Wabunge wa CHADEMA wagawana dakika 5!

Wabunge wa CHADEMA wagawana dakika 5!

Baada ya CCM kupitisha kanuni ya wabunge kuchangia kutokana na wingi wa wabunge ktk bunge..
Wabunge wa chama cha CHADEMA wamekuwa wakigawana dakika 10 kwa wabunge wawili yani dakika tano tano..

Kwa kuwa CCM wamekuwa wakihofia kuwapa wapinzani muda mwingi hivyo wabunge wa CCM wanapewa muda zaidi.Mfano CCM wakiongea wa 5 mpinzani anaongea mmoja.Hakika CCM wanatupeleka kusiko.

Wala usijali dakika ngapi wanaongea si Ni Kama mbwa koko asiye na meno ubweka sana ila Wenur kung'ata hawabweki ovyo wakibweka ipo Jambo
 
CCM kila mbinu wanayokuja nayo dhidi ya CDM inakuwa na madhara zaidi kwao kuliko kwa walengwa. Dawa pekee ni kutimiza ahadi mlizotuahidi, pambaneni nashida za wananchi siyo na CDM. Vinginevyo mnazidi jichimbia kaburi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nadhani Hii ni katika kujaribu kuleta Usawa katika Ugawaji wa muda katika kuongea----Tunakubaliana kwamba Wabunge wanapoongea,ndio tunaona jinsi wanavyotutetea ama wasivyoweza kutututetea.
Huwa mnaona kwamba michango mingi ya wabunge,hutolewa kwa maandishi,Lakini kwa sababu watanzania tunafuata sana emotions zetu na si uhalisia wa mambo,basi wale wabunge ambao wanatoa michnago yao kwa maandishi sisi hatuwaoni kama wanafanya lolote.Ikumbukwe kwamba wakisema kila mbunge kule bungeni aongee,basi itabidi bunge liwe la miaka miwili mizima kuweza kumaliza kipindi bunge moja la bajeti.
Na kila mbunge,ana haki ya kusema yeye ndiye achaguliwe kuongea LIVE kile anachochangia.
Sasa je,nani aseme na nani asiseme LIVE?
Kumbuka kuonekana LIVE,watanzania wanakuona na kukuthaminisha(hasa wengi wao wanachukulia ndio muda wa kueleweka kwamba wanafaa)

Katika Siasa za Vyama vingi,inakuwa vigumu zaidi kuweza kupanga nani ataongea na nani asiongee.

Kila mmoja atataka aongee

Sasa cha kufanya ni nini hapa?Inatafutwa njia ambayo ni "Objective" ili kuwapa wabunge wengi zaidi muda wa kuongea LIVE
Na kwa sababu hivi ni vyama vingi,basi kila chama lazima wabunge wake wanafanana katika "nini cha kusema",ingawaje si mara zote.
Hivyo,kama ndivyo,basi kwa sababu kuna wabunge 300 kutoka vyama A,B,C na D,na Idadi ya wabunge katika vyama hivyo ni 200,50,40,10,respectively,then wape uwiano wa muda hivyo hivyo,kwa mfano katika saa moja la LIVE bunge talk,watapata katika uwiano wa 40mins(muda kwa ajili ya wabunge hao 200 kutokea chama A wanaotaka kuongea),10mins(muda kwa ajili ya hao wabunge 50kutokea chama C wanaotaka kuongea),7mins( muda kwa ajili ya wabunge hao 40 kutokea chama C wanaotaka kuongea) and 3mins(muda kwa ajili ya wabunge hao 10 kutokea chama D wanaotaka kuongea).....Objectively,utaona kwamba kila mbunge wa bunge amepewa hapo dakika 60/300=0.02
Hapo kumbuka kila Mbunge analalamika kwamba mbona mie sipewi muda?ama Chama kimoja kinasema mbona sie hatupewi muda?-----na suluhisho la kweli linakuwa hilo lililofanyika.

Kwa hiyo,kama nilivyotangulia kusema wabunge kutoka chama kimoja ni lazima kwa kiasi kikubwa wanakuwa wanashabihiana misimamo yao,na hivyo hata cha kuongea wanakuwa wanashabihiana,na kutofautiana ni kidogo,pia kukubaliana ni rahisi---hivyo basi,kila chama inatakiwa wajipange kuweza kuona ni namna gani watatumia muda wao ili kuweza kuwakilisha kile wanachotaka kuongea

Sasa nadhani wabunge wengi zaidi watakuwa wanaongea.
Lakini nadhani bado kila chama kitakuwa kinachagua nani wa kumpandisha chati kwa muda gani,ili apewe muda mrefu zaidi (kutoka kwenye ule muda wao wanaopewa)----Kumbuka wabunge wote mashuhuri wametokana na kuongea sana bungeni(watanzania tunapenda watu wanaoongea jamaniiiiiii...chaaaaaa!mburaaaaa)

Ndio maana hua unaotaga unakabwa usiku.
Yaani hao wabunge wa CCM hata kama hawana cha kuongea wapewe tu muda kisa wako wengi??

We ushamsikiaga Mohammed Dewji wa Singida akiongea??

So huyu nae ajumuishwe katika calculation za kutafuta muda wa CCM wakati haongeagi chochote??
 
Baada ya CCM kupitisha kanuni ya wabunge kuchangia kutokana na wingi wa wabunge ktk bunge..
Wabunge wa chama cha CHADEMA wamekuwa wakigawana dakika 10 kwa wabunge wawili yani dakika tano tano..

Kwa kuwa CCM wamekuwa wakihofia kuwapa wapinzani muda mwingi hivyo wabunge wa CCM wanapewa muda zaidi.Mfano CCM wakiongea wa 5 mpinzani anaongea mmoja.Hakika CCM wanatupeleka kusiko.

Tatizo la CCM hawaangalii mbele zaidi ya pua zao!!! Hivi wanadhani wataendelea kuwa majority bungeni milele? Hivi hawajui sheria ni msumeno unakula MBELE na NYUMA?...
 
Bravo Chadema,

Always kuna njia tofauti ya kufikia lengo! 5dk zitawapa nafasi ya kuzungumzia issues tu!! Nasikitika kutoka CCM ktk 10dk hizo hizo dakika 7 zitakuwa za kutoa shukrani kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM, Makamu wake, Katibu Mkuu, Sekretariat, familia zao.
 
Back
Top Bottom