Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Hoja yako ni ya msingi sana. kinachoikuta CHADEMA sasa ni matatizo ya kukua kwa chama. wakati wa bunge lililopita, CDM walikuwa wachache sana bungeni, na walileta changamoto kubwa sana kwa sababu karibu wote walikuwa wanajituma. kwa hiyo kutokana na kuwa na wabunge wengi zaidi bunge hili, tulitarajia makubwa zaidi kwa ulinganifu ule ule wa bunge lililopita, kwamba kama wabunge 4 wa CDM kila mmoja aliwakilisha 10 wa CCM, basi wabune 40 wa CDM watabeba 400 wa CCM. pengine haikuwa hivyo, ijapokuwa kuna majembe yameingia bunge hili ambapo bunge lililopita hayakuwepo, na yamefanya kazi kubwa sana. lakini kuna pia mambo ya msingi ya kuangalia:
1. Chama kiwe na programu ya kuhamasisha na kuwezesha wabunge na madiwani wake. hapa ni kupitia mafunzo, kuwapa feedback juu ya utendaji wao na kila baada ya kipindi fulani, kufuatilia ahadi zao, utekelezaji wao wa mikakati ya chama katika maeneo yao.
2. kutambua kwamba umuhimu wa kwanza ni kuwajibika jimboni, wala siyo bungeni. wabunge na madiwani wanatakiwa kuwatumikia wananchi kwa kutoa huduma ya hali ya juu. hapa wanahitaji msaada kutoka kwa wapambanaji mbalimbali. mimi binafsi nilikuwa tayari kutoa msaada huo kwa mbunge wangu wa CDM, na nilitamka hivyo alipotutembelea eneo letu. lakini niliishia kupewa simu ya msaidizi wake na pamoja na jitihada zangu, sikufanikiwa kupata nafasi ya kufanya chochote. inabidi ziwekwe taratibu zitakazoruhusu wanaopenda kujitolea kusaidia chama katika shughuli mbalimbali waweze kufanya hivyo.