Barbarosa hiyo Posho hawalipwi kama hisani bali ni stahili yao inayotokana na wao kuchaguliwa na wananchi, pia Magufuli hana hiyari ya kuwalipa au kutokuwalipa kwani hata yeye hizo pesa hazitokani na kuuza Mifugo ya Familia yao bali zinatokana na Kodi tunazotozwa watanzania wote waliomchagua na wasiomchagua Magufuli!! Na wala hizo Posho hazitokani na fedha zilizopatikana kwa kuuza kadi za CCM hivyo wabunge toka vyama vingine wakose sifa za kupewa!!
Kutokwenda kwenye sherehe za kuapishwa kwa Magufuli hakuko Kikatiba bali hizo posho zinatokana na sheria zilizotungwa kwa kufuatisha Katiba iliyopo inayoshabikiwa na CCM hata kama ni Hovyo kabisa!! Kuna ujinga miongoni mwetu kuona kama serikali inafanya mambo kwa hisani jambo ambalo si sahihi.