Wabunge wetu mjifunze kuuliza maswali yenye mantiki

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,979
45,865
Kwa kweli nadhani huu ni ugonjwa wa taifa sasa , baada ya kuonekana kuwa ni tatizo la kudumu kwa wanahabari swala hili la kutokuwa na maswali yenye kulenga kutafuta suluhu ya matatizo ya waliowachagua au kuibua mijadala yenye mantiki, nalo limekuwa tatizo sugu sasa kwa wabunge wetu.

Unakuta sehemu kubwa ya swali la mbunge au hoja atakayoitoa bungeni ni hearsay tu, hakuna objectivity yoyote katika swali lake.

Au unakuta 90% ya argument yake ni baseless na irrelavent, unabaki kujiuliza kama huyu ndiye mh. Mbunge na kuna watu wanategemea kitu chanya kutoka kwake.

Itatubariki sana sisi wananchi kama kodi zetu zikitumika kwa kugharamia hoja zenye kuleta tofauti katika maisha yetu kuliko kila siku kusikia stori za mtaani zikifika na kujadiliwa Bungeni, inafikia mahali unashindwa kutofautisha vijiwe vyetu vya kahawa na hapo mjengoni.

Kwakweli mnatusikitisha sana.
 
Labda kwavile wanawakilisha wananchi basi mawazo ya vijiwe ndio yanawakilishwa
 
Back
Top Bottom