Baba Askofu Mwamakula!
Wabunge waliitishwa kikao kupewa maelekezo ya kuwa wakati wa kuchangia Hotuba ya Rais, wasigusie kabisa mambo ya mauaji ya halaiki ya Watanzania wasio na hatia ya tarehe 29 - 31 Oktoba 2025.
Waliambiwa kuwa wachangie kwenye mambo ya kimaendeleo. Waseme mambo aliyoyafanya Samia na ahadi zake zilizotekelezwa! Wamsifie kwani wameambiwa kuwa hali bado haijatulia, hivyo kama watachangia kwa kuhoji mambo ya mauaji hiyo itaibua mjadala mkubwa sana!
Inasemekana kuwa Rais Samia mwenyewe na watu wake wa karibu walioyaratibu mauaji yale bado wanagopa sana kelele za Watanzania. Ni imani yangu kuwa kwa kupitia ukurasa wako watu wataelewa kinachoendelea Bungeni. Hili jambo linawasumbua sana baadhi ya Wabunge lakini wamefungwa mikono.
Hakuna ye yote ya mtu kutoa maoni huru au ya siri.
Kwa mfano, mfumo wao wa kura za ndiyo na hapana uliendelea kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Kwa mtindo huo, wajumbe wote wanalazimika kusema ndiyo ili wasionekane ni waasi. Kwenda kinyume au kutoa mawazo na maoni mbadala ni hatari kubwa sana.
Hata wakati wa kumpata Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wa Kamati za Bunge, mchakato pia ulitawaliwa na maelekezo na takrima kubwa!
Iko hivi kwenye upatikanaji wa Spika walimteua Zungu na Naibu wake, kisha 'wakamshawishi' kila Mbunge ili kuwabariki. Baada ya kumaliza walihamia kwenye kuteua Wenyeviti wa Kamati za Bunge. Wabunge wanalia wanadai wananchi wajue ya kuwa hakuna Bunge tena, kwa kuwa limetekwa, wao wameporwa haki ya kuchagua viongozi wao wa Kamati kama vile wananchi walivyonyang'anywa haki yao ya kuchagua!
Kwa mfano, Mh. Jaffari Chege wa Rorya alitaka kugombea Uenyekiti wa Kamati, ila aliambiwa yeye atakuwa Makamu Mwenyekiti! Na hakuna watu waliojaza fomu wala kuomba kura.
Mhe. Devotha Minja amepewa Uenyekiti wa Kamati ya PAC bila kuwepo kwani yeye alikuwa India kwa matibabu tangu baada ya uchaguzi! Hii ya vitisho kutolewa kwa Wabunge ya kuwa Mbunge ye yote atakaechangia Hotuba ya Rais kinyume na matakwa yao, basi Mbunge huyo ajiandae kushughulikiwa! Hawataki kabisa hiyo tarehe 29 Oktoba ijadiliwe Bungeni ijapokuwa kuna kundi kubwa la Wabunge linatamani hoja hiyo ijadiliwe. Wabunge wanataka wananchi pia wajue kuwa hata hiyo katiba mpya kupatikana itakuwa ngumu.
J. L. S.,
Dodoma, 27 Januari 2026.