Wabunge Kafumu na Kamata, wajiuzulu uongozi kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,536
Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya viwanda na biashara Mhe.Dr.Dalaly Peter Kafumu (CCM) ametoa rai ya kujiuzulu uongozi wa kamati hiyo kutokana na kutofautina sana na serikali kwenye mpango wa kuifanya Tanzania we ya viwanda na kukosa muda wa kutumikia wananchi wa jimbo lake

Dr.Kafumu ametoa rai hiyo kwenye kikao cha kwanza cha kamati ya viwanda na biashara kilichoanza leo.



IMG_4326.JPG


Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Vicky Kamata amesema kuwa ikiwa Dr.Kafumu atajiuzulu uenyekiti, naye atajiuzulu nafasi yake ya makamu mwenyekiti.

IMG_4325.JPG


SOURCE: Nimezungumza na wajumbe wa Kamati, wamedhibitisha taarifa hizo.!
 
Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya viwanda na biashara Mhe.Dr.Dalaly Peter Kafumu (CCM) ametoa rai ya kujiuzulu uongozi wa kamati hiyo, kufuatia kuandamwa na baadhi ya viongozi wa serikali kufuatia nia yake ya kumtembelea Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbless Lema alipokuwa gerezani.

Dr.Kafumu ametoa rai hiyo kwenye kikao cha kwanza cha kamati ya viwanda na biashara kilichoanza leo. Kafumu na Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Vicky Kamata walipanga kumtembelea Mhe.Godbless Lema gerezani kwa kuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Baada ya taarifa hiyo, viongozi mbalimbali walisikika kukosoa utaratibu huo na kuwaita wasaliti. Kafumu amesema haoni sababu ya wao kuitwa wasaliti kwa kuonesha nia ya kumtembelea mjumbe mwenzao wa kamati. "Mhe.Lema ni mjumbe mwenzetu wa kamati hii, kwanini ionekane ni dhambi kumtembelea alipopata matatizo?" Dr.Kafumu amewahoji wajumbe wa kamati hiyo?

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe.Vicky Kamata amesema kuwa ikiwa Dr.Kafumu atajiuzulu uenyekiti, naye atajiuzulu nafasi yake ya makamu mwenyekiti.
Tatizo ni wabunge wasiostahili kuwa wabunge. Sifa ya kujua kusoma na kuandika ni mbaya, ni mbaya, haifai. Ni sifa anayostahili kijana kuingia darasa la kwanza, siyo kuwa mbunge.

Hao wanaozomea ni wale wanaotegemea ukereketwa kupitishwa na chama. Hawana jinsi nyingine ya kuishi watokako zaidi ya kusifia CCM na hawana uwezo wa kukosoa.
 
Back
Top Bottom