Wabunge jipangeni kuikosoa Serikali

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
BUNGE linatarajiwa kuanza mikutano yake Mwishoni mwa wezi huu, ikiwa ni siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani yuko tayari kukosolewa yeye na Serikali yake ili kumuonyesha maeneo yenye matatizo aweze kuchukua hatua kubadilisha dosari zilizopo.

Wabunge tunawataka mlitumie Bunge hili linaloanza Mwishoni mwa mwezi huu kubeba ajenda mahususi zinazoakisi uhalisia wa maisha ya watu mnaowangoza kwa sababu Kiongozi mliyekuwa mnafanyia unafiki kwa kumpongeza asubuhi, mchana na jioni amewastukia na kutaka akosolewe ili aweze kuona changamoto za nchi na kuzitatua.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia nawe ubadilike uliongoze Bunge vizuri liweze kuikosoa Serikali kama inavyopaswa kufanya kwani kiongozi uliyekuwa unadhani unamsaidia yeye amekataa pongezi zenu na anataka kukosolewa ili arekebishe makosa yanayowaletea shida wananchi na kusabababisha malalamiko kila kona.

Mfano kwa sasa yako matatizo mengi kwenye Ruzuku ya Mbolea, Kupanda kwa bei za bidhaa, tatizo la umeme na maeneo mengine muhimu yanayogusa maisha ya wananchi.
 
Thubutu yao! Huoni hako kamtego wanakafahamu vizuri sana kwani ye yote atakayekosoa ataingia kwenye black book na 2025 jina lake litakatwa!
 
Mzee ulikuwa Mars au 😂😂😂 maana siku hizi Dunia ni kijiji hata kama upo Kandahar ingekuwa umeshajua kama Bunge lenyewe lipo au halipo...
 
Back
Top Bottom