na Simbachawene) ionekane tu kwamba ni profesa Muhongo ndio tatizo na sio viongozi wote hawa wawili ambao wameshindwa kazi ya kuongoza wizara hiyo nyeti?
Jibu lilikuwa ni kutafuta waziri mwingine mpya kutoka eneo lingine ili aendeleze au kubadilisha sera za madini na nishati, likiwemo suala la kudhibiti malipo makubwa yanayofanywa kwa TANESCO kwa ajili ya usambazaji umeme.
Wewe kaa na usubiri utakuwa kuona mambo makubwa yanaibuka baadae kidogo.
Upo mkuu?Huna lolote wewe ni wivu tu madaraka ndo unaokusumbua..! What's wrong with simbachawene? Nyie bavicha jinsi mlivyo hata angewekwa nani bado tu mngekuja na opinion zenu uchwara.