Wabunge wanapopiga kelele kukatwa Kodi katika Mafao yao, ni Ubinafsi

Malick M. Malick

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
658
312
:WABUNGE WANAPOKUA WAKALI KATIKA MASLAI YAO

Baadhi ya wabunge wamekua Wakali sana, katika mjadala wa bajeti 2016/2017 na mjadala kwao ni kua wao hawastahili kukatwa kodi katika mafao yao "Kiinua mgongo" hapo ndio utagundua Ubinafsi wa hawa wabunge wetu . Nimeshangaa sana, nazidi kushangaa sana..

Ukisikia sababu zao,unaweza kapata kizunguzungu , wanamwambia waziri wa Fedha sababu yeye sio mbunge wa Jimbo .. Hivyo hajui mambo ya katika Jimbo ..

Wabunge wako tayari kuzalilisha Wananchi (Wapiga kura) ili jambo lao lipite, wanasingizia kua wao ndio kila kitu katika jimbo, ni uongo uliopitiliza, eti kila msiba wa katika jimbo mbunge anatakiwa kuchangia, kila mtoto haliekosa hada mbunge anatakiwa kuchangia ni uongo uliopitiliza.. Ni kuwadunisha Wananchi na kuwafanya Wananchi kua wao ni omba omba wakati sio kweli, mengi wanayo ombwa wabunge ni yale ambayo walihaidi kuyafanya wao Kama wao, wakati wanaomba kura, Leo wanawasemanga wana nchi, kua Wanadai Maslai yao, kwa lengo la kwenda kugawana nao.. Huu ni mzaa mkubwa kwa wananchi watanzania.

Mtindo wa WABUNGE kudai maslai yao, na kuweka kichaka wapiga kura, kua wao wamebeba mzigo mzito kwa wananchi, ni dharau kwa wananchi, kila mwananchi anajishughurisha katika jimbo, na ukweli ni kua baada ya uchaguzi kupita, wabunge wengi ubadili namba za simu, kwa kuogopa ata kupokea simu ya Salamu tu.

Wabunge walinde maslai yao kwa nguvu za Hoja sio blah blah sizizo na msingi..

Mimi binafsi naunga mkono kwa serikali na waziri wa fedha kwa kuanza kukata kodi kwa wabunge katika kiinua mgongo Chao,pia serikali ifikirie kuanza kutoa kiinua mgongo(Mafao), kwa Wabunge ambao wanashindwa kurudi Bungeni , wale ambao wanakua wanaendelea wasipewe mpaka itakapo tokea amekoma kua Mbunge .

Serikali isigeuke nyuma katika hili.. Waziri wa Fedha.. Waambie wabunge, Ubunge sio kazi ya Maslai, kama wanataka maslai wakafanye kazi za Taaluma zao.

Watu wanao stahili kufutiwa kodi katika Mafao (Kiinua mgongo ni watumishi wa Umma tu, ili iwe motisha watu kufanya kazi katika Serikali) sio Wabunge , Ubunge si kazi ya kitaaluma, Watu wanaacha kazi za Taaluma kwenda katika Ubunge, Watu wanaacha biashara zao kwenda Ubunge. Kwahiyo wanaenda kwa hiyali sio kulazimishwa.. Asietaka ajiuzuru, Waziri wa Fedha wajibu jibu fupi tu, wanaruhusiwa kujiuzuru Ubunge.

Serikali inatakiwa kwenda mbali zaidi, ifikirie kufuta na posho za kukaa katika bunge, Ubunge sio kazi, inayomfanya mtu akadai maslai yake, Ubunge utumishi tu(Kujitoa) kuwakilisha wananch.. Anaewaza kupata Maslai katika Ubunge, afikirie mara mbili, kuendelea au kuacha.. NCHI isonge mbele.

Nimefarijika kutowaona Wabunge vijana wakiingiaa katika mtego huu,nawapongeza wote watakao kua pamoja na serikali katika hili la wao kukubali kukatwa kodi katika Mafao yao pale wanapo maliza Utumishi wa Ubunge..

Ushahuri wangu Mhe Waziri wa Fedha,Dr Mpango, mfikirie kwa watumishi wa Umma kuhusu Kodi, katika mafao yao watumishi wa Umma kwa kweli,hapa ndio pa kuangaliwa kwa jicho la Tatu, ningeomba mfanye mabadiliko ya sheria katika ili, mtoe hamasa kwa watumishi wa UMMA.

Wakatabahu
Ndimi
Malick Maliki
Lindi Vijijini
 
Back
Top Bottom