Wabunge ni mazo yetu-utumbo wao ndio tulichozalisha

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Wabunge wanatokana na matakwa, kura, chaguo na mapendekezo yetu. Kila Mtanzania mwenye umri wa mika 18 kwenda juu mwaka 2010 alikuwa na uwezo ama kugombea, kupiga kura, kushawishi na kupendekeza mbunge au Raisi, diwani na mwenyekiti wa mtaa/kijiji nk.

Kinachotokea dodoma leo tusihuzunike kwani ndio uwezo wetu wa kuchagua, kuwakilisha na kutuma wajumbe wetu. Ukiona Mbunge mjinga, mpuuzi, mwongo, mwizi, fisadi mzushi, mpayukaji, lugha chafu, elimu na uelewa duni usistaajabu ila jua hilo ni chaguo lako.

Wapo baadhi ya wapiga kura watasema wao haiwahusu kwani wabunge wao wana weledi na sifa za kuwa bungeni hongereni ninyi mliochagua sura na mifano yenu. Ila wale wanaolia na utendaji wa wabunge wao wajue kila afanyacho mbunge na kusema kinadhihirisha wazi ummakini au ujinga wa wapiga kura wake. Kama mbunge ni mwongo, mzushi, mipasho nk jua hata jimbo lake liko kimipasho na watu wake wanaona ndio kipimo chao.

Wananchi tuache kulalamika tuwe sababu za suluhisho. Mwaka 2015 unakuja kila jimbo, kata ijipange iamue je imedhirika na uwakilishi wa mtu wao bungeni? Je inaona uwakilishi wa diwani wao unafaa? Je huduma za kijamii, afya, elimu, maji, barabara uwekezaji wa kata, jimbo na wilaya unatetewa kwa nguvu zote na wawakilishi? Je wananchi husika wanapenda mijadala ya mipasho, uzushi, siasa na makelele ya matusi yasiyo na tija. Fanyeni tathimini ya mwakilishi wenu CHUKUENI HATUA. Dodoma kumekuwa kichaka cha wehu, majuha, na wachumia matumbo lets stop it.

Chief Mkwawa
2015 lazima kuwe na mabadiliko ya kweli jimboni kwangu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom