Wabunge wa CHADEMA wamkaribisha Lowassa

Wabunge wa CHADEMA wamkaribisha Lowassa

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
Baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamezungumzia taarifa zinazosambaa zikieleza kuwapo mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho, wengi wao wakimkaribisha.

Wakati wabunge hao wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea mitandao ya kijamii.

“Nitazungumza pale mambo yatakapokuwa sawa, siwezi kuzungumza sasa, subirini… sasa hivi mambo mengi yanazungumzwa kwenye mitandao,” alisema Dk Slaa ambaye pia anatajwa kuwa mgombea wa chama hicho ndani ya Ukawa.

Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa ni suala la mtu binafsi. Hata hivyo, jitihada za kumpata Lowassa jana hazikufanikiwa kwani simu yake iliita pasi na kupokewa.

Hivi karibuni, idadi kubwa ya madiwani wa CCM walirudisha kadi zao na kujiunga na Chadema wakisema sababu ni kutoridhishwa na kukatwa kwa jina Lowassa kati ya wagombea urais wa CCM.

Kadhalika, mtandao wa kijamii uliokuwa ukimuunga mkono mbunge huyo wa Monduli unajulikana kwa jina la 4U Movement ulitangaza kuhamia CHADEMA hali inayoashiria kuwa kuna dalili ya Lowassa pia kujiunga nao.

Wakiandika katika akaunti ya Twitter ya 4U Movement, wafuasi hao walisema: “Ukimya ni hekima na ukimya ni busara. Ukimya wa Edward Lowassa ni kutafakari Safari ya Matumaini... Tuungane kuyapata mabadiliko nje CCM.”

CHADEMA ni kanisa la wokovu

Akizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.

“CHADEMA ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi,” alisema.

Kuhusu viongozi wa CCM kuhamia CHADEMA, Msigwa alisema inawezekana kasi hiyo inachagizwa na Lowassa kukosa nafasi aliyoitaka ndani ya chama hicho.

“Unapokuwa mwanasiasa unakuwa na wafuasi, inawezekana wengine wanaohamia CHADEMA ni watu wake ambao wameona mtu wao amekosa nafasi aliyoitaka ndiyo maana wanakihama chama,” alisema.

Msigwa alisema CHADEMA ilikuwa inakusanya wanachama wapya kwa muda mrefu hata kabla ya vuguvugu la Lowassa na chama chake kuibuka na ushindi na wanaohamia wanafanya hivyo kwa sababu wanakipenda chama na wameichoka CCM.

Huenda akatimiza safari ya matumaini

Akizungumzia ujio wa Lowassa kwenye chama hicho, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema iwapo Lowassa atahamia CHADEMA anakaribishwa na huenda akaitimiza safari yake ya matumaini.

“Namkaribisha Lowassa CHADEMA, huenda safari yake ya matumaini ikaishia huku, akawa mwanachama au hata kiongozi,” alisema.

Alisema hakuna shaka kuwa mbunge huyo wa Monduli ana nguvu ndani ya CCM ndiyo maana viongozi wengi wa chama hicho wanakihama wakati huu.

“Hiyo ilijionyesha kuanzia kwenye Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu, Lowasa amekamata wajumbe kwa asilimia 80 na hiyo ni ishara kuwa ameishika CCM,” alisema.

Lema aliongeza kuwa wanaoihama CCM hawaihami kwa bahati mbaya, bali wameona mtu wao waliyemtarajia ameondoka.

“Ni wengi wanaohamia CHADEMA, kwa sasa kadi zimetuishia na hiyo ni ishara kuwa CCM inakufa, ripoti za mikoa yote tunazo,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya alisema wanaoihama CCM kwa sasa wamegundua kuwa chama pekee kinachoweza kutetea wananchi ni CHADEMA.

“Sisi tunawakaribisha kwa mikono miwili, waje tuchape kazi, ilimradi wanafuata kanuni na taratibu za chama, basi. Wamejionea wenyewe kuwa CCM hakuna chochote,” alisema.

Alisema CCM waliamua kupitisha katiba bila kuwapo kwa Ukawa, lakini sasa wameona kuwa walichokifanya ni makosa na wameanza kurudi CHADEMA ambako wanaamini kuna demokrasia ya kweli.

Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso alisema: “Tunamkaribisha kwa mikono miwili. Tumekinyooshea CCM vidole kwa muda mrefu kuwa kuna rushwa na makundi na hilo linajidhihirisha sasa. Lakini wale wote wanaokuja CHADEMA, tunawakaribisha ili mradi wafuate kanuni na taratibu zetu.”

Paresso alisema hana tathmini ya kina kuhusu wafuasi wa Lowassa wanaoihama CCM, bali wanaokihama chama hicho wameona kina matatizo.

Atakiwa akidhi vigezo na masharti

Licha ya kuonyesha kumkaribisha, katika chama hicho, baadhi ya wabunge walimtaka Lowassa afuate kanuni ili awe mwanachama mwenye sifa.

Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde alisema anakaribishwa lakini hana budi kufuata sheria na kanuni za chama... “Anatakiwa afuate taratibu za chama, milango ipo huru, lakini afuate kanuni… asije akafikiri ataleta taratibu zake hapa, sitakubali.”

Silinde alisema wanaohamia CHADEMA hawajapendezwa na mwenendo mzima wa uteuzi wa mgombea wa urais na hivyo wameifuata demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo lakini alisema endapo atajiunga, chama hicho kitampokea kulingana na vigezo na taratibu.

“Akihamia CHADEMA nitatoa maoni yangu lakini ninachoweza kusema ni kuwa kila mtu ana haki ya kwenda chama chochote ili mradi ana tija,” alisema.

Mdee alisema wanaCCM wanaohamia CHADEMA wamesoma alama za nyakati na kuona kuwa CCM haiendani na ahadi zake.

Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo alisema, Lowassa ni binadamu wa kawaida kwa hiyo kuhamia kwake CHADEMA si kitu cha ajabu ilimradi afuate kanuni... “Cha muhimu afuate masharti ya chama, kanuni na taratibu, kama watu wanahama vyama vingine yeye ni nani asihame CCM?”

Lyimo alisema wanaCCM wengine wanakaribishwa kujiunga kwa sababu kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul, aliwataka wana CCM na Lowasa kuhamia zaidi Chadema ili kuunganisha nguvu na kuichukua nchi.

“Mfikishie salamu Lowassa mwambie karibu kwenye jeshi la ukombozi,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu tutaona na kusikia mengi.

Binadamu unapokuwa katika mazingira ya kufa na njaa unaweza hata kula kinyesi chako!

Wanasiasa wanapokuwa katika mazingira ya do or die, hawaoni hata aibu kula matapishio yao ya kisiasa!

Kwa jinsi trends za kiuchumi na kisiasa zinavyojionyesha hapa Tanzania, kama wapinzani hawataingia Ikulu katika uchaguzi huu, basi wasahau tena kwa miaka 10+

Ni vigumu sana katika chaguzi za Africa kumwondoa madarakani Rais anayegombea (defeat incumbent president)

Huu ndiyo mwaka ambao wapinzani wana nafasi baada ya Rais Kikwete kuzuiwa na Katiba!

Hata hivyo nina wasi wasi kama wataweza kumpiga chini Magufuli ambaye anasaidiwa na Sheria za Uchaguzi achilia mbali kukubalika kwake nchini.

CHADEMA is trying to throw the kitchen sink at CCM!
 
Yule Mzee Wasira aliyesema Upinzani mpaka kukaribia uchaguzi watakuwa wamesha futika kama ilivyotokea kwa vyama vilivokuwa tishio kwa CCM mbona simsikie na utabiri wake?.
 
kimtazamo japo wanasem watashind kwa goli la mkono lakini kwa nguvu ya lowassa sitarajii kama wawakilishi wetu katka vituo vya kuhesabia kura watahongwa kirahisi...hii ni ishara tutashinda viti vingi vya ubunge hata tusiposhinda uraisi
 
Ng'wanamapalala, Lowasa ameshindwa kuirubuni ccm kwa usanii wake. Sasa ccm imefurahia kudhibiti mafuriko ya kifisadi kwa vidole, kelele za nini tena?

Ninashauri endeleeni kumnadi yeboyebo wenu mnayeamini ni mtu sahihi kabisa kuwa mwenyekiti wa ccm kulilko wanaccm wote. Habari za Lowasa achaneni nazo kwa sababu hana madhara kwenu tena. Mmeshajikomboa, hizi tararila na taarabu zote juu ya lowasa za nini tena?

Nami naungana na wengine kwamba Lowasa ni mtanzania kama watanzania wengine. Anauhuru wa kutokushiriki ama kushirika siasa na chama chochote akipendancho na hakuna sheria inamzuia. Masuala yake na wenyeji wake kama ni kweli, aachiwe yeye na wenyeji wake wamalizane na si jukumu la ccm tena kufuatilia anakwenda wapi kufanya siasa na nani kwa taratibu gani.

CHaDEMA ni chama kikubwa kuliko vyama vyote vya siasa Tanzania. Kinasera ya mlango wazi kwa kila mtu ili mradi afuate sheria za chama. Sasa lowasa kama akiamau kufuata sheria na taratibu atakazokuwa kawekewe na CHaDEMA kama ataamua kujiunga nacho, kuna tatizo gani? Kazi ya CHaDEMA ni kunoa wanachama wake wapya including Lowasa kama atajiunga kutoka ghafi kuwa safi ndani ya chama. Hilo waachieni wao anajua taratibu na kanuni zao.

Ccm isonge mbele kutatua migogoro yao, iwaache UKaWA nao waendelee na uimarishaji wa umoja wao na vyama vyao.

Siku njema.
 
Yule Mzee Wasira aliyesema Upinzani mpaka kukaribia uchaguzi watakuwa wamesha futika kama ilivyotokea kwa vyama vilivokuwa tishio kwa CCM mbona simsikie na utabiri wake?.

Huwezi kushindana na wakati halafu ushinde....WAKATI SI MILELE....!!! Hakuongozwa na hekima aliposema vile bali mihemko ya kisiasa
 
Eti LOWASSA amtaka ZITTO kuwa waziri mkuu endapo atapitishwa kupeperusha bendera ya UKAWA kama ndo matakwa yake bora asipokelewe kabisa kwani hana dhamira ya dhati ya kumkomboa mtanzania.
 
Hapa naona CCM inatapatapa inachanganyikiwa wamejawa na woga wasijue lakufanya wamebaki wapweke kutokana na kila mtu kuchukuwa fito zake. Wamebaki kutafakari, je tuijengeje nyumba iliyovunjika? Tupateje Lishe safi ya watoto wenye utapiamulo. Hii ndiyo CCM ya kila MTU aliyeoondoka na kipande chake!
 
Kila jambo lina wakati wake. Nyakati za mwisho wa CCM ni sasa maazingira yote yanazitokeza. Huu ni wakati wa upinzani hususani CDM kuchukua nchi. Ila kama michezo mingine ni lazima wawe making katika lala salama hii.
 
Yule Mzee Wasira aliyesema Upinzani mpaka kukaribia uchaguzi watakuwa wamesha futika kama ilivyotokea kwa vyama vilivokuwa tishio kwa CCM mbona simsikie na utabiri wake?.

Acheni kumjadili kiongozi mwenye heshima zake kama Mhe Wasira. Nyie subirini kumkaribisha fisadi papa na vidagaa vyake vilivyotangulia, Mbowe anauza chama kwa tamaa ya pesa! Ama kweli fedha fedheha! Tungoje speech ya Slaa kuhusu list ya mafisadi papa 11 sijui ataibadili! Msipoangalia chadema ndio kitageuka chama cha mafisadi, Msubirini na Karamagi,Rostam, na wenzake wengi tu.
 
Kila mabadiliko yanafanywa na mtanzania mwenyewe. .. kama kweli tunataka mabadiliko kila mmoja ni wajibu kujichukulia kuwa ni wathamani na viongozi hutuheshimu kabla ya kupiga kura lakini baada ya hapo thamani zetu hushuka zaidi ya kitoweo cha sikukuu. Changes are by you and me tujiandikishe tupige kura tuchague njia sahihi.... jiwe gizani mhusika atatoa sauti....
 
Wakuu,
Mtanisamehe kwa kutokuunga mkono ujio wa Edo CDM. Kiukweli kabisa chadema haikutakiwa imsubiri mtu ili imfanye kuwa mgombea wao. Chama kimekomaa kisiasa, hao watu wa ccm wanaojiunga na CDM na wanapokelewa kwa shamra shamra kubwa ni udhaifu uliopitiliza kwa chama changu. Wapo wenye uwezo wa kuongoza chama na wenye uwezo wa kuwa raisi wa jamhuri.

Nachelea kusema kuwa upinzani bado hatujajua lengo letu ni kitu gani na tunataka kufanya nini. Ninachokiona wazi ni maamuzi magumu ya kula matapishi yetu wenyewe. Tulihubiri na kuwasihi watu kwamba mafisadi hawatakiwi tena kwenda ikulu. Dr Slaa kwa kinywa chake akiwa na akili timamu aliwataja akina Edo kwamba ni vinara wa ufisadi Tanzania, kumbukeni "list of shame", leo tumeshau?! Hainingii akilini hata kidogo eti leo Lowassa anaonekana kuwa msafi pale tu atakapokuja CDM, ila akiwa CCM ni msafi, narudia huu ni upungufu wa akili mkubwa na kutokuwa na kumbukumbu.

Nawaomba CDM, chonde chonde, kuweni na maamuzi yenye tija, acheni kukumbatia maslahi yenu binafsi. Na endapo Edo ataenda CDM, huu ni ushindi kwa CCM, maana watatumia nafasi hii kwamba wao waliwakataa mafisadi ila wapinzani wakawapokea. kwa namna moja au nyingine watu watarudisha imani kwa CCM. Tufanye jitihada za dhati kuongeza wabunge wa upinzani, raisi tuangalie mtu huko huko UKAWA na sio kumsubiri Edward eti atakuja na watu kutoka CCM.

Watanzania tumekuwa na akili fupi kiasi kikubwa na hatuna dira kabisa, hii ni ishara kwamba hata upinzani utafanya yale yale yanayofanywa na CCM, na hawatakuwa na jipya kamwe!!!!!

C.C
Ben Saanane,
Tumaini Makene,
Kurugenzi ya Habari. et al.
 
Yaani baada ya miaka yote hii ya kupambana na ufisadi, na kuwa na wazalendo wanaoipenda nchi kwa moyo na kuchukia ufisadi toka moyoni; yaani kweli bila aibu Viongozi wetu wanasimama na kukaribisha mafisadi wale wale tuliowasuta waje katika chama ambacho hadi juzi niliamini tuko pamoja katika vita ya ufisadi; kumbe hatuko serious? imeniuma sana hadi jana nimekosa usingizi.

Mwenyekiti Mbowe pokea ujumbe huu: Mpokee Lowasa wako lakini tegemea wapiganaji wote tutaondoka CDM na kukuacha na Fisadi wako. Hivi hata akili ndogo huna? hadi ifikie mtu kukataliwa na CCM si maovu yake yamefika hadi kuzimu? Unadhani anashindwa kukinunua haka kaCDM ketu? Kama aliweza kununua kura za ushindi CCM HADI AKAKATWA JUU KWA JUU atashindwa nini na CDM?
Be warned!!!!

Chadema si kanisa wala msikiti kuwa walio wachafu waje na kutubu, wachafu ni wachafu tu mbele ya haki, mngetoa tamko rasmi wachafu wabaki huko huko kuchafu sio kuja CDM. Sasa ndio mnatuletea aibu gani hii Mwenyekiti? tutaficha wapi nyuso zetu sisi makamanda tuliokijenga chama kwa misingi ya upambanaji wa ufisadi?

Leo kweli mnawaleta tena? Hapana, hapana jamani Siku hiyo hiyo Lowassa amaingia Chadema mtegemee tunaochukia ufisadi toka moyoni tutatoka Chadema. M/kiti, Kumbe wewe na wenzako ni wanafiki?

Tuamini CDM HAINA ITIKADI? inaniuma sana.
 
Mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu tutaona na kusikia mengi.

Binadamu unapokuwa katika mazingira ya kufa na njaa unaweza hata kula kinyesi chako!

Wanasiasa wanapokuwa katika mazingira ya do or die, hawaoni hata aibu kula matapishio yao ya kisiasa!

Kwa jinsi trends za kiuchumi na kisiasa zinavyojionyesha hapa Tanzania, kama wapinzani hawataingia Ikulu katika uchaguzi huu, basi wasahau tena kwa miaka 10+

Ni vigumu sana katika chaguzi za Africa kumwondoa madarakani Rais anayegombea (defeat incumbent president)

Huu ndiyo mwaka ambao wapinzani wana nafasi baada ya Rais Kikwete kuzuiwa na Katiba!

Hata hivyo nina wasi wasi kama wataweza kumpiga chini Magufuli ambaye anasaidiwa na Sheria za Uchaguzi achilia mbali kukubalika kwake nchini.

CHADEMA is trying to throw the kitchen sink at CCM!
Mkuu tumechoka na literature zako kuhusu lowassa sasa kama huna chakuandika bora uuchune
 
Rudi lumumba ukale unga, unatafuta nini? Ondoa kupayuka payuka kwako hapa, nani alikuambia tatizo la Watanzania liko kwa mtu fulani, sisi tunapambana kubomoa mfumo wa kikoloni wa ma-CCM wewe unabwabwaja mate yatusaidie nini..... tutatumia silaha zote kuufumua hata Kikwete akija atapewa shule na kuambiwa kaa hapa uwajibike chini ya mfumo imara.

Nini kinakuuma, kwa nini usiumie kwa Elimu duni, huduma za afya mbovu, maji hakuna, umeme utafikiri ni kibatari kinapulizwa na upepo na kuzimazima........ bilaliful

Yaani baada ya miaka yote hii ya kupambana na ufisadi, na kuwa na wazalendo wanaoipenda nchi kwa moyo na kuchukia ufisadi toka moyoni; yaani kweli bila aibu Viongozi wetu wanasimama na kukaribisha mafisadi wale wale tuliowasuta waje katika chama ambacho hadi juzi niliamini tuko pamoja katika vita ya ufisadi; kumbe hatuko serious? imeniuma sana hadi jana nimekosa usingizi.
Mwenyekiti Mbowe pokea ujumbe huu: Mpokee Lowasa wako lakini tegemea wapiganaji wote tutaondoka CDM na kukuacha na Fisadi wako. Hivi hata akili ndogo huna? hadi ifikie mtu kukataliwa na CCM si maovu yake yamefika hadi kuzimu? Unadhani anashindwa kukinunua haka kaCDM ketu? Kama aliweza kununua kura za ushindi CCM HADI AKAKATWA JUU KWA JUU atashindwa nini na CDM?
Be warned!!!!
Chadema si kanisa wala msikiti kuwa walio wachafu waje na kutubu, wachafu ni wachafu tu mbele ya haki, mngetoa tamko rasmi wachafu wabaki huko huko kuchafu sio kuja CDM. Sasa ndio mnatuletea aibu gani hii Mwenyekiti? tutaficha wapi nyuso zetu sisi makamanda tuliokijenga chama kwa misingi ya upambanaji wa ufisadi? leo kweli mnawaleta tena? Hapana, hapana jamani Siku hiyo hiyo Lowassa amaingia Chadema mtegemee tunaochukia ufisadi toka moyoni tutatoka Chadema. M/kiti, Kumbe wewe na wenzako ni wanafiki? tuamini CDM HAINA ITIKADI? inaniuma sana.................
 
Wakuu,
Mtanisamehe kwa kutokuunga mkono ujio wa Edo CDM. Kiukweli kabisa chadema haikutakiwa imsubiri mtu ili imfanye kuwa mgombea wao. Chama kimekomaa kisiasa, hao watu wa ccm wanaojiunga na CDM na wanapokelewa kwa shamra shamra kubwa ni udhaifu uliopitiliza kwa chama changu. Wapo wenye uwezo wa kuongoza chama na wenye uwezo wa kuwa raisi wa jamhuri.

Nachelea kusema kuwa upinzani bado hatujajua lengo letu ni kitu gani na tunataka kufanya nini. Ninachokiona wazi ni maamuzi magumu ya kula matapishi yetu wenyewe. Tulihubiri na kuwasihi watu kwamba mafisadi hawatakiwi tena kwenda ikulu. Dr Slaa kwa kinywa chake akiwa na akili timamu aliwataja akina Edo kwamba ni vinara wa ufisadi Tanzania, kumbukeni "list of shame", leo tumeshau?! Hainingii akilini hata kidogo eti leo Lowassa anaonekana kuwa msafi pale tu atakapokuja CDM, ila akiwa CCM ni msafi, narudia huu ni upungufu wa akili mkubwa na kutokuwa na kumbukumbu.

Nawaomba CDM, chonde chonde, kuweni na maamuzi yenye tija, acheni kukumbatia maslahi yenu binafsi. Na endapo Edo ataenda CDM, huu ni ushindi kwa CCM, maana watatumia nafasi hii kwamba wao waliwakataa mafisadi ila wapinzani wakawapokea. kwa namna moja au nyingine watu watarudisha imani kwa CCM. Tufanye jitihada za dhati kuongeza wabunge wa upinzani, raisi tuangalie mtu huko huko UKAWA na sio kumsubiri Edward eti atakuja na watu kutoka CCM.

Watanzania tumekuwa na akili fupi kiasi kikubwa na hatuna dira kabisa, hii ni ishara kwamba hata upinzani utafanya yale yale yanayofanywa na CCM, na hawatakuwa na jipya kamwe!!!!!

C.C
Ben Saanane,
Tumaini Makene,
Kurugenzi ya Habari. et al.

Ndugu nimekuelewa sana lakini kumbuka asilimia kubwa ya wanachama walitoka CCM na wachache hawakuwa na chama.Sasa unaposema tusiwakubali wanachama wapya kwa hofu ya ufisadi huoni unawanyima watu Uhuru wa kujiunga na chama chochote bila kikwazo ilimradi kukubaliana na katiba ya chama unachojiunga.Ufisadi unaendana na mfumo wa chama au taasisi ilivyojipambanua.Inawezekana ukawa wewe hupendi rushwa na ufisadi lakini ukakuta utaratibu wa chama,shirika na taasisi inaruhusu na wewe lazima ufuate hali inavyotaka.
 
Back
Top Bottom