WABUNGE wa (CCM), wamemchagua Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza kuwa Katibu wao

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,502
3,483
jasson-Rweikiza_zps850e2829.png

Rweikiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, ambaye safari hii hakuwania nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Msekwa uliopo ndani ya viwanja vya Bunge, Katibu huyo mpya wa Wabunge wa CCM alikuwa akipambana na Mary Chatanda, Mariam Kisangi na Abdalah Ulega.

Wabunge wote wa CCM pia walipiga kura kuwachagua wabunge 10 kati ya 21 walioomba ujumbe wa NEC.

Waliochaguliwa ni Livingstone Lusinde, Dk Hamis Kigwangalla, Stanslaus Nyongo, Steven Ngonyani, Peter Serukamba, Faida Bakari, Agness Marwa, Munde Tambwe, Angella Kairuki na Jamal Kassim Ali.

Wabunge ambao kura hazikutosha ni Mbaraka Dau, Alex Gashaza, Hawa Ghasia, Ibrahim Raza, Profesa Norman Sigalla ‘King’, Almas Maige, Angelina Malembeka, Yahya Massare, Mattar Ali Salum na Hafidh Ali Tahir.
 
Naona "jamaa wa Magufuli" kapita baada ya "Jamaa wa JK" kugonga mwamba.

Bila shaka busara za wazee wa chama zimezaa matunda.

Ninachojiuliza JK naye si miongoni mwa "wazee wa chama" ??

Mbona maamuzi yake mengi wazee wa chama wengi wanayapinga??
 
Heeee na hawa ghasia aligombea?, huyu mama bado tu hajaanza kusoma alama za nyakati?
 
Hawa una chako Sasa hvi kuwa Mpole naona kimoyo moto unatamani Wabunge wasiwe Mawaziri Harafu Mara nyingi huwa Mtu uliyekuwa waziri then ukapigwa chini ata Bungeni unakuwa kama Msindikizaji Fulani hvi
 
Kidumu chama cha Mapinduzi! Hongera Kassim Majaliwa kupata katibu wewe ukiwa mwenyekit. Sasa mrudishe ule utaratibu wa zamani wakati wa Mkapa wabunge wa ccm mnakutana (cocus ) kabla ya vikao kuwa na msimamo mmoja kabla hamjaenda bungeni badala ya mtindo wa jakaya kutaka mkaumbue serikali hadharani bungeni matokeo yake mkazalisha makundi na kudhalilisha mawaziri hadharani
 
msomi wa karne ya 21, duh!!
 
msomi wa karne ya 21, duh!!

Siasa ni zaid ya usomi ndio sababu kuna Katibu wa Wizara ni Prof. Lakini anaripoti na kupangiwa kazi na Waziri mwenye Diploma tu! Kuna Mwenyekit wa chama ni form six failure lakin anaajiri na kuwapangia kazi makatibu wakuu wenye Phd na kuwafukuza akitaka.
 
Lusinde 'kibajaj' na Ngonyani 'prof maji marefu' ni mfano mzuri great thinkers wa Chama chetu wakitegemewa kutoa mchango katika kujenga falsafa mpya na mwelekeo wa chama
Magwiji hao wamemkosa Deo Sanga 'jah people' tuu kukamilisha safu kali ya wataalamu
 
Siasa ni zaid ya usomi ndio sababu kuna Katibu wa Wizara ni Prof. Lakini anaripoti na kupangiwa kazi na Waziri mwenye Diploma tu! Kuna Mwenyekit wa chama ni form six failure lakin anaajiri na kuwapangia kazi makatibu wakuu wenye Phd na kuwafukuza akitaka.
Tafakari upya huenda ukaelewa!
 
View attachment 345413
Rweikiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, ambaye safari hii hakuwania nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi usiku katika ukumbi wa Msekwa uliopo ndani ya viwanja vya Bunge, Katibu huyo mpya wa Wabunge wa CCM alikuwa akipambana na Mary Chatanda, Mariam Kisangi na Abdalah Ulega.

Wabunge wote wa CCM pia walipiga kura kuwachagua wabunge 10 kati ya 21 walioomba ujumbe wa NEC.

Waliochaguliwa ni Livingstone Lusinde, Dk Hamis Kigwangalla, Stanslaus Nyongo, Steven Ngonyani, Peter Serukamba, Faida Bakari, Agness Marwa, Munde Tambwe, Angella Kairuki na Jamal Kassim Ali.

Wabunge ambao kura hazikutosha ni Mbaraka Dau, Alex Gashaza, Hawa Ghasia, Ibrahim Raza, Profesa Norman Sigalla ‘King’, Almas Maige, Angelina Malembeka, Yahya Massare, Mattar Ali Salum na Hafidh Ali Tahir.
Wamekosea wangempa mzee wa vijisenti.
 
Hii ndio sisiem bana...
maprofesa wanakosa mbele ta STD seven L. Lusinde na S. Ngonyani a.k.a maji marefu.
 
Hiviii..
Angella Kairuki..
Ubabie bado unaendelea hadi kwenye Ujumbe NEC
 
Back
Top Bottom