Wabunge wa CHADEMA wamkaribisha Lowassa

Wabunge wa CHADEMA wamkaribisha Lowassa

Baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamezungumzia taarifa zinazosambaa zikieleza kuwapo mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho, wengi wao wakimkaribisha.

Wakati wabunge hao wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea mitandao ya kijamii.

"Nitazungumza pale mambo yatakapokuwa sawa, siwezi kuzungumza sasa, subirini… sasa hivi mambo mengi yanazungumzwa kwenye mitandao," alisema Dk Slaa ambaye pia anatajwa kuwa mgombea wa chama hicho ndani ya Ukawa.

Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa ni suala la mtu binafsi. Hata hivyo, jitihada za kumpata Lowassa jana hazikufanikiwa kwani simu yake iliita pasi na kupokewa.

Hivi karibuni, idadi kubwa ya madiwani wa CCM walirudisha kadi zao na kujiunga na Chadema wakisema sababu ni kutoridhishwa na kukatwa kwa jina Lowassa kati ya wagombea urais wa CCM.

Kadhalika, mtandao wa kijamii uliokuwa ukimuunga mkono mbunge huyo wa Monduli unajulikana kwa jina la 4U Movement ulitangaza kuhamia CHADEMA hali inayoashiria kuwa kuna dalili ya Lowassa pia kujiunga nao.

Wakiandika katika akaunti ya Twitter ya 4U Movement, wafuasi hao walisema: "Ukimya ni hekima na ukimya ni busara. Ukimya wa Edward Lowassa ni kutafakari Safari ya Matumaini... Tuungane kuyapata mabadiliko nje CCM."

CHADEMA ni kanisa la wokovu

Akizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.

"CHADEMA ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi," alisema.

Kuhusu viongozi wa CCM kuhamia CHADEMA, Msigwa alisema inawezekana kasi hiyo inachagizwa na Lowassa kukosa nafasi aliyoitaka ndani ya chama hicho.

"Unapokuwa mwanasiasa unakuwa na wafuasi, inawezekana wengine wanaohamia CHADEMA ni watu wake ambao wameona mtu wao amekosa nafasi aliyoitaka ndiyo maana wanakihama chama," alisema.

Msigwa alisema CHADEMA ilikuwa inakusanya wanachama wapya kwa muda mrefu hata kabla ya vuguvugu la Lowassa na chama chake kuibuka na ushindi na wanaohamia wanafanya hivyo kwa sababu wanakipenda chama na wameichoka CCM.

Huenda akatimiza safari ya matumaini

Akizungumzia ujio wa Lowassa kwenye chama hicho, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema iwapo Lowassa atahamia CHADEMA anakaribishwa na huenda akaitimiza safari yake ya matumaini.

"Namkaribisha Lowassa CHADEMA, huenda safari yake ya matumaini ikaishia huku, akawa mwanachama au hata kiongozi," alisema.

Alisema hakuna shaka kuwa mbunge huyo wa Monduli ana nguvu ndani ya CCM ndiyo maana viongozi wengi wa chama hicho wanakihama wakati huu.

"Hiyo ilijionyesha kuanzia kwenye Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu, Lowasa amekamata wajumbe kwa asilimia 80 na hiyo ni ishara kuwa ameishika CCM," alisema.

Lema aliongeza kuwa wanaoihama CCM hawaihami kwa bahati mbaya, bali wameona mtu wao waliyemtarajia ameondoka.

"Ni wengi wanaohamia CHADEMA, kwa sasa kadi zimetuishia na hiyo ni ishara kuwa CCM inakufa, ripoti za mikoa yote tunazo," alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya alisema wanaoihama CCM kwa sasa wamegundua kuwa chama pekee kinachoweza kutetea wananchi ni CHADEMA.

"Sisi tunawakaribisha kwa mikono miwili, waje tuchape kazi, ilimradi wanafuata kanuni na taratibu za chama, basi. Wamejionea wenyewe kuwa CCM hakuna chochote," alisema.

Alisema CCM waliamua kupitisha katiba bila kuwapo kwa Ukawa, lakini sasa wameona kuwa walichokifanya ni makosa na wameanza kurudi CHADEMA ambako wanaamini kuna demokrasia ya kweli.

Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso alisema: "Tunamkaribisha kwa mikono miwili. Tumekinyooshea CCM vidole kwa muda mrefu kuwa kuna rushwa na makundi na hilo linajidhihirisha sasa. Lakini wale wote wanaokuja CHADEMA, tunawakaribisha ili mradi wafuate kanuni na taratibu zetu."

Paresso alisema hana tathmini ya kina kuhusu wafuasi wa Lowassa wanaoihama CCM, bali wanaokihama chama hicho wameona kina matatizo.

Atakiwa akidhi vigezo na masharti

Licha ya kuonyesha kumkaribisha, katika chama hicho, baadhi ya wabunge walimtaka Lowassa afuate kanuni ili awe mwanachama mwenye sifa.

Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde alisema anakaribishwa lakini hana budi kufuata sheria na kanuni za chama... "Anatakiwa afuate taratibu za chama, milango ipo huru, lakini afuate kanuni… asije akafikiri ataleta taratibu zake hapa, sitakubali."

Silinde alisema wanaohamia CHADEMA hawajapendezwa na mwenendo mzima wa uteuzi wa mgombea wa urais na hivyo wameifuata demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo lakini alisema endapo atajiunga, chama hicho kitampokea kulingana na vigezo na taratibu.

"Akihamia CHADEMA nitatoa maoni yangu lakini ninachoweza kusema ni kuwa kila mtu ana haki ya kwenda chama chochote ili mradi ana tija," alisema.

Mdee alisema wanaCCM wanaohamia CHADEMA wamesoma alama za nyakati na kuona kuwa CCM haiendani na ahadi zake.

Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo alisema, Lowassa ni binadamu wa kawaida kwa hiyo kuhamia kwake CHADEMA si kitu cha ajabu ilimradi afuate kanuni... "Cha muhimu afuate masharti ya chama, kanuni na taratibu, kama watu wanahama vyama vingine yeye ni nani asihame CCM?"

Lyimo alisema wanaCCM wengine wanakaribishwa kujiunga kwa sababu kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul, aliwataka wana CCM na Lowasa kuhamia zaidi Chadema ili kuunganisha nguvu na kuichukua nchi.

"Mfikishie salamu Lowassa mwambie karibu kwenye jeshi la ukombozi," alisema.

Chanzo: Mwananchi
Mhe. Lowasa kuomba uanachama CHADEMA ni haki yake. CHADEMA kumkumbatia Mhe. Lowasa ni sawa na mtu mzima kula kujitukana mwenyewe au kutokuwa na msimamo.
 
speaking of a mind being at a cross road,i am so indifferent on this...should i welcome the white hair or should i smack the sh!t out of him.
 
Leo tujitokeze kwa wingi kuwasikiliza viongozi wetu wakuu wa Chadema, viwanja vya Magomeni Mwanza, pia mkutano huo utarushwa live na kituo cha ITV. Mbowe, Slaa, Prof. Safari, Mnyika na Salumu, pia wabunge waliohamia Chadema toka, Ester Bulaya na Lembele watawasha moto leo Mwanza.
 
Wakuu,
Mtanisamehe kwa kutokuunga mkono ujio wa Edo CDM. Kiukweli kabisa chadema haikutakiwa imsubiri mtu ili imfanye kuwa mgombea wao. Chama kimekomaa kisiasa, hao watu wa ccm wanaojiunga na CDM na wanapokelewa kwa shamra shamra kubwa ni udhaifu uliopitiliza kwa chama changu. Wapo wenye uwezo wa kuongoza chama na wenye uwezo wa kuwa raisi wa jamhuri.

Nachelea kusema kuwa upinzani bado hatujajua lengo letu ni kitu gani na tunataka kufanya nini. Ninachokiona wazi ni maamuzi magumu ya kula matapishi yetu wenyewe. Tulihubiri na kuwasihi watu kwamba mafisadi hawatakiwi tena kwenda ikulu. Dr Slaa kwa kinywa chake akiwa na akili timamu aliwataja akina Edo kwamba ni vinara wa ufisadi Tanzania, kumbukeni "list of shame", leo tumeshau?! Hainingii akilini hata kidogo eti leo Lowassa anaonekana kuwa msafi pale tu atakapokuja CDM, ila akiwa CCM ni msafi, narudia huu ni upungufu wa akili mkubwa na kutokuwa na kumbukumbu.

Nawaomba CDM, chonde chonde, kuweni na maamuzi yenye tija, acheni kukumbatia maslahi yenu binafsi. Na endapo Edo ataenda CDM, huu ni ushindi kwa CCM, maana watatumia nafasi hii kwamba wao waliwakataa mafisadi ila wapinzani wakawapokea. kwa namna moja au nyingine watu watarudisha imani kwa CCM. Tufanye jitihada za dhati kuongeza wabunge wa upinzani, raisi tuangalie mtu huko huko UKAWA na sio kumsubiri Edward eti atakuja na watu kutoka CCM.

Watanzania tumekuwa na akili fupi kiasi kikubwa na hatuna dira kabisa, hii ni ishara kwamba hata upinzani utafanya yale yale yanayofanywa na CCM, na hawatakuwa na jipya kamwe!!!!!

C.C
Ben Saanane,
Tumaini Makene,
Kurugenzi ya Habari. et al.

Umesomeka mkuu,,,hata kama yeye lowasa hatakubali kujiunga na CDM hizo kauli na tetesi za viongoz wa cdm kumtaka lowasa ajiunge nao zimekishushia hadhi cdm..mi najiondoa rasmi CDM
 
Gamba Ng'wamapalala

Kila Siku lazima uanzishe thread inayomhusu Lowassa na CHADEMA.
Acha wivu wa Kike Mkuu,muacheni Mzee wa watu afanye analoona linamfaa,huku kutapata kwenu Ma agents wa Magamba ni indication kuwa huyo Mzee Mnamgwaya sana.
 
Last edited by a moderator:
Rudi lumumba ukale unga, unatafuta nini? Ondoa kupayuka payuka kwako hapa, nani alikuambia tatizo la Watanzania liko kwa mtu fulani, sisi tunapambana kubomoa mfumo wa kikoloni wa ma-CCM wewe unabwabwaja mate yatusaidie nini..... tutatumia silaha zote kuufumua hata Kikwete akija atapewa shule na kuambiwa kaa hapa uwajibike chini ya mfumo imara.

Nini kinakuuma, kwa nini usiumie kwa Elimu duni, huduma za afya mbovu, maji hakuna, umeme utafikiri ni kibatari kinapulizwa na upepo na kuzimazima........ bilaliful
Wapumbavu kama wewe hawafundishiki, mmeona kuchukua watu wa mfumo ule ule, tena wanaotuhumiwa ufisadi ndio kuleta mabadiliko? au mmeshakuwa wachumia tumbo? Baada ya Lowasa kugawa fedha CCM na kuwagawa watu mnataka aje kugawa CDM na kutugawa? wewe na Mwenyekiti ni vibaraka, mnatakka hela za Lowasa , washenzi kabisa!!! na mkimpokea mtatukoma!!!! Shenzz!
 
Gamba Ng'wamapalala

Kila Siku lazima uanzishe thread inayomhusu Lowassa na CHADEMA.
Acha wivu wa Kike Mkuu,muacheni Mzee wa watu afanye analoona linamfaa,huku kutapata kwenu Ma agents wa Magamba ni indication kuwa huyo Mzee Mnamgwaya sana.

Sikiliza dogo, Huku CDM nilidhani fisadi hata akiwa wapi lazima asakamwe!!!!
sasa hili la kumkaribisha ni geni kwangu, hivi kesha tutasimama jukwaani kukemea ufisadi wakati tunaukaribisha? Mungu inusuru CDM!
 
Ng'wanamapalala, Lowasa ameshindwa kuirubuni ccm kwa usanii wake. Sasa ccm imefurahia kudhibiti mafuriko ya kifisadi kwa vidole, kelele za nini tena?

Ninashauri endeleeni kumnadi yeboyebo wenu mnayeamini ni mtu sahihi kabisa kuwa mwenyekiti wa ccm kulilko wanaccm wote. Habari za Lowasa achaneni nazo kwa sababu hana madhara kwenu tena. Mmeshajikomboa, hizi tararila na taarabu zote juu ya lowasa za nini tena?

Nami naungana na wengine kwamba Lowasa ni mtanzania kama watanzania wengine. Anauhuru wa kutokushiriki ama kushirika siasa na chama chochote akipendancho na hakuna sheria inamzuia. Masuala yake na wenyeji wake kama ni kweli, aachiwe yeye na wenyeji wake wamalizane na si jukumu la ccm tena kufuatilia anakwenda wapi kufanya siasa na nani kwa taratibu gani.

CHaDEMA ni chama kikubwa kuliko vyama vyote vya siasa Tanzania. Kinasera ya mlango wazi kwa kila mtu ili mradi afuate sheria za chama. Sasa lowasa kama akiamau kufuata sheria na taratibu atakazokuwa kawekewe na CHaDEMA kama ataamua kujiunga nacho, kuna tatizo gani? Kazi ya CHaDEMA ni kunoa wanachama wake wapya including Lowasa kama atajiunga kutoka ghafi kuwa safi ndani ya chama. Hilo waachieni wao anajua taratibu na kanuni zao.

Ccm isonge mbele kutatua migogoro yao, iwaache UKaWA nao waendelee na uimarishaji wa umoja wao na vyama vyao.

Siku njema.

Nimechekaje dah....magufuli kumbe yeboyebo
 
Mkuu unabidi uelewe siasa ....

We bado uko mbali na hata mtembeo huujui ni upi.

Tulisema nguvu ya umma.

Huwezi ukaizuia nguvu ya umma.

Wengi washailewa slogan yetu ni mwaka wa nguvu ya umma.

Huu ndio msimu na huu ni ndio mwaka nguvu ya umma imesema Tanzania.

Bado wengine hamujaelewa tu ?
 
Sikiliza dogo, Huku CDM nilidhani fisadi hata akiwa wapi lazima asakamwe!!!!
sasa hili la kumkaribisha ni geni kwangu, hivi kesha tutasimama jukwaani kukemea ufisadi wakati tunaukaribisha? Mungu inusuru CDM!

Na Wewe ni CHADEMA ?!?!?!?!??!
Majanger haya jamani
 
Ng'wanamapalala, Lowasa ameshindwa kuirubuni ccm kwa usanii wake. Sasa ccm imefurahia kudhibiti mafuriko ya kifisadi kwa vidole, kelele za nini tena?

Ninashauri endeleeni kumnadi yeboyebo wenu mnayeamini ni mtu sahihi kabisa kuwa mwenyekiti wa ccm kulilko wanaccm wote. Habari za Lowasa achaneni nazo kwa sababu hana madhara kwenu tena. Mmeshajikomboa, hizi tararila na taarabu zote juu ya lowasa za nini tena?

Nami naungana na wengine kwamba Lowasa ni mtanzania kama watanzania wengine. Anauhuru wa kutokushiriki ama kushirika siasa na chama chochote akipendancho na hakuna sheria inamzuia. Masuala yake na wenyeji wake kama ni kweli, aachiwe yeye na wenyeji wake wamalizane na si jukumu la ccm tena kufuatilia anakwenda wapi kufanya siasa na nani kwa taratibu gani.

CHaDEMA ni chama kikubwa kuliko vyama vyote vya siasa Tanzania. Kinasera ya mlango wazi kwa kila mtu ili mradi afuate sheria za chama. Sasa lowasa kama akiamau kufuata sheria na taratibu atakazokuwa kawekewe na CHaDEMA kama ataamua kujiunga nacho, kuna tatizo gani? Kazi ya CHaDEMA ni kunoa wanachama wake wapya including Lowasa kama atajiunga kutoka ghafi kuwa safi ndani ya chama. Hilo waachieni wao anajua taratibu na kanuni zao.

Ccm isonge mbele kutatua migogoro yao, iwaache UKaWA nao waendelee na uimarishaji wa umoja wao na vyama vyao.

Siku njema.

Nakupa Big Up
 
Yule Mzee Wasira aliyesema Upinzani mpaka kukaribia uchaguzi watakuwa wamesha futika kama ilivyotokea kwa vyama vilivokuwa tishio kwa CCM mbona simsikie na utabiri wake?.
Mkuu,
Kuna kauli zingine huhitaji hata kuzichambua kama una fikra pana.

Hii ni sawa na mtu mwenye akili akakuambia jambo ambalo anafahamu nila kijinga halafu na wewe ukalikubali, atakudharau.

Wale waliodhani kauli ya Wasira ilikuwa na chembe ya ukweli, nadhani aliwadharau sana.
 
Hawajielewi:kubomoa ni rahisi sana kuliko kujenga .Mm nnakubaliana kabsa ya kuwa kila mtu anahaki ya kujiunga na chama chote ,lakin cdm ni chama kichanga bado kinakua na Edo amesababisha makundi ndani ya ccm,Matokeo yake atakigawa chadema kwa kununua baadhi ya wanachama ili kuunda team maana yeye edo anatafuta umaarufu kwa kutumia pesa.Na kidiplomasia mtu wa hivyo ni hatari sawa. Ushauri kwa Mhe.mbowe nnajua uko makini sana na umekipgania hiki chama kwa mda mrefu,umeunganisha makundi mbalimbali iliyajitambue na kupgania haki.ucifanya kazi ya kuvuka bahari zaidi ya miaka 20 ,na umefika ufukweni harafu ukakutana na mamba.Tafakari machonzi ya watanzania wanyonge waliomwanga damu na kupoteza viungo kwa ajili ya kujenga chama isije kuvuta chadema kabsa
Katika siasa za tanzanania
 
Naona mafuriko yamezuiwa na kope za macho....hi hii
SINA IMANI NA UKAWA
 
Ndugu nimekuelewa sana lakini kumbuka asilimia kubwa ya wanachama walitoka CCM na wachache hawakuwa na chama.Sasa unaposema tusiwakubali wanachama wapya kwa hofu ya ufisadi huoni unawanyima watu Uhuru wa kujiunga na chama chochote bila kikwazo ilimradi kukubaliana na katiba ya chama unachojiunga.Ufisadi unaendana na mfumo wa chama au taasisi ilivyojipambanua.Inawezekana ukawa wewe hupendi rushwa na ufisadi lakini ukakuta utaratibu wa chama,shirika na taasisi inaruhusu na wewe lazima ufuate hali inavyotaka.

Muda utaamua mkuu! Namwomba Mungu UKAWA isivunjike maana ndio lililokuwa tumaini langu la pekee kwenye kuunda serikali mwaka huu. Ila naona matumaini yangu yanayoyoma kadri suku ya uchaguzi inavyokaribia
 
Chadema hawampendi Lowassa wanapenda wapambe wake hasa wa Kaskazini. Kaskazini yote imeenda kwa Chadema ukiacha Tanga na wamasai wa Arusha. Chadema wanajua wakipata watu wa Lowassa watakuwa wamechumua Kilimanjaro, Arusha na Manyara yote. Hivyo Lowassa anatumika baada ya uchaguzi watamtupa nje
 
Mhe. Lowasa kuomba uanachama CHADEMA ni haki yake. CHADEMA kumkumbatia Mhe. Lowasa ni sawa na mtu mzima kula kujitukana mwenyewe au kutokuwa na msimamo.
Mkuu,
Lowassa hajaomba uanachama CHADEMA bali anakaribishwa kwa mikono miwili na baadhi ya wabunge wa CHADEMA.
 
Mkuu tumechoka na literature zako kuhusu lowassa sasa kama huna chakuandika bora uuchune
Huyo Ng'wamapalala achana naye anahangaika kweli kweli na asipoangalia karibu atachanganyikiwa...thread moja baada ya nyingine, ni kama vile kaweka kabisa kibanda humu JF. Kuna watu kila wakiifikiria Tanzania bila CCM, usingizi huoooo unaaga. Umezaliwa ndani ya chama cha kifisadi na kukulia kwenye ufisadi halafu wanatokea watu wanaanza kuupiga vita ufisadi, na wewe hujui maisha nje ya ufisadi, mbona utatamani ardhi ipasuke.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Ng'wamapalala achana naye anahangaika kweli kweli na asipoangalia karibu atachanganyikiwa...thread moja baada ya nyingine, ni kama vile kaweka kabisa kibanda humu JF. Kuna watu kila wakiifikiria Tanzania bila CCM, usingizi huoooo unaaga. Umezaliwa ndani ya chama cha kifisadi na kukulia kwenye ufisadi halafu wanatokea watu wanaanza kuupiga vita ufisadi, na wewe hujui maisha nje ya ufisadi, mbona utatamani ardhi ipasuke.
Mkuu,
Sasa wewe unafahamu vipi kama nimeweka kibanda humu kama wewe hukuweka kibanda humu kukifahamu kila mara kile ninachokileta?

Badala ya kupambana na hoja zangu, ingekuwa ni vizuri ukapambana kwanza na wale walisema kama wakiingia madarakani watamfunga Lowassa halafu leo wanamkaribisha ndani ya chama kwa mikono miwili huku wakimhakikishia safari yake ya matumaini itakamilika.

Kama ni habari, walaumu gazeti la Mwananchi ambalo limeandika hii habari.

Suala muhimu siyo kubadili chama au jina la chama, suala muhimu ni kubadili mfumo wa fikra na mitazamo.

Siyo wote walioko CCM ni mafisadi na siyo mafisadi wote ni CCM.
 
Back
Top Bottom