Wabunge wa UKAWA watoka kinyonge sana tena leo 17 Juni, 2016

Mabula83

Member
May 10, 2016
49
57
Leo nimegundua kitu kumbe hawa wabunge wa ukawa wanaonekana kuna wanaojitambua na wasiojitambua nimemuona Mh Mbatia asubuhi ya leo akikataa kutoka bungeni lakini wengine wakikomaa kutoka

Binafsi nampongeza Mbatia kwa kuonyesha kutokubaliana na suala zima la kutoka mjengoni namshauri aongee na hao wenzake wabaki tu hakuna kitu kisicho na mwisho kwenye dunia hii bana isitoshe wao ni wanasiasa lazima wajue jinsi ya kucheza na siasa

Mh Mbatia big up umesomeka sana tu na tupo tunaokuunga mkono kwa hilo komaa na hao wachanga wa siasa
 
Leo nimegundua kitu kumbe hawa wabunge wa ukawa wanaonekana kuna wanaojitambua na wasio jitambua nimemuona Mh Mbatia asubuhi ya leo akikataa kutoka bungeni lakini wasiojitambua wakikomaa kutoka

Binafsi nampongeza Mbatia kwa kuonyesha kutokubaliana na suala zima la kutoka mjengoni namshauri aongee na hao wenzake wabaki tu hakuna kitu kisicho na mwisho kwenye dunia hii bana isitoshe wao ni wana siasa lazima wajue jinsi ya kucheza na siasa

Mh Mbatia big up umesomeka sana tu na tupo tunaokuunga mkono kwa hilo komaa na hao wachanga wa siasa
Mkuu, hata mie nimeshtushwa sana na hali hiyo. Nimemuona Mheshimiwa James Mbatia licha ya kwamba amekaa mstari wa mbele ila amekuwa mtu wa mwisho kutoka Bungeni. Ni kama alikuwa anasubiri kitu fulani. Na bado
 
Cha msingi wametoka wote...hata wanavyotoka wanawawakilisha wananchi pia.Waliowanyonge zaidi ni hao wa CCM mkuu ambao wamegeuza bunge kuwa kikao cha chama.
 
Mungu alikuwa ana maana yake sana kumpa kila mwanadamu kichwa chake ili aweze kufikiri na kuamua mwenyewe baada ya kutafakari.

Kumuacha mtu mwingine kutumia kichwa chake na kukuamulia la kufanya ni ukosefu wa busara na kutokubali maamuzi ya hekima aliyoyafanya mwenyezi Mungu kwa waja wake.
Akili ni nywele kila mtu Mungu Kampa zake.

Lakini si zile za bandia.

Asalam aleykumu wabunge wote.
 
Kila mbunge mwisho wa siku atahukumiwa na wapiga kura wake. Sina hakika lakini nafikiri kuna wabunge wengine wapo mjengoni kitambo na majimboni kwao shida za wananchi zimeshatatuliwa, lakini wengine ndiyo kwanza wameanza na majimboni kwao kuna mahitaji mengi ya wapiga kura.

Waheshimiwa wabunge tafakarini na mchukue hatua.
 
alikuwa anafuatilia bado kama kuna ccmmmm waliobakiwa na mdondo ila dawa imewapata vilivyo wabunge wa fissssim
 
BUNGE la bajeti linaloendelea mjini Dodoma, juzi limehudhuriwa na wabunge 85 badala ya 277 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya wenzao wa Kambi ya Upinzani kususa vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson kwa madai kuwa hawana imani naye.

Bunge la Jamhuri ya Muungano lina jumla wa wabunge 395, kati yao 118 ni kutoka vyama vya upinzani na 277 ni wa CCM wakiwamo wateule wa rais.

Sasa hawa wana tofauti gani na wabunge wa upinzani waliosusia bunge, je na wao wakatwe posho?

Kwa habari kamili soma Mtanzania Bunge ladoda, wabunge 85 wajadili bajeti
 
Kweli niliona, tofauti na siku zingine leo walikuwa wanyonge mno. Comrade amewashika akili, wengine zimeanza kuwarudi.
 
Hivi kwani wenyeviti wa bunge yule dada, Mzee wa vijisenti na Zungu hawapo hapo bungeni mpaka huyu dada kukomaa hivi. Anafaidisha nani. Haya magamba yanachukia dada kukalia kila siku kiti. Awaachie basi na wenzake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom