Wabunge wetu mbona kimya bei ya sukari kwa wapiga kura wenu?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Nimeshangazwa sana Na viongozi wa nchi hii wakiwemo Wabunge wetu kukaa kimya Juu ya upatikanaji Na bei ya sukari hapa nchini.Nilitegemea wabunge wetu wangehakikisha sukari inapatikana Kwa bei nafuu lakini badala take in kama Serikali imepandisha bei ya sukari Kwa wananchi wake.Tuliambiwa serikali imeagiza sukari Kutika nje mbona hatuoni unafuu wowote? Ndugu zetu waislaam wanaanza mfungo wa Ramadhani , sukari in muhimu katika chakula chao mbona serikali haikemei bei kupanda?Wabunge wetu hebu lisemeeni bungeni.
 
Ukiona sehemu wabunge wamecharuka sana ujue wanawapaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa ktk majimbo yao na Tanzania kwa ujumla, kamwe mwanasiasa hawezi kumkwamua mwananchi mnyoge ktk taabu na shida zake, ukumbuke masikini ni malisho ya tajiri. Wakati masikini alalalama kwa maumivu ya bei na upatikanaji wa sukari, matajiri wanayo na wanamuuzia mwananchi huyu mnyonge kwa bei wanayotaka, haijalishi wanamkamua damu au maji, afe apone hawahusu. Kamwe,Kura sio suluhisho la maisha ya masikini ila kuwatafutia maisha bora wanasiasa na familia zao.
 
Viongozi wetu wamejaa hofu kila mtu anafanya kazi kwa hofu nani anaweza akamwambia Mfalme yuko uchi hayupo!!!! Hongereni wabunge mliofukuzwa bungeni na mnao toka bungeni wakati wa vikao kwani mnaionyesha dunia nini watanzania wanataka lakini mtawala ameziba masikio.Vilaza ni watoto wa wakulima na wafanyakazi wadogo watpto wao hata akiwa divisheni ZERO anapelekwa kozi nzuri vyuo vikuu hapa nchini au nje ya nchi.Mtoto gani wa kiongozi alikuwa anasoma ualimu UDOM? watoto wao hawasomi ualimu kama alivyosema Bashe hii kozi ni ya watu waliokata tamaa.Watoto wao wanasoma biashara na uchumi ili waje kufanya kazi TRA na BOT.Sukari imepandishwa bei kutokana na wachumi kushindwa kuchukua nafasi yao na kumwacha Mfalme akiongoza bilaa weredi baado sakata la UDOM tulioumia ni sisi walala hoi si Mfalme na kundi lake.
 
Hao wabunge wako walitoka nje unajua watoto wao wanasona wapi na wanafanya kazi wapi? Funguka na fanya utafiti unajua
 
Nimeshangazwa sana Na viongozi wa nchi hii wakiwemo Wabunge wetu kukaa kimya Juu ya upatikanaji Na bei ya sukari hapa nchini.Nilitegemea wabunge wetu wangehakikisha sukari inapatikana Kwa bei nafuu lakini badala take in kama Serikali imepandisha bei ya sukari Kwa wananchi wake.Tuliambiwa serikali imeagiza sukari Kutika nje mbona hatuoni unafuu wowote? Ndugu zetu waislaam wanaanza mfungo wa Ramadhani , sukari in muhimu katika chakula chao mbona serikali haikemei bei kupanda?Wabunge wetu hebu lisemeeni bungeni.

Kuna mambo muhimu zaidi ya hilo... Maswala ya Elimu na Afya ni muhimu kuliko Bru ya sukari ... Hilo ni la kupita tu.....
 
Hapo nyuma tuliona viongozi wa serikali wakiwa bize kutafuta kina nani wameficha sukari. Leo kila kiongozi yupo kimya je tatizo limeisha au ulikuwa ni usanii tu.
Leo hapa Tabora kilo ya sukari tunanunua kuanzia shilingi 4,000/= mpaka 6,000/= za kitanzania. Kinachonishangaza sukari yenyewe ni ya Kilombero na Kagera.
Maswali ya kujiuliza,
1. Je, gharama za uzalishaji zimepanda kulinganisha na nyuma kabla ya zuio la sukari kutoka nje?
2. Je, huu ni mkakati wa wamiliki wa viwanda kutengeneza faida maradufu, na je serikali haioni hili jambo?
3. Je, wanaopandisha bei wako juu ya sheria na watumbua majipu wanawaogopa?
4. Je, kwa nini nisiache kuamini kwamba serikali imetengeneza hili tatizo ili baadhi ya watu wajipatie mapesa ya bure kutoka kwa watanzania masikini?
Karibuni kwa mjadala.
 
Hili tatizo la sukari lisije likasababisha balaa hasa wakati wa mfungo wa Ramadhan. Iwapo serikali haitafikiria vinginevyo ili kurejesha hali iliyokuwepo awali, nina hofu sana kama tutavuka salama.
 
Masheikh wanaweza kutoa kauli
 
aachwe huyo jesca.tuangalie mambo ya msingi.jesca sio chanzo cha tatizo.!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom