Wabunge msiburuzwe na maneno ya Rais Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge msiburuzwe na maneno ya Rais Kikwete!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 11, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu cha kuangalia sana kama mwitikio wa watawala wakati wa dharura. Kwani ni wakati huo ambapo watawala wanahisi kuwa wanaweza kupitisha jambo lolote lile kwa kisingizio cha "dharura". Katika nchi ya kidemokrasia ambayo msingi wake ni sheria, uhuru, uwazi, usawa na kuwajibika (miongoni mwake) ni jukumu la wananchi kuangalia sana kile watawala wanafanya katika wakati wa kawaida lakini zaidi wakati inapotokea dharura.

  Alichofanya Rais Kikwete jana ni kitu ambacho endapo kitakumbatiwa kwa haraka na kumezwa bila hata ya kuangaliwa kwa ukaribu tunaweza kujikuta tumeruhusu kitu cha hatari zaidi katika uchumi wetu.

  Kwanza, uamuzi wa yeye kutoa pendekezo la matumizi haya makubwa ambayo yana implication nzito sana kwa uchumi wa taifa nje ya Bunge ni uamuzi ambao unanifanya nijiulize kwanini hakutaka kuzungumza na wawakilishi wa wananchi Bungeni.

  Huu mtindo wa kuzungumza na "wazee" itabidi siku moja tuukomeshe kwani kama mambo mazito kama haya yanazungumzwa kwa watu ambao moja hawawezi kupewa nafasi ya kujadili kilichosemwa na pili kuzungumza tu kama vile kuwalisha watu chakula bila kuwapa muda wa kunywa maji ni mtindo mbaya.

  Kama tukikubali kuwa hali ni mbaya kama Rais alivyoichora kwenye mawazo ya baadhi ya watu kwa karibu theluthi mbili ya hotuba yake basi alichagua mahali pasipo sahihi kufafanua ubaya wa hali hiyo.

  Lipo kundi moja tu ambalo kitaifa linawawakilisha Watanzania na pekee limepewa jukumu la kusimamia serikali na kundi hilo haliitwi "wazee wa mkoa fulani". Kundi hilo siyo wakufunzi wa Chuo Kikuu na kundi hilo siyo mashabiki fulani bali ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa kuamua kupeleka mapendekezo yake nje ya Wabunge, na kwa kuamua kupigia debe matumizi makubwa kabisa ya serikali wakati wa amani nje ya Bunge, Rais Kikwete amejaribu (naombea bila mafanikio) kulikwepa Bunge na hivyo kuwanyima wabunge haki ya kupitia mpango mzima wa serikali.

  NI kwa sababu ninafahamu kuwa Mkullo atakaposimama atakuwa ametengenezewa njia rahisi ya kuleta bajeti hiyo ya matumizi ya serikali na mpango huu wa ajabu.

  Natumaini wabunge watasahau yote aliyoyasema Rais Kikwete na kumsikiliza Mkullo na bajeti yake na hicho pekee ndicho kiwe kipimo cha nini kinatakiwa kufanyika kukabiliana na hali ya uchumi nchini. Waipime hotuba hiyo ya bajeti, wachuje matumizi yasiyo ya lazima na ikibidi watungie sheria ya kushughulikia suala hili la matatizo ya kiuchumi badala ya kujaribu kuliingiza ingiza kwenye mipango mbalimbali kama nyongeza na mwisho wake kutengeneza mchezo wa kupoteza mabilioni ya fedha ambayo ni kawaida ya serikali.

  Wakati huu wa dharura; wabunge wetu ndio wanatakiwa kusimama kama kinga ya mwisho dhidi ya ubabe (the last defense against tyranny) wa serikali.

  Cheche wiki hii itachambua mapendekezo haya ya Rais na kuyaonesha ni kwanini kwa maneno mawili ni "wizi mtupu"! Ni mapendekezo ya mtu maskini ambaye anajifikiria ni tajiri kwa vile ati anaweza kukopa na hivyo kuanza kupanga matumizi ya kifahari ya fedha za kukopeshwa!


  Wabunge, msiburuzwe!
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  huu ustaarabu wa rais kupeleka mapendekezo kwa "wazee" kwanza sijui tumeutolea wapi.

  ikiwa tunaendeshwa na hao wazee ....bunge la nini?

  kikwete angelipeleka maelezo yake ya kuchechemua uchumi bungeni kwa kifupi na kumuacha mkullo aingie kwenye details.

  lakini kwa nnavyowajua wabunge wa ccm .......madhali kasema kikwete ndio limeshapita hilo
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Huo ujumbe more or less kautoa kwa wabunge wa CCM. He is telling them that you are either with us or against us. Anajua bajeti imeshaanza kuwekewa ngumu hata kabla haija somwa ndiyo maana anai safishia njia.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  na wabunge wa ccm walivyokuwa wazembe wataipitisha tu bajeti madhali bossi wao kikwete keshasema ipite.

  ni wakati wa wananchi wanaochagua wabunge kujiuliza .........wabunge wapo bungeni kwa maslahi ya nani?
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hilo ndilo tatizo moja la kuwa na bunge lililo jaa wabunge wa chama kinacho shika serikali.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  na ukirudi kwenye mchanganuo wake, inaonyesha kuwa kumbe 'tuna uwezo' wa kupata matrilioni ya kushughulikia matatizo. Kwa tanzania matatizo ya uchumi wa dunia yamekuja kuonmgeza tu matatizo ambayo tumeshayazoea na kuyaona kuwa sehemu ya maisha yetu. Kwa nini hatukuamua tangu zamani kuwa na mipango kama hii, ya kutafuta haya matrilioni na kuunusuru uchumi wetu? Kwa nini tumesubiri mpaka uchumi qwa dunia umeyumba na ndio tumeona umuhimu wa kufanya hivi wakati uchumi wetu siku zote unapepesuka?
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Serikali yetu ni reactive siyo proactive.
   
 8. Radical

  Radical JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2009
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 374
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  When it comes to CCM, it's always 'siasa' hata kwenye issues za high importance.

  Mabomu, siasa;
  bajeti, siasa,
  Mafisadi, siasa;
  Need I say more....?
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa Nchi za wenzetu alipaswa kuziomba pesa hizi kwa wawakilishi wetu. Nao wangeyachambua maombi haya waone kama kweli kuna haja ya kukopa, kubana matumizi, kuongeza wigo wa kodi au kuangalia upya vipa umbele vyetu. Mmewabana sana kwenye ufisadi ni lazima watafute njia ya kupata mapesa haya kwa namna yoyote ile. Iangalieni hiyo Benki ya TIB, TADB mpya, na miradi zitakakoelekezwa pesa hizi.
   
 10. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Mwanafalsafa!

  Nilishasema Rais JMK aka Matonya is not serious na ana IQ ndogo sana ameamua kuongea na wazee wa kigogo akijua hataulizwa swali hata moja na ameweza kuongea pumba tupu. Mkulo ni jambazi ni one of the GVT boys turned poiltician kama alivyo Pinda... If aliwashauri watu huko kilosa wajiunge na DECI what do you expect from that idiot.

  Matonya kazungumza upuuzi just speak it loud!!! As long as anazungumzia kupeleka billions huko TIB alikomteua Peter Noni the monster kuzisimamia tujue imekula kwetu... Hiyo mikopo ya matrekta wataishia kupewa wahindi wakanunue tillers za kichina.. He is a good dreamer huko nyuma tulianzisha CRDB (BENKI YA USHIRIKA NA MAENDELEO VIJIJINI)and we all know what happened!! Tulikuwa na THB no single house was built apart from watu kunenepeana na nyumba hazikumalizika ! Awaulize CCM what hapenned and he was a minister!! Kikwete acha usanii!!!

  Reforms haziletwi kwa kupump fedha kwenye mfumo but rather radical changes,,, Nani alimwambia tatizo la kilimo cha TZ ni ukosefu wa mbolea!!! na inaletwa kwa mtindo wa Ruzuku and for some parts of the country only ! Alivyo kilaza siajsikia pamba ambayo haijanunuliwa kwa wajameni anafanya mikakati gani!!! Angekwenda hata pale Chalinze wakulima wa mananasi pale kiwangwa wangemwambia matatizo yao badala ya kuwasikiliza akina Tyson!!!

  Kama kila mwezi wapumbavu wa EWURA wanatoa bei elekezi za mafuta which is the engine of growth hiyo mikopo italipwa vipi kama kila mwezi bei ya mafuta inapanda!! If he could think like an economist not a political onea !! angefikiria ku-inject windfall kwenye bei ya mafuta ili angalau kwa mwaka mmoja kukawa na stability ya bei!! Anawaambia mabenki wapostpone kulipwa mikopo kutoka kwa waliokopa !! Where is the analysis kwamba ni nani kakopa na akiendelea kulipa who will be affected in terms of job losses!!!! kama serikali yake imeshindwa kufix a meaningful minimum wage anazungumzia ajira zipi!!!
  Biashara kama kawaida CCM watapitisha hiyo budget kwa ujinga wao lakini wajue wanachimba makaburi yao tena wengi wao wazikwa hapo Kinondoni as usual... this is another none starter for Matonya!!! Kila la heri....
   
 11. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ni mpango wa kusikitisha kwa taifa maskini kama letuuu..
  wabunge (wa ccm) mpaka sasa sijaelewaa dhamira zao na uwezo wao vina uhusiano sawaa au ni kuendekezaa unafiki na upumbavuuu???

  mpango huu kama alivyoeleza JK umesimamiwa na Gavana katika kuandaa na hatimaye cabinet kuukubaliii!!! shame prof ndulu!! sitaki kuamini huyu ndo mmoja ya wachumi wakongwe nchinii!!!

  blah blah za jana ni nyingi na kama alivyochagua hadhira ya kuwakilisha amepata kila alichokitaka kusikilizwa kwa kusifiwa ili waleeeee...

  Waziri wa fedha alielezee bunge matumizi ya bajeti ya iliyopita yametumikaje na impact gani imepatikana..natumai wabunge makini watauliza swali hili rahisi ila lenye maana kubwaaa...vipaumbele vyetu kama elimu, barabara, maji, afya, nishati, kilimo nk pesa tulizotenga zimefanikisha nini na kwa kiasi gani?????

  Bado tatizo la budget implimentation halijitokezi kwa uwazi kwa wabunge na jamiii ka ujumla..naomba tuwe na mjadala wa kuhoji hiliii...

  Kama taifa tunahitaji kuwa makini katika vipaumbele vyetu na utekelezaji wake...
  nimeshangaa sanaa porojoo za jana zinazopelekeaa kuongezaa umaskini kwa zaidi ya 50% miaka miwili ijayoooo...
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hata mimi naona so long Mwenyekiti kasema basi bajeti imepita. Kwani yeye pamoja na kuwa mkuu wa Serikali (Rais) vile vile mkuu wa bunge. Kwani hakuna mswada wowote unaoweza kupitishwa na bunge na ukaanza kutumika bila yeye kutia mkono wake.

  nafikiri kuzuia hili ni LAZIMA KUFIKIRIA KUANGALIA UPYA KAZI ZA RAIS IKIWA NA PAMOJA NA KUMPUNGUZIA MADARAKA HUSUSAN KATIKA HII MIIMILI YA MAHAKAMA NA BUNGE.

  Lazima Mahakama na Bunge viwe vyombo huru kabisa na Serikali iwe huru bila kuingiliana katika uwajibikaji kwa wananchi.

  MABADILIKO YA KATIBA NI MUHIMU SANA.


  Umm majjid.
  Doha
   
 13. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Mkuu Mkereme, nakubaliana na wewe sana kwa maelezo yako hapo juu.

  Nilishangazwa sana kusikia Mabenki yakiombwa yasitoze riba kwa pesa za mikopo itakayoitoa. Mikopo ambayo serikali inai-guarantee kwa 20% tu tena kwa miaka miwili. Je, inflation inayoongezeka kila siku nani atakaeilipia? Naamini kabisa kuwa, baada ya hiyo miaka miwili, inflation itakuwa imefikia 20% (kwa kuwa sasa iko kwenye 15%). Ninavyoona ni kwamba, mipango yake itakuwa very temporary na yenye madhara makubwa sana kwenye Bank zetu. Ni wazi kabisa kuwa Bank zetu zitapata hasara endapo agizo hili litafanywa kama alivyosema Rais. Itabidi nianze kuondoa pesa zangu CRDB kabla haijadondoka.

  Wabunge wetu leo watajadili kidogo sana Bajeti. Watafanya hivyo kwa kuogopa kupingana na hotuba ya Rais ambayo wala hawana nafasi ya kuijadili. Hawawezi kuijadili kwasababu, muda wa kufanya hivyo haupo, na zaidi Rais amekuwa mjanja sana kuisoma nje ya Bunge akikwepa mambo mawili makubwa.

  Moja ni hotuba yake kuingia kwenye hansard za Bunge kama kumbukumbu baada ya kujadiliwa na maswali mengi kujitokeza. Maswali ambayo hakuna anaeweza kuyajibu (baadhi ya maswali hayo ni haya yanayoanza kuulizwa humu JF) kutoka serikalini.

  Pili, amekwepa kuonekana kuwa anataka ku-influence Bunge kupitisha Bajeti (kwa kisingizio kuwa alikuwa akiongea na Wazee wa Dodoma na si Wabunge peke yao). Kwa minajili hii, Bunge litakuwa na wajibu wa kuipitisha kwa kuwa ina baraka za Rais (wa chama chao), pia kwa kuwa wasipofanya hivyo, wanaweza kuhofia kupoteza mshiko wao kisiasa kwani wazee wanaweza kuwa wameikubali zaidi (hasa inapozungumzia stimulus kwa Wakulima wa Pamba, Kahawa n.k.) ambao kwake (Rais) ni watu muhimu sana kisiasa.

  Vile vile, endapo wabunge watasimama kidete na kuipinga kwa kutumia hoja za nguvu, basi watafanikiwa kuiokoa nchi. Watakuwa wameokoa nchi kwa kuwa, Rais hawezi kuamua tu kutumia mabilioni yote hayo bila ridhaa ya Bunge. Na wabunge wana wajibu wa kuipanga bajeti itakayosomwa ili iwe na manufaa zaidi ya kujenga baadhi ya watu kisiasa. Japokuwa kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha uchaguzi wa mapema zaidi.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu sina cha kuongezea. You said it all.
   
 15. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hotuba ya JK kwa wazee, inaniklumbusha enzi ya interview zilizokuwa zinaendeshwa na madiwani wa darasa la 7 kwa graduate kwenye local govt.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Huu utaratibu nadhani umeundwa kwa sababu kama angelihutubia bunge hiyo hotuba yake ingefanywa ajenda ya bunge na kujadiliwa; nahilo halikuwa lengo lake,lengo ni kuwablackmail hawa wabunge waipitishe hiyo bajeti feki kiulaini !!. Hotuba zake mara nyingi huwa hazina substance kwahiyo kuwaruhusu wabunge kuzijadili inakuwa kama kumuumbua mkuu wa nchi, kwahiyo huwa hawapendi hotuba zake zijadiliwe na kama mnakumbuka ile hotuba yake ya kwanza kwa wabunge iliwekewa mizengwe mpaka leo hii haijajadiliwa na bunge!!
   
 17. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  wazee kama wazee hawana power yoyote ya kuchallenge aliyokuwa anaongea kikwete, raisi kama angetaka kujua mtizamo wake unapokelewa vipi, angeitisha press conference kisha akaeleza mtizamo wake na kuwapa watu muda wa kuuliza maswali, lakini kwa wazee kama wale wengi wakiwa CCM hakuna kitu ambacho wangepinga...sasa tuone wabunge watakuwa na mtizamo upi kuhusu bajeti na mtizamo wa kiongozi wao, wafuata mkumbo utawaona na wanamapinduzi utawaona...
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ningewasii wabunge wetu wawe ngangali na wazalendo wanapojadili bajeti hii ama sivyo mtakuwa mnatunyonga sisi wapiga kura wenu!! Lazima muangalie priorities zitakazoisaidia nchi katika mipangilio ya miradi mingi itakayopendekezwa na mawaziri; kwa mfano katika wizara ya miundombinu, hakuna sababu zozote za kiuchumi zinazofanya kuwa uamuzi wa kujenga barabara ya lami yenye lane nne kutoka Chalinze hadi Tanga [ barabara ambayo ni ya lami anyway!]iwe na higher priority kuliko ujenzi wa barabara kutoka Tabora hadi Kigoma!! Ujenzi wa barabara hii ya kwenda Kigoma ni overdue na ni muhimu zaidi kusaidia uchumi wetu kwani utafungua sehemu yote ya magharbi ya nchi ambako kuana infinite untapped potential. Wabunge lazima wapime vipaumbele objectively na sio kupendelea sehemu wanakotoka viongozi haitatusaidia!
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wabunge wetu hawanabudi kuijadili bajeti hii bila woga wowote na waongozwe na uzalendo wa kuipenda nchi na si kujikomba kwa viongozi! Inabidi wawe makini hasa wanapojadili miradi mbalimbali ya wizara wahakikishe kuwa miradi inapangwa kufuata priorities ambazo zitaleta maendeleo kwa nchi; kwa mfano katika wizara ya miundombinu imependekezwa kuboresha barabara ya lami toka Chalinze hadi Tanga iwe na lane nne[ kumbuka kuwa barbara iliyopo ni ya lami na inapitika mwaka mzima!]; na hapo hapo kuna hii barabara ya kutoka Tabora hadi Kigoma yenye potential kubwa sana kufungua sehemu ya magharibi ya nchi yetu lakini bado inapigwa danadana! Wabunge lazima wahakikishe kuwa kuna objectivity katika ranking ya miradi na kupendelea sehemu wanakotoka viongozi kisiwe kigezo cha kupeleka miradi.
   
Loading...