Wabunge wa Canada wampongeza Rais Magufuli. Wasema ni miongoni mwa Marais wachache duniani

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
WABUNGE wa Bunge la Canada wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jinsi anavyofanya kazi zake za kuwapambania Watanzania wa chini ili wawe juu kwa kuwapatia maendeleo yaliyo na tija.

Wamesema Rais Magufuli ni miongoni mwa marais wachache duniani, wenye kuthamini wananchi wake kwa kuwapambania kupata mahitaji muhimu, ambayo nchi inastahili kupata kwa kubana mianya ya wakwepaji wa kulipa kodi, ambayo ndio ingechangia kwa upatikanaji wa maendeleo kwa kuwa Pato la Taifa limeongezeka kidogo.

Maneno hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Jumuiya ya Madola kutoka Canada, Yasmin Rentasi katika kikao cha kamati hizo mbili za Canada na Tanzania kwenye Ukumbi Mdogo wa Bunge jijini Dar es Salaam, huku Kamati ya Bunge la Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Dk Raphael Chegeni.

Rentasi alisema Serikali ya Canada ipo tayari kutoa misaada mbalimbali ya kibunge ili kuhakikisha Bunge la Tanzania, linakuwa ni Bunge bora katika usimamizi mzuri wa kisheria na kuishauri serikali juu ya masuala ya msingi yenye kuleta tija katika nchi hiyo.

“Tunaipongeza serikali ya Rais Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania kwa kubana matumizi, kupambana na mafisadi, kudhibiti rushwa hivyo hali hii inaonesha jinsi Tanzania itakavyofanikiwa kukuza uchumi wake kutoka chini na kuongezeka, pia kutapelekea kupungua kwa kiwango cha umaskini pamoja na kuboresha huduma za kijamii kwa muda mfupi,” alieleza Rentasi na kuongeza:

“Mimi nilizaliwa hapa Tanzania (Dar es Salaam) wakati huo baba yangu alikuwa akifanya kazi hapa enzi za Mwalimu Nyerere, niliondoka hapa nikiwa mdogo sana, lakini nafarijika leo kurudi hapa na kuona Tanzania inasonga mbele.”

Aidha, aliwataka Watanzania kumwombea Rais Magufuli ili apambane na mchwa ambao wana lengo la kutaka kumkwamisha katika kutekeleza ahadi yake aliyoipanga kuwafanyia Watanzania.

Kwa upande wake, Dk Chegeni aliwapongeza wabunge hao wa Canada, kwa kuona juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli kupambana na kuinua uchumi. Alisema Tanzania ni nchi yenye utulivu na siasa safi hivyo aliwaomba wabunge hao kuwekeza zaidi ili wananchi wa Tanzania wanufaike kupitia serikali yao ya Canada.

Alisema Tanzania na Canada zitaendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ya maendeleo kwa ajili ya kuwahakikishia wananchi wake upatikanaji wa huduma bora za kijamii.

Chanzo: Habarileo
 
Mbona hilo liko wazi utawala mpaka wa mungu unajua kuwa magufuli anafanya kazi nzuri ni wachache fulani tu wanampinga kwa kutumia migongo ya wanasheria na wanasiasa..jambo la kufurahisha magufuli anajua yote na yuko makini sana ..pambano la ubaya na wema litaisha kwa magu kushinda
 
.......... inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa jinsi anavyofanya kazi zake...
Sawa ila Next time unapoamua kumsifia huyu mtu, usiipotezee PHD yake, usije ukaonekana kama unamdhihaki bana..... mimi namuogopa sana huyu mtu, kuna mtu alihoji PHD yake ikatokea kama coincidence akapotea na hajulikani alipo mpaka sasa, ngoja niendelee kusubiri uchunguzi wa polisi kuhusiana na kulipuliwa kwa ofisi za mawakili
 
Huko sio inakoshikiliwa ndege yetu?
Ndiyo uuone unafiki wa mzungu! Hao ndiyo waliosema kuwa huko tuendako hali ya tanzania kiuchumi itakuwa mbaya! Leo wametusifia rais wetu hivyo hatuna namna ila ni kuwasifia tu! Hawajasema kuwa magu ni nabii aliyetumwa na mungu?
 
Ulitegemea Wageni wanaomtembelea huyo bwana pale Magogoni waache kumpongeza??

Hata Bokassa alikuwa akitembelewa na Wazungu walikuwa wanampongeza..

Na tuna uhakika gani kama kweli kapongezwa??
Kwanza kutembelewa tu ni ishara ya kumpongeza. Nasema hivyo maana tulisikia mmoja wa raia wetu aki amuru mataifa yatutenge! Yatuzomee. Lakini kama yanayotokea ni kinyume chake basi tunapongezwa.
 
Back
Top Bottom