Wabunge wetu wajitathmini waheshimike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wetu wajitathmini waheshimike

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by shabibu, Jul 11, 2012.

 1. s

  shabibu New Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Naamini sote tuwazima kwa uwezo wa Muumba wa mbingu na ardhi

  Ndugu zangu,
  Najitahidi kuacha kuwafikiria wanasiasa wa tz lakini nashindwa. Sijui ni vipi wanajisikia pale wanapoona wananchi wanteseka kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii huku wao wakipeleka mipasho na viduku bungeni. Sielewi ni kwa kiasi gani kwa dhati wanaiangalia tz baada ya miaka 20 mbele. Wandhani madaktari ndio wapo kwenye mgomo pekee. Hawajui kuwa walimu walianza mgomo wao miaka mingi iliyopita. Angalia wanafunzi wanaomaliza shule na hata vyuo.. Wengi hawaakisi maarifa yao kwa jamii.

  Wabunge wangeamua kuacha siasa mkumbo za magwanda na magamba; mafisadi na watakatifu wakaangalia mustakbali wa nchi na maslahi ya vizazi. Chama-dola kimekuwa kikitumia kanuni na taratibu rasmi kutetea maslahi ya chama badala ya taifa, vyama shindani vimekuwa vikitumia muda mrefu bungeni kuonesha kuwa wao wanaweza kuwashambulia na kujibu hoja za maneno kwa kutumia akili na mantiki ya hali ya juu badala ya kujadili masuala madogo tu yanayowagusa wananchi kama huduma za afya, barabara, maji, elimu n.k? Jiulize, kwa mfano Dar es Salaam pekee ina wabunge zaidi ya 8, madiwani zaidi ya 75, mameya 4, viongozi wote hawa wa kisiasa (wa kuchaguliwa) wanatokana na vyama mchanganyiko. Pamoja na wanasiasa hao pia kuna watendaji tele wakiwemo wansiasa wa kuteuliwa kama RC na DC! Pia kuna utitiri wa watendaji kuanzia ngazi ya mkoa hadi mitaa. Angalia hali ya uchafu, barabara, maji, umeme, ufisadi, ukabaji, ubakaji, ukahaba na uchafu mwingine ulioenea. Sisemi kuwa dar es Salaam kama Dubai wala London ila naamini inaweza kuwa kama Moshi na Mwanza... Hili nalo wadau wa Dar es Salaam hamliwezi (au nanyi mnakula na wezi? japo nanyi si wezi?).

  Badala ya kufikiria njia bora ya kuwaletea maendeleo wananchi wanaanza kutukanana (rejea kauli ya meya Wabunge wa Dar es Salaam wanafikiri kwa makalio). Ni kweli yawezekana meya kaliona na kuhihisi yeye ni msafi na mtakatifu kama ilivyo ada na slogan ya sasa, ukiwahi tu kumuita mwenzako fisadi wewe unakuwa mtakatifu. Ila tujiulize Wabunge wa Dar es Salaam ambao ni wajumbe wa kila kikao cha maamuzi kuanzia huko mtaani hadi Taifa wanafikiri kama tunavyofikiri sisi hasa WEWE!!! Si ndio hawa walikurupuka kumshambulia Magufuli wakaambulia kejeli za kiranja wao Mh. Pinda (walidhani naye hatumii akili). "Tatizo wewe Magufuli una utani sana (kuhusu nauli za kivuko)" Mh. Pinda alimaliza kesi kwa jibu hilo, wote kimyaa.

  Nampongeza mh. Zitto, J.Makamba, Shibuda (nikimaanisha yeye John M) kwa kujitahidi kuwa wao wanapochangia au kusimama na kusimamia misimamo yao. Shibuda hachelei kuitwa msaliti kwa kusema ya moyoni mwake. Zitto hachelei kutengwa wala hahitaji kuigiza ili wananchi wake wamuone. Makamba pamoja na kuwa aliwahi kudaiwa kumfitinisha mtangulizi wake jimnoni lakini anayoyafanya na kuyatanga ni ushahidi wa dhamira yake kwa wananchi wake na taifa lake (sina hakika bado kama hatafisidika kwa unaibu waziri)

  ni wabunge wangapi wa ccm ambao kwa dhati wanaunga mkono wasiyoyataka wala kuyaamini nyoyoni mwao kwa sababu tu ni msimamo wa chama? Ni wabunge wangapi wanakosoa bajeti kuanzia mwanzo hadi mwisho lakini wanamaliza michango yao kwa kuunga mkono hoja kwa 100%. Kioja na kichekesho. Ni wabunge wangapi wa ushindani wanaamua kushika kuhubiri bungeni badala ya kuchambua na kuliongoza bunge kuwa kioo ya siasa za kiistaarabu na demokrasia, mbunge unaajisifu na kutamka "fungeni mlango tupigane humu (ushindani)" na mwingine anajibu "kwanza tukiamua kupigana sisi ni wengi tutawashinda (ccm)".

  Inaumiza zaidi kuona namna tunavyohujumiwa ni wanasiasa, kampeni za uchaguzi mdogo kila chama kinajitahidi kuonesha ufundi wa kufuja pesa na maneno (lugha mbaya). Rejea chaguzi za igunga na arumeru mashariki. Kama kweli wanasiasa wanatupenda, kwa nini zile pesa za kukodisha helikopta na bendi za muziki wasiamue kutuchimbia visima, kununulia madawati na hii ikawa ni sehemu nzuri sana ya kampeni. Ni mengi yanatia kinyaa kwa wansiasa wetu...... Nishauri kuwa wabunge wote walazimishwe kwenda kuishi kwenyw majimbo yao waende Dar es Salaam wakati wa likizo kama wanafunzi wafanyavyo. tena wao wanafuata twisheni ya Mchikichini, wabunge watachagua cha kufuata hapa.

  Nikikumbuka YOTE hayo nakuja kugundua kuwa YULE ALIYEIMBA WIMBO WA KARIAKOO akilifananisha Bunge kaka Kariakoo, ana akili sana tena sana kuliko wengi wa wabunge. Hebu naombe ULE WIMBO uwekwe humu UWE WIMBO RASMI wa JF wakati huu BUNGE likiendelea.

  Ubabe wa bungeni ndio unahamishiwa kwenye roho na mustakabali wa nchi!
   
Loading...