Wabunge na madiwani wa upinzani tunzeni vizuri viinua mgongo vyenu,2020 hamtaweza kutoboa mkatafute kazi nyingine

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Imeandikwa na,
Augustino Chiwinga
Nyota njema huonekana asubuhi ndivyo walivyosema makuhani na wahenga wa kale, wakiwa na maana ya kwamba dalili ya jambo lolote jema huonekana mapema sana.

Ndivyo hivyo hivyo unavyoweza kusema kwamba dalili za Chama Cha Mapinduzi {CCM} kuibuka na ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 90 katika uchaguzi wa mwaka 2020 zimeanza kuonekana mapema.

Tangu Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ilipochaguliwa na kuingia madarakani kwa awamu ya tano kumefanyika jumla ya Chaguzi ndogo kadhaa ambapo CCM imeweza kushinda kwa ngurumo za radi kwa kuchaguliwa katika Kata 142 kati ya Kata 144.

Ukiacha ushindi wa Kata 77 katika uchaguzi wa juzi wa Tarehe 12/8/2018, CCM pia iliweza kuchaguliwa katika Kata 19 kati ya 20 zilizoshiriki uchaguzi mdogo wa kwanza wa madiwani uliofanyika Januari 22 mwaka 2017.
Aidha katika uchaguzi mdogo wa pili wa madiwani uliohusisha Kata 43 CCM iliweza kuchaguliwa katika Kata 42 na upinzani ukiokoteza Kata moja tu.

Funga kazi ilikua ni uchaguzi wa majimbo ya Longido,Singida,Kinondoni na Siha na Buyungu huko kote CCM ilifagia upinzani kwa kuibuka na ushindi mnono.

Sasa kwa nini nasema CCM itaibuka na ushindi wa kishindo wa asilimia 90 katika uchaguzi wa mwaka 2020 jibu ni hili hapa.
Katika Uchaguzi mkuu uliopita uliohusisha majimbo 262 CCM iliweza kushinda viti 189 vya ubunge.
Lakini viti hivyo vimeongezeka na kufikia viti 192 baada ya kufanikiwa kuyakomboa majimbo ya Siha, Kinondoni na Buyungu yaliyokua chini ya upinzani.

CCM imefanikiwa kuyakomboa mjimbo hayo baada ya waliokua wabunge wake kujiuzulu nafasi zao na kuvihama vyao vyao (Chadema&Cuf) na kujiunga na CCM ambao pia waliweza kutetea nafasi zao ukiachilia mbali Jimbo la Buyungu ambapo mbunge wake alifariki Dunia.

Na sasa hivi pia waliokua wabunge wa Chadema katika majimbo ya Ukonga,na Monduli nao wamekihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM.
Uchaguzi wa majimbo hayo unatarajiwa kufanyika tarehe 16 September ambapo CCM ina asilimia kubwa ya kuyakomboa majimbo hayo hivyo CCM itafikisha jumla ya viti 195 kamili.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 CCM ina uhakika wa kuvitetea viti hivyo vyote 194 na pia kuyakomboa majimbo 31 yanayoshikiliwa na Chadema , majimbo 37 yanayoshikiliwa hivi sasa na. Cuf ,Jimbo moja linashokiliwa na ACT- Wazalendo pamoja na jimbo moja linaloshikiliwa na NCCR-Mageuzi.
Uhakika ya CCM inatokana na umadhubuti wa chama chenyewe ikiwa ni pamoja na kuendelea kukubalika na watu wa kila rika mijini na vijijini huku Serikaki yake ikitekeleza ahadi zake kwa kasi kubwa.
Hali kadhalika upande wa madiwani CCM ina uhakika wa kutetea viti vyake pamoja kukomboa Kata zote zinazoshikiliwa na upinzani.
Wananchi wengi wa majimbo 192 yanayoshikiliwa na CCM hivi sasa watakipigia kura Chama Cha Mapinduzi katika ngazi zote za Udiwani,Ubunge na Urais

Hivyo basi Wabunge na madiwani wanaotokana na upinzani hivi sasa ni rai yangu kwamba watunze vizuri viinua mgongo vyao watakavyovipata watakapomaliza muhula wao wa uongozi mwaka 2020 kwa sababu hawataweza kushinda tena hata wakifanyaje.
Wananchi wamewachoka wapinzani na porojo zao.
Wajiandae kutafuta kazi nyingine kama za kilimo na ufugaji wa kuku lakini kushinda ubunge na udiwani wasahau kabisa.

Makali ya CCM yameongezeka ,na inazidi kushika hatamu kila uchwao na kikubwa zaidi wananchi waliochagua wapinzani wameshajua walifanya makosa na ndio maana hata kwenye chaguzi hizi ndogo wanafuta makosa yao kwa kukipa Chama Cha Mapinduzi kura nyingi sana.

CCM imeongeza hazina ya wanachama maradufu, wengi wa wanachama hao imewavuna kutoka upinzani na kutoka kwa waliokua hawana vyama tangu mwaka 2016 baada ya kuvutiwa na sera ,falsafa na muelekeo wa CCM mpya.
Ongezeko hilo litaihakikishia CCM kura million 10 za wanaCCM pekee kwa nafasi ya Urais kabla ya kupata kutoka katika makundi mengine.

Wasalaam,
Augustino Chiwinga
0659438889.
 
Mleta mada uko sahihi watumie pesa vizuri hawarudi kabisa kama wana mikopo walikopa taaisisi mbalimbali wajitahidi kulipa hata kuongeza makato ya kila mwezi ili Mali zao zisije pigwa mnada mwisho.Hili Jambo uliloshauri wachukue serious.Wasije kufa kwa pressure Na kupooza
 
watu wenye fikra kama zko n wakuchinja kama kuku hawana faida yoyote kwenye jamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom