Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,049
Kitendo kilichofanyika Bungeni wiki iliyopita na Spika Ndugai akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao ndiyo walio wengi bungeni, kwa kweli kinasikitisha sana.
Kwa wale tuliyoiangalia ile clip ya lile tukio zima la kutolewa Mbunge Mnyika mle Bungeni kama kibaka, tulibaini kuwa tukio like lilitokea kutokana na upendeleo wa wazi uliofanywa na Spika Ndugai kwa wabunge wenzake wa CCM.
Tukio lilianzia wakati Mbunge wa Mtera Lusinde alipokuwa akichangia na kuwaita wabunge wa upinzani kuwa ndiyo watetezi wa wezi wa madini yetu hapa nchini, wakati mbunge Lusinde akiendelea kuchangia, ndipo alipoibuka Mbunge mmoja wa CCM, ambapo inasemekana ni yule mwanadada Show.........nzaaa alipowasha mic yake na kutamka wazi wazi na kusikika na kila mbunge mle bungeni kuwa Mnyika mwizi......
Alichofanya Mbunge Mnyika ni kuomba mwongozo kwa Spika kama zilivyo taratibu za Bunge na kumueleza Spika kuwa yupo Mbunge mmoja amewasha mic yake na kumuita yeye Mnyika kuwa mwizi, kwa hiyo akamuomba Spika kama zilivyo taratibu za Bunge kuwa aidha mbunge huyo afute kauli yake au athibitishe wizi wake yeye Mnyika.
Cha kushangaza kupita kiasi ni kauli iliyotolewa na Spika Ndugai kwa kudai kuwa yeye hana masikio 100 ya kusikia kila linalosemwa humo bungeni, lakini hapo hapo akasema kuwa eti Mnyika apuuze hiko kilichosemwa kwa kuwa hakijaingia kwenye Hansard!
Mbunge Mnyika akaona hatendewi haki na akaendeleza kusisitiza kuwa ni lazima kanuni za Bunge ziheshimiwe na Mbunge yule aidha afute kauli yake au alithibitishie Bunge kuhusu wizi wake.
Kilichotokea baada ya pale kila mtu alijionea ni Spika Ndugai kutumia mamlaka ya kiti chake cha Spika na kuagiza maaskari wamtoe Mbunge Mnyika msobe msobe kama vile kibaka!
Walichofanya Mbunge Halima Mdee na Esther Bulaya ni kuprotest kwa kile kitendo cha kinyama kiiichokuwa kikifanywa na wale maaskari kwa Mbunge mwenzao.
Baada ya hapo ndipo tuliposikia maamuzi mengine ya kustaajabisha ya Spika Ndugai ya kuitisha chapu chapu kikao cha Kamati ya haki na maadili ya Bunge ili kiwajadili wabunge wale ambao tayari 'alishawahukumu' kwa kuwaita ni wabunge watukutu!
Maamuzi ya Kamati ya Haki na maadili ambayo inakuwa composed na wabunge wa CCM watupu, kila mtu alishtushwa nao ni kuwafungia wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa mwaka mzima, ambapo ni ukiukwaji wa wazi kabisa hata wa kanuni zao za Bubge , ambazo zimeellekeza 'maximum penalty' ya kosa lolote Bungeni ni kutohudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vya siku 20.
Jambo lingine linaloleta ukakasi ni kwa vipi Kamati hiyo ya Haki na Maadili ipore haki ya wananchi wa majimbo ya Kawe na Bunda mjini kwa 'kuwakomoa' wananchi hao wakose uwakilishi Bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja?
Kwa mlolongo mzima wa tukio lililotokea Bungeni lililohusu sakata la wabunge Mnyika, Halima Mdee na Esther Bulaya, zipo dalili za wazi zinazoonyesha kuwa ipo ajenda ya siri ya maccm ya kutaka kuligeuza Bunge leru liwe la mfumo wa chama kimoja, ambapo wajibu wake mkubwa wa Bunge hilo kuwa la kulikingia kifua serikali yetu kwa jambo lolote hata kama serikali yetu itakuwa imefanya madudu ya kutisha.
Mwenye macho haambiwi tazama......