Wabunge watano wa Jiji la Dar hawa hapa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
HATIMAYE wabunge watano (5) watakaoingia katika baraza la madiwani la halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wamepatikana, anaandika Kondo Tutindaga.

Wabunge waliochaguliwa kuingia katika baraza la jiji, ni Halima Mdee (Kawe), Saed Kubenea (Ubungo), Abdallah Mtolea (Mbagara), Dk. Faustine Ndugulile (Kigamboni) na Mussa Azzan Zungu (Ilala).

Katika uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepata nafasi mbili, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepata nafasi mbili na Chama cha Wananchi (CUF), kimepata nafasi moja.

Jiji la Dar es Salaam lina majimbo 10 ya uchaguzi, ambapo CCM ina wabunge wa wanne na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umenyakua viti sita. Sheria inayounda jiji la Dar es Salaam, inatambua wabunge watano tu kuwa wajumbe wa baraza la madiwani; kati ya wajumbe hao, angalau mmoja awe mwanamke.

Akiongea na MwanaHALISI Online, Mdee amesema, mgawanyo huo umezingatia matakwa ya kisheria ya kila halmashauri kuwa na mwakilishi. Amesema kwa sasa, jiji la Dar es Salaa lina halmashauri tano – Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Ilala.

“Tumeona tufanye makubaliano kwamba kila chama kipate uwakilishi badala ya utaratibu wa kupiga kura. Hii imetokana na utata uliopo kwenye sheria nzima inayounda jiji,” ameeleza.

Amesema, katika makubaliano hayo, CCM wamepata viti viwili na UKAWA tumepata viti vitatu.

Naye Kubenea akizungumzia uchaguzi huo alisema, “yale yalikuwa maridhiano yenye tija kwa pande zote. Kuna utata mkubwa wa kisheria na hivyo tumeona ili kumaliza suala hili, tufanye makubaliano kwa kuwa bila hivyo, shughuli za jiji zilikuwa zimekwama.”

Amesema, “baraza lisingeweza kuitwa bila kuwapo uwakilishi wa wabunge. Miradi na rasimali za jiji zilikuwa zinaendelea kuporwa na wajanja kwa kuwa baraza la madiwani haliwezi kufanya shughuli zake.

“Uchaguzi wa Naibu Meya umekwama kwa kuwa wabunge hawajakubaliana kuhusu uwakilishi wao katika jiji. Hivyo, kwa kuzingatia yote hayo, tukaona ni muhimu kufanya maamuzi haya mapema ili shughuli za jiji ziendelee.”

Kwa mujibu wa Kubenea, kulikuwa na uwezekano UKAWA kuingiza wajumbe wanne kati ya watano waliohitajika, lakini kutokana na kuona jambo hilo litawapotezea muda na lingeweza kutumika kuvunja uongozi wa jiji, wakakubaliana wenzao wa CCM kugawana viti.

Uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji umepangwa kufanyika leo, Alhamisi saa tano asubuhi katika ukumbi wa Karimjee.
 
HATIMAYE wabunge watano (5) watakaoingia katika baraza la madiwani la halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wamepatikana, anaandika Kondo Tutindaga.

Wabunge waliochaguliwa kuingia katika baraza la jiji, ni Halima Mdee (Kawe), Saed Kubenea (Ubungo), Abdallah Mtolea (Mbagara), Dk. Faustine Ndugulile (Kigamboni) na Mussa Azzan Zungu (Ilala).

Katika uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepata nafasi mbili, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepata nafasi mbili na Chama cha Wananchi (CUF), kimepata nafasi moja.

Jiji la Dar es Salaam lina majimbo 10 ya uchaguzi, ambapo CCM ina wabunge wa wanne na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umenyakua viti sita. Sheria inayounda jiji la Dar es Salaam, inatambua wabunge watano tu kuwa wajumbe wa baraza la madiwani; kati ya wajumbe hao, angalau mmoja awe mwanamke.

Akiongea na MwanaHALISI Online, Mdee amesema, mgawanyo huo umezingatia matakwa ya kisheria ya kila halmashauri kuwa na mwakilishi. Amesema kwa sasa, jiji la Dar es Salaa lina halmashauri tano – Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo na Ilala.

“Tumeona tufanye makubaliano kwamba kila chama kipate uwakilishi badala ya utaratibu wa kupiga kura. Hii imetokana na utata uliopo kwenye sheria nzima inayounda jiji,” ameeleza.

Amesema, katika makubaliano hayo, CCM wamepata viti viwili na UKAWA tumepata viti vitatu.

Naye Kubenea akizungumzia uchaguzi huo alisema, “yale yalikuwa maridhiano yenye tija kwa pande zote. Kuna utata mkubwa wa kisheria na hivyo tumeona ili kumaliza suala hili, tufanye makubaliano kwa kuwa bila hivyo, shughuli za jiji zilikuwa zimekwama.”

Amesema, “baraza lisingeweza kuitwa bila kuwapo uwakilishi wa wabunge. Miradi na rasimali za jiji zilikuwa zinaendelea kuporwa na wajanja kwa kuwa baraza la madiwani haliwezi kufanya shughuli zake.

“Uchaguzi wa Naibu Meya umekwama kwa kuwa wabunge hawajakubaliana kuhusu uwakilishi wao katika jiji. Hivyo, kwa kuzingatia yote hayo, tukaona ni muhimu kufanya maamuzi haya mapema ili shughuli za jiji ziendelee.”

Kwa mujibu wa Kubenea, kulikuwa na uwezekano UKAWA kuingiza wajumbe wanne kati ya watano waliohitajika, lakini kutokana na kuona jambo hilo litawapotezea muda na lingeweza kutumika kuvunja uongozi wa jiji, wakakubaliana wenzao wa CCM kugawana viti.

Uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji umepangwa kufanyika leo, Alhamisi saa tano asubuhi katika ukumbi wa Karimjee.
Hapo kwenye bold pana hitaji masahihisho kidogo kama sikosei
 
Ukawa wana busara sana, ingekuwa ccm ndio wengi wangekomaa na uchaguzi kwa kuwa wao ndio wangeshinda.. wajifunze ubinafsi ni ulafi..walitusumbua sana kwenye swala la umeya.
Hapa naomba tusaidiane. Hivi ni kwa nini kila inapotokea nafasi hizi za uteuzi CHADEMA wanaishinda CUF? Kwa mfano, walipofanya uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na Ilala, CHADEMA ndo wamesimamisha nafasi ya Umeya na CUF kupewa Naibu Meya. Huo si ubinafsi?
 
Kama wewe hapa, badala uje na jambo la maana unaanza yasiyo na maana.
Halafu ukiitwa BWEGE utasema unatukanwa?
Mbona unalitumia vibaya jina la mbunge wenu? Hujui kuwa BWEGE ni SELEMAN BUNGALA, yule mbunge wenu wa Kilwa Kaskazini kupitia CUF?
 
Hapa naomba tusaidiane. Hivi ni kwa nini kila inapotokea nafasi hizi za uteuzi CHADEMA wanaishinda CUF? Kwa mfano, walipofanya uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na Ilala, CHADEMA ndo wamesimamisha nafasi ya Umeya na CUF kupewa Naibu Meya. Huo si ubinafsi?
Idadi ya wabunge wa CUF na CHADEMA inalingana? Ungehoji basi mbona NCCR hawapati nafasi hata moja!
 
Naomba kuuliza kwa waliopo Dar es Salaam, hivi Abdallah Mtolea ni mbunge wa Mbagala ama Temeke?
 
Idadi ya wabunge wa cuf na chadema inalingana? Ungehoji basi mbona nccr hawapati nafasi hata moja!
NCCR hawana mbunge wala Diwani Dar es Salaam. Hivyo itakuwa ni uchizi kumteua Mbatia kwenye Halmashauri ya Jiji
 
Back
Top Bottom