Wabunge wa CCM wana mkakati wa kuligeuza Bunge letu kuwa la mfumo wa chama kimoja?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,137
Kitendo kilichofanyika Bungeni wiki iliyopita na Spika Ndugai akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao ndiyo walio wengi bungeni, kwa kweli kinasikitisha sana.

Kwa wale tuliyoiangalia ile clip ya lile tukio zima la kutolewa Mbunge Mnyika mle Bungeni kama kibaka, tulibaini kuwa tukio like lilitokea kutokana na upendeleo wa wazi uliofanywa na Spika Ndugai kwa wabunge wenzake wa CCM.

Tukio lilianzia wakati Mbunge wa Mtera Lusinde alipokuwa akichangia na kuwaita wabunge wa upinzani kuwa ndiyo watetezi wa wezi wa madini yetu hapa nchini, wakati mbunge Lusinde akiendelea kuchangia, ndipo alipoibuka Mbunge mmoja wa CCM, ambapo inasemekana ni yule mwanadada Show.........nzaaa alipowasha mic yake na kutamka wazi wazi na kusikika na kila mbunge mle bungeni kuwa Mnyika mwizi......

Alichofanya Mbunge Mnyika ni kuomba mwongozo kwa Spika kama zilivyo taratibu za Bunge na kumueleza Spika kuwa yupo Mbunge mmoja amewasha mic yake na kumuita yeye Mnyika kuwa mwizi, kwa hiyo akamuomba Spika kama zilivyo taratibu za Bunge kuwa aidha mbunge huyo afute kauli yake au athibitishe wizi wake yeye Mnyika.

Cha kushangaza kupita kiasi ni kauli iliyotolewa na Spika Ndugai kwa kudai kuwa yeye hana masikio 100 ya kusikia kila linalosemwa humo bungeni, lakini hapo hapo akasema kuwa eti Mnyika apuuze hiko kilichosemwa kwa kuwa hakijaingia kwenye Hansard!

Mbunge Mnyika akaona hatendewi haki na akaendeleza kusisitiza kuwa ni lazima kanuni za Bunge ziheshimiwe na Mbunge yule aidha afute kauli yake au alithibitishie Bunge kuhusu wizi wake.

Kilichotokea baada ya pale kila mtu alijionea ni Spika Ndugai kutumia mamlaka ya kiti chake cha Spika na kuagiza maaskari wamtoe Mbunge Mnyika msobe msobe kama vile kibaka!

Walichofanya Mbunge Halima Mdee na Esther Bulaya ni kuprotest kwa kile kitendo cha kinyama kiiichokuwa kikifanywa na wale maaskari kwa Mbunge mwenzao.

Baada ya hapo ndipo tuliposikia maamuzi mengine ya kustaajabisha ya Spika Ndugai ya kuitisha chapu chapu kikao cha Kamati ya haki na maadili ya Bunge ili kiwajadili wabunge wale ambao tayari 'alishawahukumu' kwa kuwaita ni wabunge watukutu!

Maamuzi ya Kamati ya Haki na maadili ambayo inakuwa composed na wabunge wa CCM watupu, kila mtu alishtushwa nao ni kuwafungia wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa mwaka mzima, ambapo ni ukiukwaji wa wazi kabisa hata wa kanuni zao za Bubge , ambazo zimeellekeza 'maximum penalty' ya kosa lolote Bungeni ni kutohudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vya siku 20.

Jambo lingine linaloleta ukakasi ni kwa vipi Kamati hiyo ya Haki na Maadili ipore haki ya wananchi wa majimbo ya Kawe na Bunda mjini kwa 'kuwakomoa' wananchi hao wakose uwakilishi Bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja?

Kwa mlolongo mzima wa tukio lililotokea Bungeni lililohusu sakata la wabunge Mnyika, Halima Mdee na Esther Bulaya, zipo dalili za wazi zinazoonyesha kuwa ipo ajenda ya siri ya maccm ya kutaka kuligeuza Bunge leru liwe la mfumo wa chama kimoja, ambapo wajibu wake mkubwa wa Bunge hilo kuwa la kulikingia kifua serikali yetu kwa jambo lolote hata kama serikali yetu itakuwa imefanya madudu ya kutisha.

Mwenye macho haambiwi tazama......
 
Ndugai ana uwezo mdogo sana kiakili na kiuongozi. Uhitaji kutumia nguvu sana kulielewa hili. Mtu wa namna hii kupewa Bunge kuliongoza ni makosa makubwa. Itatugharimu. Yote ya kuzomewa na kutukanwa kwake yanatokea kwa sababu wabunge wanaojitambua wamemuona ni zuzu. Zuzu linaudhi. Hata ukilivumilia zuzu halijiongezi. Hili jamaa la Kongwa ni hasara.
 
Inashangaza pia kwa Spika Ndugai kudai kuwa mbunge mwenzake aliyewasha mic na kumwita Mnyika mwizi hakumsikia!

Lakini siku za nyuma humo humo Bungeni alipotokea Mbunge wa upinzani kuwasha mic na kumuita yeye fa.....laaaa akasikia vizuri sana na kumtreat Halima Mdee kama amefanya kosa kubwa la jinai la kuua mtu!
 
Tuombe TLisu apeleke ili zengwe la Spika na wapambe wake kwenye mahakama lipatiwe ufafanuzi.
Spika kama hakusikia na clip inasikika wazi Nyika katukanwa mahakama itoe haki.
Maamuzi batili yafutwe!@
 
Muda mwingine tuwe wakweli na kuweka vyama pembeni hivi kwanini kila siku bulaya mdee au yale matusi tunayosikia huwa wana edit
Acheni kujitoa akili wale wawakilishi wenu hawana adabu na hata maandiko yametataa itawa cost bungeni na kwa mungu pia atawaadhibu. Nukta
 
Bwana yule 'alimtuma' India kwenda kutibiwa ugonjwa wake wa kuwa na hasira za kupitiliza na kutokuwa na subira....

Mfano halisi wa hasira zake ni namna alivyoweza kumchapa bakora mgombea mwenzie wa CCM kwenye kura za maoni kule Kongwa mwaka 2015!
Tafadhari wekeni hiyo clip na picha kuonyesha unyama wa Ndugai!!
 
Pia kuna dalili za walakinikwa opposition. 1/3 ya wabunge ni opposition, wakiungana wenyewe tu inakuwa na nguvu kuhwa. Kina malena south wapo saba tu, mziki wao sio wa mchezo.
 
Ni kweli unachosema lakini na sisi watz ikifika 2020 tukapewa kofia na t-shirt chagua padlocks kiherehere. Hawa walishagundua ile bajeti haipiti wakaona solution ñi kuwatimua hao lead team basi. Tuamke
 
Kitendo kilichofanyika Bungeni wiki iliyopita na Spika Ndugai akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM ambao ndiyo walio wengi bungeni, kwa kweli kinasikitisha sana.

Kwa wale tuliyoiangalia ile clip ya lile tukio zima la kutolewa Mbunge Mnyika mle Bungeni kama kibaka, tulibaini kuwa tukio like lilitokea kutokana na upendeleo wa wazi uliofanywa na Spika Ndugai kwa wabunge wenzake wa CCM.

Tukio lilianzia wakati Mbunge wa Mtera Lusinde alipokuwa akichangia na kuwaita wabunge wa upinzani kuwa ndiyo watetezi wa wezi wa madini yetu hapa nchini, wakati mbunge Lusinde akiendelea kuchangia, ndipo alipoibuka Mbunge mmoja wa CCM, ambapo inasemekana ni yule mwanadada Show.........nzaaa alipowasha mic yake na kutamka wazi wazi na kusikika na kila mbunge mle bungeni kuwa Mnyika mwizi......

Alichofanya Mbunge Mnyika ni kuomba mwongozo kwa Spika kama zilivyo taratibu za Bunge na kumueleza Spika kuwa yupo Mbunge mmoja amewasha mic yake na kumuita yeye Mnyika kuwa mwizi, kwa hiyo akamuomba Spika kama zilivyo taratibu za Bunge kuwa aidha mbunge huyo afute kauli yake au athibitishe wizi wake yeye Mnyika.

Cha kushangaza kupita kiasi ni kauli iliyotolewa na Spika Ndugai kwa kudai kuwa yeye hana masikio 100 ya kusikia kila linalosemwa humo bungeni, lakini hapo hapo akasema kuwa eti Mnyika apuuze hiko kilichosemwa kwa kuwa hakijaingia kwenye Hansard!

Mbunge Mnyika akaona hatendewi haki na akaendeleza kusisitiza kuwa ni lazima kanuni za Bunge ziheshimiwe na Mbunge yule aidha afute kauli yake au alithibitishie Bunge kuhusu wizi wake.

Kilichotokea baada ya pale kila mtu alijionea ni Spika Ndugai kutumia mamlaka ya kiti chake cha Spika na kuagiza maaskari wamtoe Mbunge Mnyika msobe msobe kama vile kibaka!

Walichofanya Mbunge Halima Mdee na Esther Bulaya ni kuprotest kwa kile kitendo cha kinyama kiiichokuwa kikifanywa na wale maaskari kwa Mbunge mwenzao.

Baada ya hapo ndipo tuliposikia maamuzi mengine ya kustaajabisha ya Spika Ndugai ya kuitisha chapu chapu kikao cha Kamati ya haki na maadili ya Bunge ili kiwajadili wabunge wale ambao tayari 'alishawahukumu' kwa kuwaita ni wabunge watukutu!

Maamuzi ya Kamati ya Haki na maadili ambayo inakuwa composed na wabunge wa CCM watupu, kila mtu alishtushwa nao ni kuwafungia wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa mwaka mzima, ambapo ni ukiukwaji wa wazi kabisa hata wa kanuni zao za Bubge , ambazo zimeellekeza 'maximum penalty' ya kosa lolote Bungeni ni kutohudhuria vikao vya Bunge visivyozidi vya siku 20.

Jambo lingine linaloleta ukakasi ni kwa vipi Kamati hiyo ya Haki na Maadili ipore haki ya wananchi wa majimbo ya Kawe na Bunda mjini kwa 'kuwakomoa' wananchi hao wakose uwakilishi Bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja?

Kwa mlolongo mzima wa tukio lililotokea Bungeni lililohusu sakata la wabunge Mnyika, Halima Mdee na Esther Bulaya, zipo dalili za wazi zinazoonyesha kuwa ipo ajenda ya siri ya maccm ya kutaka kuligeuza Bunge leru liwe la mfumo wa chama kimoja, ambapo wajibu wake mkubwa wa Bunge hilo kuwa la kulikingia kifua serikali yetu kwa jambo lolote hata kama serikali yetu itakuwa imefanya madudu ya kutisha.

Mwenye macho haambiwi tazama......
Wala haina haja ya kumlaumu spika kwa hayo. kiti cha spika kilidhalauriwa na makosa yalifanywa na wbunge husika. kamati iliitishawa kwa mujibu wa kanuni za bunge na adhabu ilitolewa kwa mujibu wa kanuni. hivyo vikao 20 ulivyoandika ni adhabu iliyopendekezwa na kanuni za bungwe. lakini pia kamati imepewa mamlaka ya kutaoa adhabu kadri inavyoona inafaa.
Tusipende kulaumu tu wankti makosa yanafanywa na watu wenye akili zao na wanazijua vizuri taratiu na kanuni. Hao wananchi wala hawajaporwa haki yao ya uwakilishi bungeni. wananchi hawawakilishiw kwa matusi na migomo na kaidi zisizo na msingi. wananchi wanawakilishwa kwa hoja.
Tangu lini wapinzani wamekikubali kiti cha spika na kukipa heshima yake? Wapinzani ancheni kutetea maovu yasiyoenga taifa. teteeni ukweli na haki ili kujenga demokrasia yetu. Bunge sio pori la wapiga porojo.
 
Muda mwingine tuwe wakweli na kuweka vyama pembeni hivi kwanini kila siku bulaya mdee au yale matusi tunayosikia huwa wana edit
Acheni kujitoa akili wale wawakilishi wenu hawana adabu na hata maandiko yametataa itawa cost bungeni na kwa mungu pia atawaadhibu. Nukta
Hebu pia kuwa mkweli mnyika kuitwa mwizi na spika kudai kutokuskia ni sawa?wakati yale maneno ya now anadai ameyaskia?ndani hukuskia ila now aliskia na kutoa onyo hiyo inakuwaje hapo katenda haki au la lkn maneno ya huyo mbunge anayeitwa lusinde utayaona yako sahihi?usihukumu upande mmoja hebu geuza na upande wa pili mkuu.
 
Maneno ya ndani ya kuitwa mnyika mwizi hakuyasikia ila ya now yeye kusemwa vibaya ameyaskia hapo inakuwaje mkuu ni haki au.
 
Muda mwingine tuwe wakweli na kuweka vyama pembeni hivi kwanini kila siku bulaya mdee au yale matusi tunayosikia huwa wana edit
Acheni kujitoa akili wale wawakilishi wenu hawana adabu na hata maandiko yametataa itawa cost bungeni na kwa mungu pia atawaadhibu. Nukta
Nawe kuwa mkweli, hivi kati ya wabunge Halima Mdee na Esther Bulaya, ukiwalinganisha na wabunge wenu wa CCM akina Lusinde, Mlinga na yule Msukuma ni wapi hasa watukutu na ambao ni mabingwa wa kuporomosha matusi?

Jibu hapo lipo obvious kama utaweka itikadi za kisiasa pembeni, kuwa siku zote ukiona Bunge limechafuka, basi utagundua waliochafua hali ya hewa ni akina Lusinde, huku Spika Ndugai akiwashangilia na kuwasifu na kuwaita eti hao ndiyo kiboko cha wapinzani!

Kwa mazingira ya Bunge letu linakoelekea na upendeleo wa wazi unaofanywa na kiti cha Spika sitashangaa kwa siku zijazo kuja kusikia kuwa wabunge wa CCM wamezichapa ngumi kavu kavu na wabunge wenzao wa Chadema!
 
Maneno ya ndani ya kuitwa mnyika mwizi hakuyasikia ila ya now yeye kusemwa vibaya ameyaskia hapo inakuwaje mkuu ni haki au.
Mbona yeye Spika Ndugai alipowashiwa mic na Mbunge mmoja wa upinzani na kuitwa yeye fa.....laaa, matamshi Yale aliyasikia vizuri sana?

Lakini majuzi wakati mbunge mwenzake Show.... nzaaaa alipowasha mic na kumuita Mnyika mwizi, anajifanya yeye hana masiko 100 kuweza kusikia kila kitu kinachotamkwa humo Bungeni!?
 
Ndo ushangae ss
 
Back
Top Bottom