Wabunge wa CHADEMA kutohudhuria bunge?

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Wengi tunajua yanayoendelea Arusha ambapo viongozi wakuu wa Chadema akiwemo Kiongozi wa Kambi ya upinzani yuko uwanja wa NMC hadi siku Mb wa Arusha mjini Mh. Lema atakapotoka rumande. Je itakuwa busara kwa wabunge waliotangulia Dodoma kesho kuingia bungeni wakati mwenzao anayepigania haki yao yaani unyanyasaji wa polisi kuingia bungeni?
 
Sioni mbaya wakihudhuria lakini pia kinyume chake pia sioni ubaya....
 
Ni vizuri wengine wahudhurie bunge ili kutetea miswada itakowakiliswa bungeni.lazima wajue mapambano haya ni magumu na umoja na mshikamano unahitajika.jinsi nilishuhudia mkutano uliofanyika dodoma leo jioni ,chadema wana wabunge makini wenye ushawishi mkubwa kwa wananchi ccm wanakazi kweli.
 
Kuhudhuria Bungeni siyo vibaya kwa kesho,lakini baada ya kesho wanaweza wakasusia vikao vingine mpaka mbunge mwenzao aachiwe,Tatizo la mahakama zetu zinaingiliwa sana na serikali hazina uhuru,kuna Jaji mstaafu mmoja alisema aliwahi kutoa hukumu kwa shinikizo.
Kama anayeongea hivyo ni Jaji,vipi kwa mahakimu wetu?
 
inabidi wengine wahudhurie ili waweze kudhibiti miswaada mibovu isipitishwe hovyohovyo na wabunge wagonga meza wazee wa naunga mkono kwa 100%-ccm. kumbuka wabunge wa chadema ndio wanaoendesha bunge kwa kutetea masilahi ya taifa tukiwaachia wagonga meza basi ujue tumeisha :embarassed2:
 
Mapambano ni kila upande, walioko Arusha wanatosha na walioko Dom wanatosha, Chadema ina watu makini wenye hoja makini wanaokubalika kila upande, makamanda shambulieni pande zote
 
Ni vizuri wengine wahudhurie bunge ili kutetea miswada itakowakiliswa bungeni.lazima wajue mapambano haya ni magumu na umoja na mshikamano unahitajika.jinsi nilishuhudia mkutano uliofanyika dodoma leo jioni ,chadema wana wabunge makini wenye ushawishi mkubwa kwa wananchi ccm wanakazi kweli.

Hivi kweli alipokataa kutolewa dhamana aliwashirikisha wabunge wenzake.?My take Wabunge wa chadema nendeni bungeni Kama umaarufu kajitakia mwenyewe.Mie naona tr 14 karibu angekaa mpaka 31.
 
Hive kweli alipokataa kutolewa shamans aliwashirikisha wabunge we sake?My take Wabunge wa chadema nendeni bungeni Kaaba umaarufu kajitakia mwenyewe.Mie naona tr 14 karibu angekaa mpaka 31.
Unapima upepo!
 
Back
Top Bottom