Wabunge wanahujumu mjadala ya ripoti za kamati za bunge

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Kumbe wabunge wetu, pamoja na kuaswa na spika, wanashindwa kutofautisha mjadala wa hotuba za mawaziri wakati wa bunge la bajeti na mjadala wa hotuba za wenyeviti wa kamati za bunge. Mbunge anapoomba ujenzi wa barabara katika jimbo lake una maana gani?

Wabunge wanapoacha kugusia yale yaliyotajwa katika ripoti za kamati za bunge na hasa mapendekezo kunaipunguzia hadhi bunge letu.Kwa kufanya hivyo, wabunge wanaonesha jinsi walivyo na upeo mdogo katika uelewa wa mambo yanayofanyika bungeni na jinsi wanavyopaswa kujadili na namna ya kujadili.

Kama hivyo ndivyo wabunge wanavyojadili hotuba za wenyeviti wa kamati za bunge kuna haja ya spika kuwazuia wabunge wasifanye hivyo.
 
Back
Top Bottom