Wabunge wawapongeza vijana wa Copa Coca Cola kwa Sh23.5milioni

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Hawa vijana wanastahili kuwa timu yetu ya Taifa ya vijana na wakutane angalau kila baada ya miezi mitatu ili wafanye mazoezi ya pamoja na kucheza mechi za kirafiki. TFF wahakikishe hawasambaratiki maana miaka michache ijayo wanaweza kufanya maajabu makubwa kwenye kombe la dunia ya timu za vijana na naamini wana uwezo wa kufika huko.

Wabunge wawapongeza vijana wa Copa Coca Cola kwa Sh23.5milioni

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

TIMU ya vijana iliyoshiriki michuano maalum ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Copa Coca-Cola nchini Brazil na kutwaa ubingwa, jana walionjeshwa utamu wa ushindi wakati wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Mungano walipoamua kuwajaza kitita cha zaidi ya Sh23.5milioni.

Mchango huo ulitangazwa na Naibu Spika, Anna Makinda wakati timu hiyo ilipojiwekea historia ya kuingia kwenye kikao cha Bunge kwa ajili ya kukabidhi kombe hilo mjini hapa.

Hafla hiyo ya kukabidhi kombe ilidumu kwa takriban dakika 20 baada ya waziri anayehusika na michezo, George Mkuchika kuliomba Bunge kuiruhusu timu hiyo kuingia kwenye ukumbi wake kwa kutengua kifungu Namba 136 (1) kinachozuia mgeni kuingia kwenye kikao.

Jana kamati ya uongozi ya Bunge ilipokutana, ilipendekezwa kila mbunge atoe shilingi 10,000 na fedha hizo wapewe watoto wenyewe,'' alisema Makinda.

Fedha hizo zilitarajiwa kukabidhiwa kwa Waziri Mkuchika baadaye jana na kukabidhiwa kwa wachezaji hao 16 walioteuliwa kwenye mashindano ya taifa ya Copa Coca-Cola yaliyomalizika jijini Dar es salaam mwezi uliopita.

Ahadi hiyo inamaanisha kuwa vijana hao watachangiwa kiasi kisichopungua Sh 23.5 milioni kulingana na majimbo ya uchaguzi na idadi ya wabunge waliopo sasa.

Katika hafla hiyo, Waziri Mkuchika aliliambia Bunge kuwa Tanzania ilizishinda nchi za Argentina (2-0) na Peru (5-1) na kutoka sare na Chile (0-0) na kuingia nusu fainali ambako iliishinda Paraguay (3-1).

Katika fainali ilikutana tena na Chile na kuibwaga kwa bao 1-0. Timu hiyo ilikabidhi kombe kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Wachezaji waliokuwemo katika msafara huo ni Kabari Faraji Swaleh, Mohamed Aziz Hussein, Ahmed Mohamed Chimpele, Sadik Gwaza Twabu, Adili Adam Sambiro, Kenny Ally Mwambungu, Himid Mao Mkami na Faraji Hamad Hussein.

Wengine ni Lambele Jerome Ruben, Karim Sule Suleiman, Zahoro Jailani Ismail, Jukumu Kibanda Joackim, Dotto John Greyson, Joseph Petro Mahundi, Hemed Suleiman Mohamed

na Mock Shaban Msafiri.
 
Back
Top Bottom