Wabunge Wa Tanzania kwanini hawaombi mwongozo

Makusudically

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
2,203
1,235
Nashangaa Wabunge wetu ambao kimsingi ndiyo Watu ambao tuliwachagua ili wakatuwakilishe hususan wakati wa maslahi mapana ya Taifa.

Nilitegemea Wahoji na Waombe mwongozo ili Bunge lisimamishe mijadala mingine na kutoa mda kujadili report ya Michanga na Makampuni ya Uchimbaji madini. Chakushangaza badala yake Wabunge wetu baadhi yao bila hata aibu wanajitokeza hadharani kubeza , kulaumu, na hata kuwaunga mkono waporaji wa Raslimali zetu. Bila kujali kuwa Report imeeleza kila kitu nakudhihirisha kuwa pasipo shaka tunapoteza pesa nyingi sana.

Tulitegemea badala ya kulaumu juu ya mikataba iliyoingiwa kimakosa na utawala wowote ule wa chama chochote kile, Kwa hakika kwenye hili hakuna kupoteza wakati kulaumiana, cha msingi ni kuweka mijadala mizito ta kutafuta namna ya kulikwamua Taifa kutokana na uporwaji huu wa Raslimali zetu.

Niwaombe Wabunge, Watanzsnia wote na wale wote ambao kwa hakika tunaguswa na matokeo ya uhakiki wa michanga yenye Makinikia kibao ambayo yameonekana kutoroshwa, basi tuunge mikono juhudi hizi na kila mmoja kwa nafasi yake aliyo nayo aobeshe kwa namna atakavyoweza kukerwa na yporwaji huu.
 
Wabunge wetu kwa umoja wao ndio waliopitisha mkataba mibovu iliyotufikisha hapa tulipo.

Natamani ile nguvu na umoja wao wanaokuwa nao kwenye mambo yanayogusa maslahi yao wangekuwa nao hata kwenye mambo yanayogusa maslahi ya taifa.
 
Kwa wabunge madini si issue yenye Maslahi kwa Taifa kwa sababu wanajua wameshikwa pabaya na Mwenye mamlaka na muhimili wa dola!!
 
Unaposema wabunge "wenu" unamaanisha wale wachumia tumbo, wagonga meza na waropokaji wa "ndiyoooo"?
Kama ndivyo..!! Sasa wataanzaje kuomba miongozo ilhali wao ndo wametufikisha hapa tulipo??

[HASHTAG]#Someni[/HASHTAG] [HASHTAG]#Namba[/HASHTAG]
 
Nashangaa Wabunge wetu ambao kimsingi ndiyo Watu ambao tuliwachagua ili wakatuwakilishe hususan wakati wa maslahi mapana ya Taifa. Nilitegemea Wahoji na Waombe mwongozo ili Bunge lisimamishe mijadala mingine na kutoa mda kujadili report ya Michanga na Makampuni ya Uchimbaji madini. Chakushangaza badala yake Wabunge wetu baadhi yao bila hata aibu wanajitokeza hadharani kubeza , kulaumu, na hata kuwaunga mkono waporaji wa Raslimali zetu. Bila kujali kuwa Report imeeleza kila kitu nakudhihirisha kuwa pasipo shaka tunapoteza pesa nyingi sana. Tulitegemea badala ya kulaumu juu ya mikataba iliyoingiwa kimakosa na utawala wowote ule wa chama chochote kile, Kwa hakika kwenye hili hakuna kupoteza wakati kulaumiana, cha msingi ni kuweka mijadala mizito ta kutafuta namna ya kulikwamua Taifa kutokana na uporwaji huu wa Raslimali zetu. Niwaombe Wabunge, Watanzsnia wote na wale wote ambao kwa hakika tunaguswa na matokeo ya uhakiki wa michanga yenye Makinikia kibao ambayo yameonekana kutoroshwa, basi tuunge mikono juhudi hizi na kila mmoja kwa nafasi yake aliyo nayo aobeshe kwa namna atakavyoweza kukerwa na yporwaji huu.
mkuu...una wabunge wa CCM?
maana wabunge wa upinzani wamekuwa wakiomba mwongozo kuhusu wizi huu huu kwa miaka karibia 20 sasa!
 
Back
Top Bottom