Wabunge wamtolea uvivu Rais Magufuli

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945


Wabunge wa upinzani walitumia siku ya jana kuichambua Serikali, kwa nyakati tofauti wamesema kufanya kazi kwa hofu kumesababisha Mawaziri na watendaji kupooza, wabunge hao wamsema hayo wakati wakichangia hotuba za bajeti za Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Tamisemi inaomba kuidhinishiwa Sh6.5 trilioni, huku Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ikiomba kuidhinishiwa Sh821 bilioni.

Katika mjadala huo, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema tangu mwaka 1980 hadi 2010, Afrika pamoja na rasilimali ilizonazo, imepoteza Dola 1.4 trilioni za Marekani kutokana na uongozi mbovu.

“Mojawapo ya sababu ni kwa kuwa hakuna mwendelezo kwa viongozi wanapobadilishana madaraka. Katika awamu ya tano kumekuwa na changamoto kubwa ambazo takwimu hizi zinashabihiana kuwa tutaendelea tena kupoteza mali tulizonazo kutokana na uongozi,” alisema mchungaji huyo wa Kanisa la Vineyard.

Tanzania Daima
 
Wabunge gani hawa?

IMG_20170418_083009.jpg
 
Back
Top Bottom