Wabunge hawana Kinga?

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,463
Wandugu,

Naomba ufafanuzi wa jambo hili, je wabunge wa JMT hawana kinga ki sheria inapotokea kutoelewana na vyombo vya serikali na dola wakati wa kutimiza majukumu yao? yametokea juzi tu mbunge anapigwa na police tena hawa wadogo wadogo wakati akiwa yupo kazini kuwakilisha wananchi wake waliomchagua.

kwa hali hii naamini mbunge anaweza kupigwa na kuumizwa vibaya na hata kupoteza maisha, je sheria zetu zinasemaje?

Mkuu wa mkoa ana uwezo wa kutoa amri mbunge akamatwe, apigwe na kuswekwa ndani.
Mkuu wa police wa Mkoa au wilaya pia anaweza kuamrisha mbunge akamatwe, kupigwa na kuswekwa ndani. mbunge ana kinga ipi kisheria?

Wachambuzi wa sheria naomba ufafanuzi hili la juzi limeniuma sana, kumdhalilisha mbunge namna hiyo ni sawa na kuwadhalilisha wananchi wote waliomchagua, aibu kwa nchi yetu.
 
KAKA naimani unatambuwa vizuri hii nchi na polisi wake,wabunge wanakinga ya kutambuliwa kama wabunge na utambue kuwa katiba hii isiyo na tija inawataka polisi kumhifadhi mkosaji na kumfungulia mashitaka na sio kumiga,lakini kila siku polisi wetu wakiwa na chuki na wewe ama wakipewa rushwa wao husahau sheria na katiba itakavyo na hufanya kile walichoelezwa na mtowa pesa hii ndio tz zaidi uijuavyo

wale polisi hawa kuwa na sababu za kutowa kichapo kwa mbunge bali ni kumchukuwa na kumpleka mahali husika


mapinduziiiii daimaaaa
 
nami nimeguswa sana na hili jambo la kudhalilishwa kwa mbunge wa Arusha mjini.nimeshindwa kuwaelewa kabisa hawa polisi kusudio lao lilikuwa nini.
ila tukumbuke hii sio mara ya kwanza kwani hata juzijuzi tu Zito alilalamikia polisi kumtishia bastola tena kwenye eneo la ofisi ya chama chake kigoma.
swali ni kwanini hii misukosuko na udhalilishaji unafanyika kwa wabunge wa upinzani tu tena chama kimoja?
mimi nilishapoteza imani na hawa polisi siku nyingi kwasababu hawako kwaajili ya kutulinda raia bali kuanzisha fujo na kusimamia chama chenye dola.
 
Ni kweli sheria zetu haziko wazi kwamba endapo mbunge atafanya kosa, kuburuzana na virungu ni kitendo cha utemi juu ya ubunge huyu, yaani kitendo kilichofanyika si kumkomesha Lema wala CHADEMA bali kimelidhalilisha Bunge zima la Jamhuri ya Muungano. Nategemea kusikia kauli toka ofisi za Bunge juu ya jambo hili la aibu.

Swali langu - Je kama wananchi wangechukuzwa na kitendo hicho cha mbunge wao kudhalilishwa hadharani wakaamua kuchukua sheria mkononi si maafa yangetokea? mbunge ni mtu aliyebeba watu wengi sana nyuma yake hata kama kafanya kosa kuna jia za busara zingetumika kuliko kuburuza na virungu - ni aibu kubwa kwa nchi yetu.
 
Back
Top Bottom