LGE2024 Msimamizi wa Uchaguzi Dodoma: CHADEMA wameweka mawakala 55 katika vituo 666

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
62,123
72,412
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka Mawakala 666 katika Vituo 666 vya kuandikisha Wapigakura huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiweka Mawakala 55.

Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dk. Frederick Sagamiko amesema hayo wakati mkoani humo wakati akikanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mwenendo wa uandikishaji kuwa wanaandikishwa mamluki kwenye orodha ya wapigakura.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina jumla ya vituo 666 vya kujiandikishia wapiga kura na vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinashiriki uchaguzi mkuu vimeruhusiwa kuweka mawakala wao katika kila kituo.

“Naomba nichukue nafasi hii kuwataarifu kwamba ni vyama viwili tu vilivyofanikiwa kuweka mawakala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuweka mawakala 666 katika kila kituo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanikiwa kuweka mawakala 55.” Alisema.

Sagamiko alisema Chadema wameweka mawakala katika Kata sita, kati ya Kata 41 zilizopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambazo ni Kikombo (9), Kikuyu Kaskazini (12), Chamwino (7), Chihanga (4), Ng’hong’onha (19) na Mbabala (4).

Aidha, alivitaka vyama vya siasa kufuata kanuni na miongozo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uchaguzi uwe wa huru na wa demokrasia na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutokushiriki katika uvunjifu wa amani katika maeneo ya vituo na kuzingatia kanuni ambazo tayari walishagawiwa.

Pia amewataka wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wenye sifa za kujiandikisha kujitokeza na kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa.

Dodoma.jpg

Swali.
Kwa staili hii hamuoni Aibu kuingia kwenye uchaguzi? 😂😂😂😂😂😂

Chama Cha X zamani Twitter mnaona mnavyopuuzwa? Tuliona kwenye maandamano ya kutaka kuleta vurugu Hadi huku mtaani.

Mafuriko ya mitandaoni Huwa yanawadanganya sana na bahati mbaya hamjifunzi.Watu wenye uwezo wa kununua bando hawafiki hata 5% ya Watanzania wote,mkiangukia Pua Utasikia tumeibiwa 😂😂😂
 
Chadema chama Cha X zamani Twitter kimeshindwa kupata mawakala wa Kusimamia Zoezi la uandikishaji na kupiga
Tulishasemaga siku nyingi sana hiki chama cha X hakina wanamikakati na chama hakiwezi kutoba bila ya uwepo wanamikakati na sio kutegemea wapiga kelele mitandaoni na kuongea na waandishi wa habari kuli uchao(Lema)
 
Tulishasemaga siku nyingi sana hiki chama cha X hakina wanamikakati na chama hakiwezi kutoba bila ya uwepo wanamikakati na sio kutegemea wapiga kelele mitandaoni na kuongea na waandishi wa habari kuli uchao(Lema)

Kwanini kuwe na mawakala wa vyama ikiwa uchaguzi inafuata taratibu zote za kisheria, na unaamuliwa kwa haki?

Yaani ni kama tumejenga imani kwamba bila kusimamiwa na mawakala uchaguzi hauwezi kufanyika kwa kufuata taratibu.
 
Kwanini kuwe na mawakala wa vyama ikiwa uchaguzi inafuata taratibu zote za kisheria, na unaamuliwa kwa haki?

Yaani ni kama tumejenga imani kwamba bila kusimamiwa na mawakala uchaguzi hauwezi kufanyika kwa kufuata taratibu.
Kazi Yao ni kuhalalisha matokea sio mtu Kushindwa aje Kulalamikia kuibiwa.
 
Kama mnaona taratibu hazifuatwi kwani nini mshiriki uchaguzi?


Tumejenga imani kwamba hatuwezi kutenda haki kwa wagombea bila usimamizi wa mawakala, huo ni utamaduni mbaya.

Mgombea anatakiwa atendewe haki hata kama hana mawakala ktk vituo.

Wagombea kazi yao iwe kutangaza sera zao, na sio kupanga mikakati ya hila ktk vituo vya kura kwa kushirikiana na mawakala.
 
Back
Top Bottom