Kwa vyovyote vile ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa ccm sasa wanatapatapa na ahadi yao ya kuwaletea waislamu mahakama ya Kadhi huku Tanganyika! Ili kuwatumia waislamu na kupata kura zao kwa wingi katika uchaguzi uliopita ccm walitoa ahadi hii huku wakijua hawakujiandaa kuitekeleza na hata hawakujua uendeshwaji wa mahakama hizo utakuwaje na kwa gharama za nani.
Hata katika katiba ya Chenge iliyopitishwa na ccm katika Bunge Maalumu la Katiba ya ccm chini ya Sitta bado ccm ilishindwa kutekekeza ahadi yao hiyo na hivyo kushindwa kuiweka mahakama ya Kadhi ktk Katiba hiyo. Kitendo hicho kiliamsha hasira na madai mapya ya Mahakama hiyo kwa waislamu! Hapo ndipo Waziri mkuu Pinda alipolazimika kuingilia kati mwishoni na kuwaahidi waislamu(waliokuwa BMK na walio nje) kuwa serikali ya ccm ingepeleka muswada bungeni wa mabadiliko ya sheria ili mahakama ya Kadhi iweze kutambulika kama muswada utapita ( na kwa jinsi maccm walivyo wengi bungeni basi wanao uwezo wa kuupitisha hata bila UKAWA kuupitisha).
Sasa angalizo lipo hapa:
1. Wabunge wa UKAWA kuweni makini wakati wa mjadala huo kwasababu ccm watataka nyie ndiyo mchangie sana ili muonekane kama nyie ndiyo mliokwamisha endapo mtaukataa ili kuichonganisha UKAWA na waislamu. Hili linategemewa sana baada ya zile propaganda za ccm kuwa CHADEMA ni chama cha wakristo kufeli, hasa wakati huu ambapo UKAWA umeundwa ikijumuisha watu wa dini zote.
2. Ccm wanajua tayari kuwa muswada huo wataupitisha au hawataupitisha kwa wingi wao, lakini wanachokitafuta hapo ni kuwaingiza katika mtego wabunge wa UKAWA. Hivyo basi ikiwezekana UKAWA wote wawe wa mwisho kabisa kusema neno kwenye huo muswada, ili kama ccm wataupitisha wapitishe na kama wataukwamisha waukwamishe wenyewe. UKAWA mje kumalizia tu mwisho kwa uamuzi ambao mtaona ni sahihi kulingana na ccm watakavyoamua. Hapo mtakuwa mmekwepa kuingizwa chaka na mafisadi.
3.Msiwape sababu ccm eti kwamba serikali yao sikivu (kama wanavyoiita wenyewe) kuwa ilipeleka muswada bungeni lakini UKAWA wakaupinga! Msikubali huo ujinga.
4. Muswada huo wa mahakama ya Kadhi kwa jinsi ulivyo ni bomu, ni feki na hautekelezeki kisheria!
Ni usanii mtupu kwasababu;
(a) Hauna tamko la kisheria la uanzishwaji wa mahakama hizo(Establishing Provision) kinachounda rasmi mahakama hiyo. Badala yake kuna tamko tu la kuitambua mahakama hiyo( huwezi kutambua kitu ambacho hakipo kisheria, hakijaanzishwa rasmi). Maamuzi yeyote ya mahakama hizi yaweza kuwa VOID kama hazitambuliki na sheria mama.
(b) Mahakama hizo hazijapewa muundo au ngazi za maamuzi eg ngazi ya awali ya shauri fulani, ngazi inayofuatia na ngazi ya mwisho.
(C) Mamlaka zake hazijaainishwa(jurisdiction) yake kijiografia wala kithamani. Kwamba ngazi hii inaanzia eneo lipi hadi wapi na kwa kesi za thamani ipi labda.
(d) Sifa za kuwa Kadhi hazijatajwa, hivyo unaweza kuwa na mahakama hii na bado ukawa na Kadhi asiye na vigezo kwa mujibu wa vigezo vya waislamu.
(e) Hakuna usalama wa ajira za Kadhi etc
HIVYO NASEMA UKAWA KAENI KIMYA KABISA KWENYE HUO MUSWADA, WAACHIENI CCM WAJIAMULIE AHADI YAO.. MAHAKAMA IJE AU ISIJE ITAJULIKANA MBELE YA SAFARI. MSIKUBALI KUTEGWA.