mukizahp2
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 705
- 378
[h=3]WABUNGE KABLA YA UFISADI[/h]
Posted by NEW ERA LEARNING CENTER at 4/10/2013 01:46:00 PM
Kabla ya ujio wa ufisadi uliotutoa kwenye ujamaa na kujitegemea hadi kwenye unyama na kujimegea hali ilikuwa hivi yani wabunge walikuwa wanapanda gari moja (Basi) kuelekea Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
Je leo hali ikoje kwa wabunge wetu na unadhani kwa wao kuwa kama miungu watu wataweza kuwatumikia wananchi kiukweli?
Ndugu yangu hali ni mbaya na inatisha sana na sababu ni viongozi kuwa mbali na wananchi waliowapigia kura,leo hii hakuna wa kupinga ongezeko la nauli kwa mtanzania kwa sababu wamiliki wa vyombo vya usafiri ndio watoa maamuzi.
Mwananchi wa leo ana kazi ya ziada katika kuhakikisha viongozi wake wanamjali na kumthamini kwa kumtetea katika uonevu wowote na kumsaidia kuondokana na hali ngumu ya maisha na hapo ndipo ninaiona haja ya kila mmoja wetu kujihoji na kuchukua maamuzi sasa.