Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,785
- 26,094
Kama ambavyo imekwishaelezwa na vyombo mbalimbali vya habari, rais Jakaya Kikwete alifanya mabadiliko kwenye bara za lake la mawaziri na moja ya mabadiliko hayo yanahusu wizara ngumu ya Madini na Nishati.
Rais amemteua mheshimwa George Simbachawene kuwa waziri kamili wa Wizara hiyo nyeti nchini Tanzania akiwa ni waziri wa nne kwenye serikali hii ya awamu ya nne.
Mheshimiwa Simbachawene kabla ya uteuzi huo alikuwa ni naibu waziri wa wizara hiyo kati ya mwaka 2012 na mwaka 2014 kabla ya kuhamishwa kwenda wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi katikati ya mwaka 2014.
Ilipofunguliwa Akaunti ya Escrow na baadae kuamuliwa kwamba IPTL ifanyiwe utaratibu wa kufilisiwa ni George Simbachawene aliepewa jukumu la kusimamia kazi hiyo akiwa naibu waziri wa madini na Nishani na hata baadae kushirikiana na maofisa wa wizara ya Ardhi.
Isisahauliwe kwamba kuna baadhi ya viongozi wa wizara hizi mbili walokuwa chini ya Simbachwene wakishughulika na akaunti ya Escrow ambao leo hii wako mahakamani wakituhumiwa makosa yanayohusiana na hii akaunti ya Escrow.
Lakini tangu uteuzi huu ufanywe ni mashambulizi dhidi ya watu wengine ambayo ndio yanafanyika badala ya watanzania kukaa na kufikiri huu mchezo unaofanywa na serikali hii ya sasa.
George Simbachawene si mtu sahihi kuwekwa wizara nyeti ya Madini na Nishati kwani amekosa uadilifu.
Je Bunge letu linaona hali hiyo ni sawa pia?
Kama bunge linaona kuna kasoro katika uteuzi huu basi kuna budi kupiga kura ya kutokuwa na imani na uteuzi huu.
Sifahamu maoni ya wanachama wenzangu lakini mimi nimeona hio kasoro.